Ligi za NBA, MLS zaahirisha michezo nchini Marekani kupinga kitendo cha Jacob Blake kufyatuliwa risasi

Workers remove items from the Milwaukee Bucks' bench area after they boycott an NBA play-off game

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mipira na taulo viliondolewa kwenye mabenchi yanayokaliwa na wachezaji viwanjani wakati wa Bucks
Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 2

NBA imeahirisha michezo mitatu siku ya Jumatano baada ya Milwaukee Bucks nao kusitisha michezo ili kupinga kitendo cha kufyatuliwa risasi Jacob Blake.

Blake, mwanaume mweuksi alipigwa risasi mara saba mgongoni na polisi siku ya Jumapili mjini Kenosha

Upande wa mpira wa magongo michezo mitatu ya ligi ya MLB imeahirishwa baada ya timu kuamua kutocheza, na michezo ya ligi kuu ya soka Marekani MLS pia zimeahirishwa.

Mchezaji wa Tenisi Naomi Osaka amejiondoa kwenye mechi ya WTA siku ya Alhamisi.

Aliandika kwenye ukurasa wake wa twitter kuwa hatacheza mechi ya nusu fainali ya michuano ya wazi ya Western na Southern jijini New York, akisema kuwa ''kama mwanamke mweusi ninahisi kama vile kuna masuala muhimu yanayohitaji kufanyiwa kazi haraka, kuliko kunitazama mimi nikicheza tennis''.

Chama cha mpira wa tenisi Marekani, ATP na WTA pamoja vilitangaza kuwa wanaahirisha michuano ya Western na Southern Open siku ya Alhamisi na kuwa itarejea tena siku ya Ijumaa, ikiongeza kuwa ''Tenisi kwa pamoja inachukua msimamo mmoja dhidi ya vitendo vya ubaguzi na kutokuwepo kwa usawa na haki.''

Baada kuahirisha mchezo wao dhidi ya Orlando Magic, wachezaji wa Bucks walitoa taarifa wakisema: ''Pamoja na kuwepo kwa wito wa kufanyika mabadiliko, hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa, hivyo leo mchezo wa mpira wa kikapu hauwezi kuwa kitu cha kukiangazia.''

''Tunatoa wito Jacob Blake apate haki yake na tunataka maafisa wawajibishwe.''

Mchezo wa Houston Rockets dhidi ya Oklahoma City, Thunder na Los Angeles Lakers na Portland Trail Blazers pia ziliahirishwa, ratiba za mechi hizo zitapangwa tena.

Imeripotiwa kuwa wachezaji wa NBA watakutana kujadili kuhusu kuendelea kwa michezo hiyo iliyoahirishwa.

1px transparent line

Milwaukee Brewers na Cincinnati Reds pia wameahirisha mchezo wa nyumbani wa ligi ya mpira wa magongo MLB uliokuwa uchezwe siku ya Jumatano.

''Wachezaji wa Brewers na Reds wameamua kutocheza usiku huu mchezo wa mpira wa magongo,'' ilieleza taarifa iliyotolewa na Brewers.

Ruka X ujumbe, 1
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 1

1px transparent line

''Wakati jumuia yetu na taifa liko kwenye maumivu, tulitaka kuelekeza fikra zetu kwa masuala ambayo kwa kweli yanafaa kushughulikiwa hasa ubaguzi na ukandamizaji.''

Mahasimu wa California San Francisco na Los Angeles Dodgers waliahirisha ratiba ya mchezo wao na kutoa taarifa ya pamoja kuwa: '' Wakati wote wa historia ya nchi yetu, michezo imekuwa chombo muhimu cha mabadiliko.

Ligi ya wanawake ya mpira wa kikapu nchini Marekani, WNBA imeahirisha michezo mitatu iliyotakiwa kuchezwa mji wa Bradenton, jimbo la Florida siku ya Jumatano.

Wachezaji walivaa tisheti zanye jina la Blake zilizokuwa na matundu ya mfano wa risasi, kuwakilisha idadi ya risasi alizofyatuliwa Blake na polisi.

''Tunasimama pamoja na kaka zetu wa NBA na tunaendelea na mazungumzo na kaka na dada zetu katika ligi zote ili kutazama hatua ya pamoja ya kuchukua,'' alisema mchezaji wa Atlanta Dream Elizabeth Williams alipowasilisha taarifa kwa niaba ya wachezaji wa WNBA.

Rais wa zamani wa Marekani, Barack Obama, ambaye ni mshabiki kindakindaki wa mchezo wa mpira wa kikapu, aliunga mkono uamuzi wa ligi na timu mbalibali za mchezo huo kukemea vitendo vya polisi .

Ruka X ujumbe, 2
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 2

1px transparent line

Kabla ya mchezo uliokuwa umepangwa, Kocha wa Bucks Mike Budenholzer amesema: ''Mimi, wachezaji wangu na taasisi tumefadhaishwa sana na kile kilichotokea Kenosha.