Je uvumbuzi huu ndio suluhu ya misururu mirefu inayopatikana katika vyoo vya wanawake?

Nathalie Des Isnards

Chanzo cha picha, La Voix du Nord

Maelezo ya picha, Milolongo mirefu katika vyoo vya wanawake ndio iliomshinikiza Nathalie Des Isnards kuanza biashara ya vyoo vya wanawake
Iliyochapishwa

Miaka michache iliyopita, Nathalie des Isnards aliondoka na mumewe David hadi katika tamasha la muziki ili kuona kundi lake la muziki analolipenda.

Kabla ya tamasha hilo, walikwenda haja ndogo. ''Nilipoteza takriban dakika 30 nikisubiri kwenda haja ndogo, anakumbuka. Alikasirika sana baada ya kukjosa awamu ya kwanza ya tamasha hilo.

David kwa upande wake , alitumia dakika mbili na alifanikiwa kuona tamasha lote.. Nilikasirika.

Nilijiambia, tuko katika karne ya 21 , kitu kinahitaji kufanywa kuhusu suala hili.

Hivyobasi alifikiria kutengeneza kifaa ambacho mwanamke anaweza kutumia kwenda haja ndogo.

Alitengeneza bakuli lisilo na kiti ambalo lina mlango na paa, litakaloweza kutumiwa kwa urahisi lakini pia kwa matumizi binafsi.

Licha ya ubunifu kama huo, wanawake wanaendelea kusimama kwenye mstari mrefu kwasababu kulingana na maoni ya Des Isnard 'hakuna aliyejali'.

Hatahivyo anaamini kwamba ni kutoa hamasa kuhusu tatizo hilo kupitia mitandao ya kijamii mbali na ushindani mkubwa miongoni mwa maandalizi ya matamasha kama hayo.

''Hii hufawanya wao kutoa huduma bora '', anaelezea.

''Zaidi ni kwamba waandaaji wamegundua kwamba muda ambao wanawake hutumia kupanga mstari ni muda mwingi''.

Kulingana na Des Isnards, wanawake 100,000 walitumia uvumbuzi wao , kwa jina madamePee, mwaka uliopita katika hafla 15 nchini Ufaransa , ikiwemo kombe la Dunia .

''Unawafaa wanawake wote sio tu wale wanaofahamu uvumbuzi''.

choo cha madampee

Chanzo cha picha, MadamePee

Maelezo ya picha, MadamePee anahisi kwamba vyoo hivyo vya wanawake vitapunguza tofauti ya muda unaotumia na wanaewake ukilinganisha na wanaume

Vifaa viwili tayari vimewekwa mjini Paris ili kuwahudumia raia.

Lengo ni kuhakikisha kwamba kuna usawa kwamba kila mara kunapokuwa na choo cha wanaume kuna choo cha wanawake, kulingana na mfanyabiashara huyo wa Ufaransa.

Mjini Copenhagen, msanifu Gina Périer na Alexander Egebjerg waliunda choo cha Lapee, choo cha wanawake kilicho na kifaa kinachoweza kutumika tena baada ya kuoshwa.

''Ni kizuri kinarahisisha mambo mengi'', alisema Perrier mwenye umri wa miaka 25. Wazo hilo lilijitokeza wakati walipokuwa wakijitolea katika Tamasha maarufu la Roskilde.

''Sikufikiria kwenda katika tamasha ama hafla ya michezo bila kifaa cha wanaume kukojolea kila mahala'', alisema Egebjerg mwenye umri wa miaka 29.

''Hakuna sababu kwanini wanawake hawana choo hata kidogo''.

Kulingana na utafiti wake , asilimia 90 ya mililongo mirefu ya kwenda msalani ni ya kwenda haja ndogo.

Kundi hilo linadai kwamba inachukua sekunde 30 kutumia Lapee, huku katika choo cha kawaida inachukua kati ya dakika moja hadi mbili .

Chini ya kifaa hicho ni pipa la litre 1,100 linalohifadhi mikojo hiyo baada ya watu 3,500 kwenda haja.

Choo hicho hakina milango lakini nyuta zilizojipinda zinawalinda watumiaji wake kutoonekana nje.

''Huwezi kupata wanawake waliozoea vyoo hivyo ni changamoto'', lakini Perrier anasema wanapenda muundo wake.

''Tunapokea ujumbe mwingi katika Instagram inayosema Ahsanteni'', anasema.

Lapee

Chanzo cha picha, Eric Delafosse

Maelezo ya picha, Wavumbuzi a La pee wanasema kwamba choo hicho kimerahisisha mambo

Gail Ramster, mchunguzi mkuu katika chuo cha Royal College of Art an wasiwasi kuhusu vyoo hivyo vya wanawake.

''Kuanza kutumia vyoo hivyo ni changamoto kubwa katika mabadiliko ya tabia'', anasema. ''Masuala kama nguo na faragha yanaweza kuwa tatizo kwa wanawake''.

Baadhi ya watu wamevitumia katika matamasha na wamefanikiwa, lakini sidhani kwamba vinaweza kusambazwa zaidi ya maeneo kama hayo, nina hofu zangu.

Wanawake huchukua muda mrefu katika vyoo zaidi ya wanaume kutokana na masuala ya kibaiolojia, kijamii na kimaumbile, uangalizi wa watoto na hata mavazi. Hayo ni mambo hayazingatiwi wakati watu wanapotengeza vyoo.

Tamasha la Hellfest 2019

Chanzo cha picha, MadamePee

Maelezo ya picha, Utafiti umebaini kwamba wanawake huchukua muda mrefu zaidi wanapokwenda chooni zaidi ya wanaume