Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Uefa Champions League: Manchester City kushiriki kombe la Ulaya baada ya mahakama kufuta marufuku ya miaka 2
Klabu ya Manchester imefanikiwa kubadili marufuku ya miaka miwili kushiriki katika mashindano ya klabu bingwa Ulaya kuanzia msimu ujao.
Mahakama ya kutatua mizozo ya michezo ilitangaza kwamba klabu hiyo imeondolewa makosa ya ya kifedha chini ya sheria ya Fifa siku ya Jumatatu.
Bodi ya kudhibiti matumizi ya klabu za Uefa CFCB ilitoa marufuku hiyo Februari baada ya City kukiuka sheria ya Financial Fiar Play FFP kati ya 2012 na 2016.
Faini ya City ya yuro milioni 30 sasa imepunguzwa hadi yuro milioni 10.
Ikitoa uamuzi huo siku ya Jumatatu, mahakama hiyo ilisema kwamba licha ya City kukataa kushirikiana na mamlaka ya Fifa ,ilifutilia mbali uamuzi wa shirika hilo la kudhibiti matumizi ya kifedha katika ligi ya Uefa.
City imesema kuwa uamuzi huo unahalalisha msimamo wa klabu hiyo na ushahidi uliotoa mbele yake.
''Klabu hii ingependelea kuwashukuru wanachama wa jopo hilo kwa uamuzi walioutoa'', City iliongezea.
Uamuzi huo una maana kwamba City ambayo ina hakika kwamba itamaliza katika nafasi ya pili katika ligi ya Premia msimu huu itashiriki katika kombe la klabu bingw Ulaya 2020-21.
Katika mashindano ya mwaka huu, kikosi hicho cha Pep Guardiola kitaminyana na Real Madrid katika robo fainili ya michuano hiyo katika awamu ya pili mechi itakayochezwa katika uwanja wa Etihad tarehe 7 mwezi Agosti .
Wanaongoza 2-1 kutoka awamu ya kwanza na watacheza dhidi ya Juventus au Lyon iwapo wataibuka washindi.
Je City ilikuwa inashtakiwa na nini?
Uefa ilianzisha uchunguzi baada ya gazeti la Ujerumani Der Spiegel kuchapisha nyaraka zilizovuja mnamo mwezi Novemba 2018 likidai kwamba City iliongeza thamani makubaliano ya ufadhili na hivyobasi kudanganya shirika la soka barani Ulaya Uefa.
Ripoti zinadai kwamba City ambayo imekana kufanya makosa yoyote iliidanganya Uefa kimakusudi ili kuweza kuafikia sheria za FFP ambayo inataka klabu kufanya usawa.
Je nini kitarajiwe?
Uefa huenda ikakata rufaa dhidi ya uamuzi huo katika mahakama ya Uswizi.
Hatahivyo haiwezekani kwamba rufaa kama hiyo itasikilizwa kabla ya michuano ya klabu bingwa ya 2020-21 .
Ligi ya Premia ingechukua hatua iwapo marufuku hiyo ingeidhinishwa kwasababu sheria zake za FFP zinafanana na zile za Uefa lakini sio moja kwa moja.