Kwa nini kufiwa na mwenza kunamaanisha kuwa na njaa?

woman in graveyard

Chanzo cha picha, Katie Horwich

Iliyochapishwa

Kwa kawaida kifo cha mtu uliyefunga nae pingu za maisha huwa kinasikitisha sana, lakini baadhi ya taratibu za kimila zinazofanyika katika maeneo mbalimbali duniani zinaweza kumfanya mjane kuumia hata zaidi -hususan inapokuja katika suala la vyakula kama anavyoripoti Emily Thomas.

Katika baadhi ya tamaduni, wajane hutengwa wakati wa muda wa chakula, wanazuiwa kula vyakula vitamu, na hata kulazimishwa kushiriki katika ulaji wa vyakula unaowadunisha na wa mila au ibada hatari.

Nchini Ghana, mara nyingi ni wajane maskini sana wanaoumizwa zaidi. Wakati nchi imejaribu kumaliza mila zinazowadunisha na kuwadhuru wanaoomboleza kwa sheria,baadhi ya wajane bado wananyimwa makusudi vyakula vyenye virutubisho-au hata kufanyiwa mambo mengine mabaya zaidi.

Kuna taratibu za kimila ambapo wajane wanalazimishwa kunywa msupu ambayo inasehemu ya miili ya waume zao.

Katika baadhi ya maeneo nchini Ghana, wajane wanalazimishwa kunywa supu ambayo ina kucha na nywele za marehemu waume zao.

Chanzo cha picha, Katie Horwich

Maelezo ya picha, Katika baadhi ya maeneo nchini Ghana, wajane wanalazimishwa kunywa supu ambayo ina kucha na nywele za marehemu waume zao.

"Nywele na kucha za marehemu hutumiwa, mfu huoshwa na maji yaliyotumiwa kumuosha hutumiwa kama kinywaji ambacho analazimishwa kunywa mwanamke mjane ," anasema Fati Abdulai, mkurugenzi wa vuguvugu la Wanawake wanajane na yatima, ambalo ni shirika la misaada lenye makao yake kaskazini mwa Ghana.

Baadhi ya wajane wanaweza kuepuka mila hizi zinazowakandamiza lakini wengi walio maskini hawawezi kuziepuka.

Na kwasababu kwa kawaida mali hurithishwa familia ya mume baada ya kufa, wanawake wengi huzuiwa kurithi mashamba-isipokua wanapoolewa na ndugu wa wame zao.

Inakadiriwa kuwa kuna wajane takriban 285 million na karibu mmoja kati ya wajane 10 ni maskini sana. Katika nchi nyingi ujane ni aibu-na Umoja wa Mataifa unauita unyanyasaji wanaokabiliana nao wajane kama moja ya ukiukaji mkubwa zaidi wa haki za binadamu.

"Samaki, nyama na mayai ni marufuku"

Katika baadhi ya maeneo ya dunia unyanyapaa unaoambatana na ujane upo hata katika baadhi ya jamii tajiri.

Kwa mujibu wa Chitrita Banger Gee, mwanahistolia na muandishi wa vitabu vya vyakula katika jamii za Wahindu Bengal Magharib ,hadi kufikia karne chache zilizopita, wajane katika familia tajiri walitarajiwa kutubu kwa vifoi vya wame zao.

"Walikatazwa kula samaki, nyama, mayai,vitunguu na vitunguu saumu-vitu ambavyo walikua wakivila na ghafla walikatazwa kuvila ," anasema Gee.

"Suala zima lilikua ni kuwanyima vyakula muhimu na vitamu-kana kwamba ujane ni kosa, amefanya dhambi, ambalo anapaswa kuadhibiwa-walifanikisha hilo kwa kumnyima chakula alichopenda ."

Mama yake Chitrita Banger na bibi yake Prabhabati Mukerjee

Chanzo cha picha, Chitrita Banger Gee

Maelezo ya picha, Mama yake Chitrita Banger na bibi yake Prabhabati Mukerjee

Ni kitu ambacho Gee alikishuhudia wakati alipokua mtoto, wakati bibi/nyanya yake mwenyewe alipokua mjane.

"Kwangu yalikua mabadiliko makubwa - alibadilisha mavazi yake kutoka sari zenye rangi za kuvutia na kuvaa vipuli vyeupe ," anakumbuka. "Aliacha kula pamoja na familia na hakuweza kula vitu vyote, kwa sababu alizuiwa kula baadhi ya vyakula.

"Lakini wakati akipika, baadhi ya vyakula alivyopika vilikua ."

Kama mwanahistoria wa vyakula sasa, Banger Gee anaweza kuona jinsi bibi yake alivyotumia viungo mbadala vya chakula bdaa ya kuzuiwa kula vyakula vyenye viungo.

"Hakuweza kula vitunguu,lakini alitumia asafoetida badala yake ili kuwa na ladha inayofanana na kitunguu ," anasema Gee.

Bila kujali tuko wapi duniani, wakati tunaomboleza, tunahitaji vyakula vizuri na faraja ambayo tunaweza kuipata kutokana na chakula kizuri.

Lakini kumkosa mtu tunaekula nae kunaweza kuufanya muda wa chakula kuwa mgumu sana -na kusababisha madhara kwa mwili na akili zetu.

Woman looks out of the window while holding a cup of tea

Chanzo cha picha, Getty Images

Utafiti uliofanywa nchini China,Ulaya na, umebaini kuwa miongoni mwa watu wenye umri wa uzee, ujane unahusishwa na ulaji wa chakula duni na cha aina tofauti, na kupungua kwa uzito wa mwili.

Elisabeth Vesnaver, mtafiti wa virutubisho vya chakula, alifanya utafiti wa kina kuhusu vyakula wanavyokula wajane wa Canada wanavyokula wawapo na umri wa miaka kati ya 70 na 80.

"Nilikua na bibi zangu wawili ambao maisha yao yalikua tofauti ," anasema Vesnaver.

"Mmoja, baada ya mume wake kufa, katika kipindi cha miaka miwili pia alikufa si kwa ugonjwa wowote isipokua kukosa hamu ya chakula sawa na alichokula mume wake ambaye alikua mgonjwa . Nina bibi yangu mwingine ambaye huchukulia chakula kama dawa na ni sehemu kubwa ya matunzo yake ya kibinafsi."

Athari ya kifo

Vesnaver alibaini kuwa kwa wajane wote wawili walikua katika hatari ya juu ya zaidi ya kifo katika kipindi cha miaka mwili ya kwanza.Hii ni atahri ya kifo ambayo inafahamika vizuri na amekua kila mara aliamini kuwa chakula huenda kikawa sehemu yake.

"Utafiti unatuonyesha kuwa chakula na virutubisho hubadilika katika ujane " anasema Vesnaver. "Tuliona chakula duni, kupungua kwa uzito wa mwili kusikotarajiwa, kutoburudika vya kutosha. Na Wanaume wazee hawajawahi kujifunza kamwe kujilisha wenyewe."

Hatahivyo aliongeza kuwa sio tu juu ya kuwa na ujuzi wa kupika chakula.

"Kila kinachoshangaza kwa wanawake ni kwamba wengi watapata athari mbaya sawia na wanaume licha ya kwamba wamekua wakila chakula wanachojipia wenyewe na wanachompikia kila mmoja ."

Mwanamke mmoja aliwaambia watafiti kwamba mumewe alipokufa, hakua na sababu ya kuamka. Wakati mwingine alibaki kitandani hadi saa tano au hadi saa tisa na akawa hana muda maalum wa kula chakula.

Vesnaver alibaini kuwa wanawake waliopenda kupika zaidi kabla ya kuwa wajane walikua ni wajane ambao wahisi ugumu sana wa kuandaa chakula baada ya kufiwa na wenzi wao.Walihangaika kula chakula ambacho kilikua kwa ajili yao.

Wakati wanawake ambao hawakuhisi wanawajibika kulisha familia zao walikua na kipindi rahisi cha kuangazia maisha yao tu.

iku ya harusi yao na ukumbusho wa miaka 50 ya ndoa

Chanzo cha picha, Jonathan Freedland

Maelezo ya picha, Michael Freedland na mke wake Sara siku ya harusi yao na ukumbusho wa miaka 50 ya ndoa

Na baadhi ya wanaume wajane hupata ujuzi

Michael Freedland, mwandishi wa habari na mtangazaji, alikua ameoana na Sara mwenye umri wa miaka 52.

Alipofariki miaka sita iliyopita, mida ya mlo ilikua ni migumu.

"Hapakua na furaha katika kula chakula nyumbani kabisa," Freedlandanakumbuka. Alipungua uzito wa mwilibaada ya kufiwa na mke na alihangaika kurejea maisha ya kawaida.

"Nilikua ninakula chakula kidogo sana kwakweli wakati ule, lakini nikawa mtaalamu wa kutengeneza mayai laini," alisema.

Marafiki wa Freedland na familia yake walimuhurumia wakawa wanamualika kwa chakula cha jioni.

"Nilikua najijhisi mwenye hatia kwasababu ya kualikwa kwa vyakula vya jioni, nilijihisi kama mtu wa kutegemea msaada ," says Freedland.

"Kwangu mimi nilihisi kama kuazima kitabu ambacho ingebidi nikirudishe kwa mwenyewe, nilihisi ningependa kuandaa chakula cha jioni cha watu."

Hatimae watoto wake walimshawishi kupata masomo ya mapishi-akiwa na miaka 80 na zaidi.

Baada ya masomo ya mapishi , Freedland aliongeza ujuzi wake wa kupika zaidi ya "mayai tu ", aliweza kupika vyakula vingine kama vya kukaangwa. Familia yake ilimpatia ujuzi wa kupika vyakula vyao walivyopenda pia.

"Ulikua ni uzoefu mzuri hakika-nadhani ulibadili maisha yangu kwa kweli " aliiambia BBC

Tangu aliporekodi mahojiano yale , Michael Freedland alifariki

Lisa Kolb with her husband Erik

Chanzo cha picha, Lisa Kolb

Maelezo ya picha, Lisa Kolb with her late husband Erik Kolb

Lakini je ni vipi tunaweza kuwasaidia watu waliolazimika kuwa wajane?

Lisa Kolb, mwandishi na mpishi wa vyakula vitokanavyo na wanyama mjini Washington DC, h ana baadhi ya mapendekezo . Alimpoteza mume wake Erik katika ajali iliyotokea milimani miezi 19 baada ya ndoa . Wote pamoja walikua na umri wa miaka 34 wakati huo.

"Kwa mume au mke wako mnaepika pamoja, kula pamoja, kwenda kwenye sherehe za chakula cha jioni pamoja-na pale unapompoteza inasababisha upweke mkubwa na kukaa tena kwenye meza ya chakula katika jiko tupu ni vigumu ," anasema.

"Huku kuleta chakula ni muhimu, kuwa na watu karibu yako ni bora sana. Ninadhani watu wanafikiri aah! ni chakula cha kawaida tu ni kwanini mtu aje kwa ajili ya chakula hicho?. Lakini ni chakula tu ni fursa ya kuwa miongobi mwa watu na kuhisi kuwa watu wanakujali ".

Kwahiyo kama hujui ni nini cha kusema kwa mtu ambaye anaomboleza na unashindwa utamsaidia vipi, kitendo rahisi ni kumpikia,au umkaribishe ushiriki nae chakula, linaweza kuwa ni jambo zuri sana unaloweza kumfanyia mtu aliyefiwa na mume au mke wake.