Ndege ya kampuni ya Ryanair yabadili mkondo baada ya 'ilani ya bomu' kupatikana msalani

Ndege ya kampuni ya Ryanair yabadili mkondo baad ya ilani ya bomu kupatikana msalani

Chanzo cha picha, ABDUR RAHMAN MASHAL

Maelezo ya picha, Ndege hiyo ilipelekwa katika eneo la mbali la uwanja huo wa ndege kabla ya abiria kushukishwa.
Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 1

Ndege moja iliokuwa ikitoka Krakow kuelekea mjini Dublin ililazimika kutua kwa ghafla baada ya ilani moja iliokutwa ndani ya choo kudai kwamba kulikuwa na vilipuzi ndani ya ndege hiyo.

Ndege hiyo ya kampuni ya Ryanair ilibadili mwelekeo hadi katika uwanja wa ndege wa Stansted ambapo maafisa wa polisi wa Essex wanaikagua.

Ndege mbili za kijeshi aina ya RAF Typhoon ziliisindikiza ndege hiyo ambayo ilitua mwendo wa saa kumi na mbili .

Msemaji wa ndege hiyo alisema: Ndege hiyo ilitua vizuri lakini ilipelekwa hadi katika eneo la mbali ambapo abiria walishuka salama.

Kanda ya video ya RAF ilikuwa ikisambazwa.

Andy Kirby , kutoka Essex alisema: Inaonekana kama ndege za kijeshi za eurofighters zilikuwa zikizunguka juu ya nga ya uwanja wa ndege wa Stansted."

Transparent line
Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe

Transparent line

Msemaji huyo wa Ryanair aliongezea katika taarifa kwamba: Ndege hiyo na abiria wake wanachunguzwa na maafisa wa polisi wa Uingereza ambao wataamua iwapo wataendelea na safari yao ya kuelekea mjini Dublin kwa kuabiri ndege nyengine.

Abiria mjini Dublin wanaosubiri kuelekea Krakow wanaingizwa katika ndege tofauti ili kupunguza uwezekano wa kuchelewa .

Maafisa wa polisi wa Essex walisema: Tumefanikiwa kuwatoa abiria wote kutoka katika ndege hiyo.

''Ndege hiyo hadi kufikia sasa imetengwa katika uwanja wa ndege wa Stansted na uchunguzi wetu unaendelea''.