Mawimbi ya mgongano wa mashimo mawili meusi angani yaripotiwa duniani miaka bilioni 7 baadaye

Iliyochapishwa

Fikiria nishati nane za jua zikiachiliwa kwa mpigo. Hili ndilo wimbi la"mshtuko" wa mvuto uliosambaa baada kushikana kwa mashimo mawili meusi angani.

Athari ya mshikano huo ilisafiri kwa takriban miaka bilioni ili kufika ardhini na bado zilikuwa na nguvu kuyumbisha vifaa vya kutambua mwanga nchini Marekani na Itali mnamo mwezi Mei mwaka uliopita.

Watafiti wanasema kwamba mgongano wa mashimo hayo mawili ulisababisha kitu kimoja chenye uzani ulio mara 142 zaidi ya ule wa jua.

Wanasanyi kwa muda mrefu wamekuwa wakifuatilia uwepo wa mashimo meusi angani ambayo ni madogo na hata makubwa.

lakini ugunduzi huu mpya unaleta tabaka jipya la mashimo meusi yalio na ukubwa wa kadri na uzito wa kati ya mara 100 - 1000 zaidi ya jua.

Uchambuzi huo ndio wa hivi karibuni kutoka kwa kituo cha kimataifa cha LIGO-VIRGO, ambacho kinasimamia mifumo mitatu ya kutambua mawimbi ya mvuto nchini Marekani na Ulaya.

"Inashangaza, kweli," alisema prof Nelson Christensen kutoka Côte d'Azur Observatory huko Ufaransa. "athari za Wimbi hilo zilisambaa kwa miaka bilioni saba.

Kwa hivyo tukio hili lilitokea 'kabla ya nusu' ya kuundwa kwa Ulimwengu, na sasa limewahamisha wapelelezi wetu hapa Duniani," aliambia BBC News.

Algorithms au mahesabu ya kompyuta zilibaini chanzo kuwa wakati wa mwisho wa mgongano wa mashimo mawili meusi yanayozunguka - moja lenye uzani wenye ukubwa mara 66 kuliko ule wa Jua letu, na jingine lenye uzani mkubwa mara 85 zaidi ya jua.

Umbali wa mshikamano wa mashimo hayo meusi ulidaiwa kuwa kilomita bilioni trilioni 150.

Kuhusika kwa kitu chenye uzito mara 85 ya jua letu kwenye mgongano kumewafanya wanasayansi wa kushirikiana kukaa chini kwa sababu uelewa wao wa jinsi mashimo meusi hutengenezwa kufuatia mlipuko wa nyota hawawezi kuwajibikia kitu kwa kiwango hiki.

Nyota zinapomaliza uwezo wake hulipuka na kusababisha shimo jeusi - iwapo ni nyota kubwa.

Lakini fizikia inayodhaniwa kufanya kazi ndani ya nyota inaonyesha uundaji wa mashimo meusi katika tabaka fulani kati ya uzani wa mara 65 au 120 zaidi ya jua haiwezekani.

Nyota kama hizo hulipuka na kuangamia na haziachi chochote nyuma.

Ikiwa sayansi inasema ukweli kuhusu hatua hii basi maelezo sahihi kuhusu uwepo wa kitu chenye uzani mara 85 zaidi ya jua ni kwamba kilitokana na mshikamo wa mashimo mawili meusi.

Na hiyo, anaamini Prof Martin Hendry, kutoka Chuo Kikuu cha Glasgow, Uingereza, kwamba ina athari kuhusu jinsi Ulimwengu ulivyoumbwa.

"Tunazungumza kuhusu miungano, njia inayowezekana kutengeneza mashimo meusi makubwa na makubwa," alisema. "Kwa hivyo, nani anayejua? Shimo hili jeusi-lenye umbo la jua lenye uzani ulio zaidi ya mara 142 ya jua linaweza kuendelea kuungana na mashimo mengine makubwa meusi - kama sehemu ya mchakato wa kujenga ambao huenda hadi kwenye mashimo meusi makubwa ambayo tunadhani yapo katikati ya sayari.

Picha kwa hisani ya