Ndoa ya msichana yageuka ndoto baada ya video ya utupu kuwekwa mtandaoni

Chanzo cha picha, Getty Images
Tume ya Hisbah kaskazini Magharibi mwa Jimbo la Sokoto nchini Nigeria imethibitisha kukamatwa kwa vijana watatu kwa madai ya kutuma video ya msichana akinyanyaswa kingono na mmoja wao.
Rekodi zinaonesha tarehe ya harusi ya msichana huyo ilipangwa mwezi ujao, lakini mchumba wake aliahirisha baada ya vijana hao kutoa video hiyo kwenye mitandao ya kijamii.
Mkuu wa Bodi ya Hisbah Dk.Adam Bello Asarawa aliiambia BBC kwamba mama wa msichana huyo alikuwa amewalalamikia akisema kuwa tangu 2017 vijana walimdhalilisha msichana huyo kwa kurekodi video.
''Mvulana huyo alimrubuni msichana na kumpeleka hotelini ambako alimpiga picha ya video akiwa mtupu,'' alisema Dk Adam.
Kamanda wa Bodi ya Hisbah Dk.Adam Bello Asarawa aliambia BBC kwamba mama wa msichana huyo alikuwa amewalalamikia akisema kuwa tangu 2017 vijana walimdhalilisha msichana huyo kwa kurekodi video.
"Tulimchunguza mvulana huyo na alituthibitishia kuwa jambo hilo lilitokea kwamba walikuwa hotelini na kile alichomfanyia, na kwamba tumewakamata marafiki zake wawili na pia wamedai kwamba alikuwa amewatuma.
"Kwa hivyo yeyote aliyepata video, aliipata kutoka kwa marafiki hawa wawili," kamanda alisema.
Kwanini mvulana huyo alirekodi video?
Kamishna wa Hisbah alisema kijana huyo hakutoa sababu yoyote kwanini alirekodi video hiyo na kuisambaza.
"Tuligundua tu wakati huo. Ni utoto." Nadhani alifanya hivyo kunyanyasa na kuharibu maisha ya wanawake na heshima yao, "alisema Dk Adamu.
Kamanda huyo alisema walimuuliza kijana huyo kama angemuoa msichana huyo kwani alikuwa amevuruga mipango ya ndoa yake. "Aliniambia hakuwa na nia ya kufanya hivyo, Mvulana huyo alikuwa na umri wa miaka 17 na msichana alikuwa na miaka 16 wakati wa tukio hilo.
Mvulana huyo sasa ana miaka 20 na msichana miaka 19 kwa mujibu wa rais wa Hisbara.
''wote walikuwa watoto tukio hilo lilipotokea kwa sababu hakuna aliyekuwa na miaka 20 wakati huo.''
Wazazi wa msichana walisema nini?
Amesema aliiweka video hiyo kwa miaka mitatu akiwa na nia kuwa siku moja ataitumia kumharibia ikiwa leo na kesho tabia yake itabadilika.
"Nilikuwa nimekaa mwezi Juni wakati shangazi yangu aliponiita kutoka Lagos na kumsalimia yule aliyemwona kwenye video ya utupu. Nilimwita binti yangu na kumuuliza, na akaniambia kuwa yeye pia alikuwa akisikia kutoka kwa wanafunzi wenzao.
"Kwa hivyo nikamwambia anamlaumu nani? Kisha akaniambia jina la yule kijana. Nikasema alinipa namba yake. Kisha nikaenda nyumbani kwa wazazi wake, nikamuuliza kijana huyo binti yangu alikuwa amemfanya nini maishani na akaamua kumnyanyasa?
''Akasema hakuna baya alilolifanya. Huyu hapa ni msichana kwenye video ambaye anonekana kama amelewa. Mtu yoyote anayefahamu nilichofanya kwa ajili ya binti yangu ni lazima anisaidie kulia.
"Ndipo mama wa kijana akamwita baba yake na kusema," Njoo uone mambo ambayo mtoto wako amefanya. " Ndipo baba akamtaka atuoneshe, na yule kijana akafungua video na tukaiona. "
Mama wa msichana huyo alisema baba wa mvulana kisha aliitisha mkutano wa siri, "ili isiwe jambo kubwa,'' kwa mujibu wa mama.
''Nilikwenda pia kwa Hisbah na kulalamika . Ilikuwa tarehe 17 Oktoba, lakini kijna alisema alivunja ndoa kwa sabau alitumiwa video.''
Kwa mujibu wa ripoti, baada ya msichana kuamua kuolewa na mwanaume mwingine, aliiweka video hiyo kwenye mitandao yakijamii, hali iliyosababisha mchumba akatae kumuoa.
Hali ya binti ikoje?
Mama yake amesema kuwa binti yake alikuwa na hofu kuwa hataweza kula. Hana ajira na amekuwa akilia mchana na usiku.
''Sasa tuna mpango wa kutafuta sehemu ya kumpeleka ili aweze kupumzisha akili,'' alisema.
Mama wa binti alisema nia yake ni kuona kuwa aliyehusika na tukio hilo anawajibishwa.
Adhabu gani itampata kijana huyo na marafiki zake?
Kamanda wa Hisbah alisema kuwa suala hilo litapelekwa mbele ya NAPTIP kuangalia sheria zilizowekwa katika sehemu inayohusiana na kukiri uhalifu kwa watoto.
"Tuligundua tu wakati huo. Kisha tukawasiliana na Bodi ya Udhibiti wa uhariri wa video na filamu ili nao wafanye kazi yao.
"Ikiwa watafanya jambo sahihi, basi kutakuwa na kesi." Na sababu ya marafiki hao wawili kujumuishwa kwa sababu wana hatia ya kueneza picha za utu












