Virusi vya corona: Je unajua ugonjwa wa corona huenda ulianza mapema mno?

Chanzo cha picha, AFP
Kuanza kufurika kwa watu hospitalini huenda kunaashiria kwamba corona ilianza mapema mno, utafiti unaonesha
Kuanza kumininika kwa watu hospitalini kunaashiria kwamba huenda vcorona ilikumba China mapema kabla ya kuripotiwa rasmi, utafiti unaonesha.
Watafiti wa Havard wanasema picha za setilaiti zinaonesha kuongezeka kwa wagonjwa wengi katika hospitali tano kwenye mji wa Wuhan kuanzia mwisho wa Agosti hadi Desemba.
Ongezeko la wagonjwa wakati huo kunaendana na kuongezeka kwa utafutaji wa taarifa za dalili za kukohoa na kuharisha kipindi hicho hicho.
China imesema kuwa utafiti huo ni dhihaka na uliotegemea taarifa zisizo za kweli.
Inaaminika kwamba virusi hivyo vilijittokeza sana China Novemba.
Mamlaka iliripoti visa vya ugonjwa wa mapafu yaani nimonia kwa Shirika la Afya Duniani (WHO) Desemba 31 2019.
Je utafiti huo ulionesha nini?
Watafiti walipitia data ya setilaiti katika hospitali tano za Wuhan, kwa kulinganisha na data ya mwisho ya msimu uliopita 2018 hadi kipindi sawa na hiki 2019.
Katika kisa kimoja, watafiti walibaini magari 171 yakiwa yameegeshwa katika moja ya hospitali kubwa huko Wuhan, Hospitali ya Tianyou Oktoba 2018.
Data ya setilaiti kipindi sawa na hicho 2019 zilizonesha magari 285 yakiwa katika sehemu hiyo hiyo ikiwa ni ongezeko la asilimia 67.
Pia kulikuwa na ongezeka la maneno yaliyokuwa yanatafutwa mitandaoni yanayohusishwa na dalili za virusi vya corona katika mtandao wa Baidu wakati huohuo.
"Utafiti zaidi bado unahitajika kufanywa kubaini hasa kile kilichotokea na watu kujifunza namna ugonjwa huu ulivyolipuka na hadi ukafika kwa binadamu. Kwa hiyo huu ni ushahidi mwingine."
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje Hua Chunying alikanusha madai hayo katika mkutano na wanahabari Jumanne.
"Nafikiri ni jambo linaloshangaza, la kustaajabisha sana kufikia hitimisho kama hilo kwa kuzingatia mambo yasiyo na uhakika kama vile watu wengi kuwa hospitali kwa wakati mmoja," alisema.
Lakini je athari ya utafiti huu ni zipi
Mwandishi wa BBC China John Sudworth anasema data zilizotumiwa na watafiti hazikuwa za uhakika, kwa mfano, hawakuweza kukusanya data ya kutoka kwa picha za setilaiti siku hiyo hiyo kwa miaka kadhaa kufuatana.
Lakini kama maambukizi yalikuwa tayari yapo - pengine yakachelewa kubainika, baadhi ya watu wangekuwa wametoka mji wa Wuhan na kwenda miji mingine jambo ambalo limeshuhudiwa katika maeneo mengine duniani ambako kunasemekana ugonjwa wa Covid-19 ulianza kuingia mapema, mwanahabari wa BBC anasema.
Hata hivyo huenda ikawa maonevu kutumia utafiti huo kama ushahidi wa kwamba China ilichelewa kuchukua hatua, kwasababu kuna uwezekano China haikuweza kubaini ugonjwa huo kabla haujatambulika rasmi, mwanahabari wa BBC anaongeza.

Chanzo cha picha, Harvard University
China iliripoti kwamba imepokea wagonjwa wengi wa maradhi ya homa ya mapafu ambayo haikujulikana chanzo chake kwa WHO Desemba 31, 2019.
Siku tisa baadae, mamlaka ya China ikabaini kwamba wamegundua virusi vipya vya corona na baadae vikapewa jina la Sars-CoV-2 yaani Covid-19.
Wuhan na miji mengine ya China yalianza kutekeleza hatua ya kusalia ndani Januari 23, 2020.
WHO ilitangaza kwamba Covid-19 ni janga la kitaifa Januari 30, 2020 baada ya kuthibitishwa kwa wagonjwa 82 nje ya China.


Uchambuzi naHelen Briggs, Mwanahabari wa BBC wa masuala ya afya
Vipimo vinaashiria kwamba virusi vilikuwepo lakini sio vyote vyenye kuhusishwa na soko la kuuza vyakula vya baharini na hakuna mnyama yoyote ambaye ametambuliwa rasmi kama chanzo.
Na kutoka wakati huo ushahidi umekuwa ukionesha kwamba huenda virusi vya corona vilianza kusambaa mapema ikiwemo kutoka kwa daktari mfaransa ambaye alisema mgonjwa wake alithibitishwa kupata maambukizi mwishoni mwa Desemba.
Na sasa hivi kuna ushahidi mpya kutoka kwa picha za setilaiti, na maneno yanayotafutwa kupitia mitandao kunakoashiria kwamba watu walifika kwa wingi hospitalini kipindi fulani kabla ya corona kutambulika na kuna wengi ambao ambao kipindi hicho hicho walikuwa wanataka kujua kuhusu dalili za kile wanachopitia mtandaoni hasa katika mji wa Wuhan.
Na sasa hivi utafiti pekee zaidi wa virusi kwa wanyama na binadamu ndio unaoweza kutoa jibu, ingawa kuna uwezekano wa kutojua kabisa ugonjwa huo ulianza lini na chanzo chake ni nini.














