Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Virusi vya corona: Wanawake ambao hawawezi kuavya mimba katika wakati wa amri ya kukaa nyumbani
Amri ya kitaifa ya kutotoka nje imeyafanya maisha ya wanawake wa India wanaojaribu kupata huduma salama za kutoa mimba kuwa magumu limeripoti jarida la Menaka Rao.
Katika wiki ya mwisho ya mwezi Mei, msichana mwenye umri wa miaka 20 mwanafunzi wa chuo katika mji mkuu wa India , Delhi, aligundua kuwa ana ujauzito.
Mwanamke , Kiran, ambaye jina lake limebadilishwa kulinda utambulisho wake, alikua tayari amemeza tembe za kuavya mimba baada ya kushauriwa hivyo na rafiki yake ambaye alikua daktari. Lakini tembe hazikufanya kazi na kwahiyo, chaguo pekee lililokua limesalia ni kufanyiwa upasuaji kutoa mimba
India, hatahivyo, ilikua chini ya agizo la watu kutotoka nje ili kukabiliana na kusambaa kwa virusi vya corona kuliko nchi nyingine yoyote duniani, ilisitisha usafiri wa anga, treni na basi na watu waliagizwa kubaki majumbani mwao wakati wote iwezekanavyo.
Ingawa hospitali zilifungua milango, ziliagizwa zitoe huduma muhimu tu. Kwahivyo hospitali kubwa nyingi zilifunga huduma za idara za matibabu ya wagonjwa wanaokuja na kwenda na kufunga upasuaji wa kielekroniki.
Huku dawa za kuzuwia ujauzito na uaviaji mimba zilihesabiwa kama huduma muhimu, amri ya kutotoka nje ilifanya hali kuwa ngumu kwa wanawake wanaotaka huduma za afya ya mausuala ya afya ya uzazi na ngono.
Kwa mujibu wa utafiti wa hivi karibuni, mimba zipatazo milioni 1.85 zipo katika uwezekano mkubwa wa kuathiriwa nchini India na Covid-19
Inakadiriwa kuwa mimba milioni 15.6 hutolewa nchini India kila mwaka.
Hii itamaanisha wanawake wanaofanyiwa upasuaji kwasababu ya kuchelewa kupewa tembe za kuavya mimba au mimba zisizokusudiwa ni mambo yanayowalazimisha wanawake kufanya kutoa mimba kwa njia zisizo salama.
Mchakato duni
" Wakati mkasa unapotokea , hakuna mtu anayezungumza juu ya ngono na afya ya uzazi ," alisema Jasmine Lovely George, anayeendesha kituo cha Hidden Pockets, jukwaa linalosaidia kubporesha upatikanaji wa huduma za afya ya uzazi. Alisema kwamba shirika lakelilishuhudia ongezeko la juuu la simu za wanawake wanaoomba usaidizi wakati wa amri ya kutotoka nje.
Hata kununua kununua kipimo cha utambuzi wa ujauzitpo ilikua ni vigumu kwa baadhi ya wanawake kwani walikuwa wamekwama majumbani mwao, alisema.
" Wanawake wengi walikua ima nyumbani baada ya kufungwa kwa vyuo, au wakifanyia kazi nyumbani. Tuliasikua kuwa kawaida alikua ni baba ambaye alikua akiytoka nje, na kile ambacho waliweza kuomba ilikua ni vitambaa vya usafi ."
Madaktari na wanaharakati wa masuala ya afya katika miji mbali mbali nchini India walisema kuwa walikua wamepokea simu za kuomba usaidizi kutoka kwa wanawake ambao walikua hawawezi kupata huduma salama ya kuavia mimba zao.
Baadhi yao hata walisema kuwa wanafahamu matukio mengine ambapo wanawake waliokuwa wakitaka huduma ya kutoa mimba walifukuzwa kutoka hospitali, au waliambiwa warudi baadae, jambo lililowalazimisha kuavia mimba kwa njia ya upasuaji.
Dkt Suchitra Wadhwa wa Jumuiya ya Mpango wa uzazi wa famili jijini Delhi alisema kuwa alipata simu kutoka Delhi , na jimbo jirani la Uttar Pradesh zilizopigwa na wanawake waliokua wakitaka huduma za matibabu zinazohusiana na uaviaji mimba. Lakini hakufanya hivyo kwasababu ni kinyume cha sheria kwa daktari kutoa huduma ya uaviaji mimba bila kusajiri huduma hiyo , na wao wenyewe huwa hawahisi vyema kufanya hivyo.
"Nilisikia visa ambapo wanawake walioomba mimba zao zitolewe katika hospitali za serikali mjini Mumbai katika muhula wa kwanza wa ujauzito wao walifukuzwa. Madaktari waliwaambia wasubiri warudi baada ya wiki chache baadae . Tulilazimika kuwatafuta madaktari wengine ambao wangewasaidia wanawake hawa ," Alisema Dkt Shilpa Shroff, anayefanya kazi na taasisi ya uaviaji mimba salama Asia - Asia Safe Abortion Campaign.
Na hali ilikuwa hata ngumu zaidi kwa wanawake maskini, na wale wanaoishi maeneo ya vijijini nchini India.
Lakini kliniki ya Bi Rao' haikuwa na kibali cha kushughulikia uaviaji mimba za muhula wa kwanza wa ujauzito
"Alikasirika sana na alikua analia. Tulimuagiza aendende kwenye hospitali ya serikali iliyopo karibu, tukifahamu vizuri sana kwamba watamwambia aondoke bila huduma. Wengi wa wateja wetu walilalamika juu ya kutohudumiwa ," Bi Rao alisema.
Katika kijiji cha Jharkhand kilichopo katikati mwa India, kiongozi wa vijana , Anki Kasma Turi, alisema kuwa alijitahidi kuwasaidia wanawake wawili waliokua wakitafuta huduma ya kuavia mimba katika wiki ya pili ya mwezi Machi , hata kabla ya ya kutelekezwa kwa amri ya ''lockdown'' nchini India.
Lakini walirudishwa wakati amri ya kutotoka nje ilipoanza kutekelezwa. Mmoja wa wanawake hao alikua na watoto watatu, na mwingine alikua na watoto wanne.
"Wengi ni jamii za wakulima na hawakutaka kuwa na watoto zaidi. Sasa wanalazimika kuendelea na ujauzito wao ," Bi Turi anasema.
Unaweza pia kusoma:
Tatizo linaendelea
Ingawa amri ya kutotoka nje ya kitaifa imeondolewa, watu bado wanaendelea kufanyia kazi nyumbani nchini India, na vyuo vyote bado havijafunguliwa. Miji mingi- kama vile Bangalore na Chennai - vimeweka sheria ya kutotoka nje huku idadi ya visa vya maambukizi vikiongezeka na miji zaidi inaweza kuchukua hatua sawa na hiyo kwani hali ya janga la corona inaendelea kuwa mbaya katika miji tofauti.
Mjini Delhi, Kiran hatimae aliwasiliana na Inayat Kakar, mtafiti wa masuala ya afya, ambaye pia ni sehemu ya kikundi cha wataalamu wa afya ya umma, kinachowasaidia watu kupatra huduma za matibabu.
"Wazazi wake walikuwa na wasi wasi mkubwa juu ya maambukizi ya Covid-19 na hawakumruhusu atoke nje si kwa muda mrefu ambao aliuhitaji kumuona daktari ," Bi Kakar anasema.
Kiran hatimae aliwaambia wazazi wake kuhusu ujauzito wake, lakini bado walipata ugumu wa kumpata daktari kwani ujauzito wake ulikua tayari umepita wiki 14-15, na alikuwa karibu afikie kiwango cha mwisho cha wiki ya 20- ambazo ni ukomo unaokubalika kwa mujibu wa sheria ya India ya utoaji mimba.
"Mama yake aliwapigia simu madaktari kadhaa wa wanawake. Tuliwaita madaktari kadhaa wa wanawake, lakini hatukufanikiwa. Baadhi walipandisha gharama zao hadi 70,000 rupia ($933;£738) kwa utoaji mimba ," Bi Kakar alisema.
Kutokana na wasiwasi na hofu inayozingira Covid-19, imekua ni vigumu kuelewa ni kiliniki gani na hospitali zinazofanya kazi na ni zipi hazoifanyi kazi, alisema Dkt Sana Contractor, ambaye amewasaidia wanawake kadhaa kupata huduma ya salama za uaviaji mimba.
Alikua ni yeye na wenzake katika kikundi cha usaidizi wa matibabu ambao hatimae walimsaidia Kiran kumpata daktari ambaye anaweza kuavia mimba yake salama.
Lakini si wanawake wote wenye bahati hiyo.