Benjamin William Mkapa: Matukio mbalimbali katika picha

Chanzo cha picha, IKULU TANZANIA
Benjamin Mkapa aliliongoza taifa la Tanzania kwa miaka 10 baada ya uchaguzi wa kwanza wa kuhusisha vyama vingi mwaka 1995.
Alipokea madaraka kutoka kwa Rais wa pili, Ali Hassan Mwinyi ambaye alibadili sera ya uchumi ya nchi kutoka kwenye ujamaa.
Lakini pia alikuwa Mkapa aliyefanya mabadiliko muhimu yaliyofanya nchi kungia kwenye mapinduzi ya kiuchumi.

Chanzo cha picha, IKULU TANZANIA
Hata baada ya kuondoka madarakani, Bwana Mkapa alifahamika katika kuongoza jitihada kadhaa za upatanishi katika ukanda wa Afrika, ikiwemo kusimamia kupatikana kwa amani nchini Kenya wakati wa vurugu za baada ya uchaguzi mwaka 2008.

Chanzo cha picha, Getty Images
Pia aliongoza mazungumzo ya upatanishi nchini Baurundi kati ya Serikali ya nchi hiyo na upinzani mwaka 2016 yaliyokuwa na nia ya kumaliza mzozo wa kisiasa wa muda mrefu.

Chanzo cha picha, Getty Images
Baada ya kustaafu, Benjamin Mkapa kwa namna moja au nyingine alikua mpatanishi wa mazungumzo ya amani ya DRC, Zimbabwe, Sudani Kusini na Burundi. Hayati Mkapa alifanya jitihada za kuhakikisha kuwa Afrika inakuwa sehemu nzuri ya kuishi.
Rais Mkapa alisomeshwa elimu yake ya msingi na sekondari na mamishionari wa Kikatoliki, na kwa maisha yote amekuwa muumini wa madhehebu hayo.

Chanzo cha picha, Getty Images








