Mwanamke Mfaransa akamatwa baada kwa kuchuchua video akiwa mtupu eneo takatifu

Iliyochapishwa

Mwanamke Mfaransa amekamatwa nchini India kwa kutengenea video yake akiwa uchi kwenye daraja takatifu lililoko katika mji wa kaskazini wa Rishikesh.

Video hiyo iliyochukuliwa mkwenye daraja la Lakshman Jhula ilitumwa kwenye mitandao ya kijamii.

Mwanamke hyo sasa anakabiliwa na mashitaka chini ya sharia ya intaneti ya India , na anaweza kufungwa hadi miaka mitatu jela iwapo atapatikana na hatia , limesema shirika la habari la AFP.

Daraja hilo linalopita juu ya mto Ganges ambao ni eneo takatifu na eneo maarufu sana kwa watalii.

Mwanamke huyo ambaye baadae aliachiliwa kwa dhamana, aliwaambia polisi kuwa video hiyo ilitengenezwa kwa ajili ya kunadi biashara yake ya vipuli vya urembo.

"Labda Ufaransa haya mambo hayapingwi. Lakini Rishikesh ni eneo takatifu na Lakshman Jhula ni eneo ambako miungu ya Hindu Ram, kaka yake Lakshman na mke wake Sita walipita mto Ganges," RK Saklani, mkuu wa kituo cha polisi ambako mwanamke huyo alipelekwa aliliambia shirika la habari la AFP.

Mwanamke huyo ambaye utambulisho wakehaujatangazwa rasmi, alikamatwa siku ya Alhamisi baada ya polisi kufahamishwa juu ya picha zake za video.

"Wakati wa kuhojiwa na polisi, alikiri kuwa alipiga video hiyo ya uchi lakini akadai hakufahamu kuwa kupiga picha za aina hiyo ilikuwa ni kinyume na sharia nchini India.

Alisema kuwa alipiga picha na video kwa lengo la kunadi biashara yake ya mikufu ya shanga ," afisa mwingine wa polisi aliliambia gazeti la India Hindustan Times.

Kesi hiyo inaweza kuchukua miezi kadhaa kabla ya hukumu kutolewa.