Waziri wa Uganda akamatwa na polisi baada ya kufyatua risasi zinazodaiwa kuua

Waziri Mwesigwa Rukutana alichukua bunduki kutoka kwa mlinzi wake na kufyatua risasi upande wa wapinzani wake

Chanzo cha picha, Daily Monitor/Uganda

Maelezo ya picha, Waziri Mwesigwa Rukutana alichukua bunduki kutoka kwa mlinzi wake na kufyatua risasi upande wa wapinzani wake
Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 2

Polisi nchini Uganda imemkamata na kumuweka mahabusu Naibu waziri wa kazi nchini humo Mwesigwa Rukutana kufuatia tukio ufyatuaji wa risasi katika eneo la Ruhama wilayani Ntungamo, ambapo mtu mmoja ameuawa.

Walinzi wake watatu pia wamekamatwa na polisi.

Waziri Mwesigwa Rukutana amekamatwa na jeshi la polisi baada ya picha za video zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii jana Ijumaa zilizoonesha akichukua silaha kwa mlinzi wake na kuwafyatulia risasi dhidi ya wampinzani wake.

Waziri Rukutana

Chanzo cha picha, Mitandao ya kijamii

Risasi hizo ziliangukia kichwani Dan Rwiburingi ambaye inayesemakana amefariki dunia leo alipokua akipata matibabu hospitalini.

Picha kadhaa pia zimekua zikisambazwa kwenye mitandao ya kijamii zikionesha Bwana Rukutana akishikilia bunduki. Pia kuna picha zinazoonesha muathiriwa wa shambulio hilo:

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe

Tukio hilo lilitokea wakati wa kampeni za kuwania kiti cha ubunge jimbo la Rusheni wilayani Ntugamo magharibi mwa Uganda kwa tiketi ya chama tawala cha NRM.

Kulingana na Matokeo yaliyotolewa jana wilayani waziri Rukutana alipoteza kiti cha ubunge ambacho kilichukuliwa na mpinzani wake Naome Kabasharira.

Mawaziri 10 katika serikali ya rais Museveni wamepoteza viti katika kura za mchujo za chama

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Mawaziri 10 katika serikali ya rais Museveni wamepoteza viti katika kura za mchujo za chama

Katika uchaguzi huo zaidi ya mawaziri 10 katika serikali ya rais Museveni wamepoteza viti katika kura za mchujo wa chama, ambapo kampeni za uchaguzi huo zimekua zikigubikwa na ghasia, vitisho na rushwa kwa wapiga kura.

Kulingana na Mwandishi wetu wa Kampala polisi walipelekwa katika wilaya za magaharibi mwa Uganda kusaidi kuimarisha usalama ulinzi kufuatia ghasia.