Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Jinsi meli tano za mafuta zilizokuwa zikielekea Venezuela zilivyozua hofu kati ya Marekani na Iran
Hali ya wasiwasi kati ya Marekani na Iran imechukua mkondo mpya nchini Venezuela.
Likiwa Katikati ya mlipuko wa corona, taifa hilo la Amerika ya Kusini lilikumbwa na uhaba mkubwa wa gesi suala ambalo limeathiri vibaya uchumi wake na taifa la Nicholas Maduro badala yake limeamua kutafuta usaidizi kutoka kwa Iran.
Utawala wa rais Donald Trump kwa muda mrefu umekuwa umeiwekea vikwazo vya kisera ambavyo vinalenga kushinikiza kuanguka kwa uongozi wa Maduro, ambaye anamshutumu kuwa mtawala haramu.
Hiyo ndio Iran ambayo pia nayo inakabiliwa na vikwazo ikishutumiwa na Marekani kwa kuwa mfadhili mkubwa wa ugaidi wa kimataifa.
Uhasama kati ya Washington na Tehran uliongezeka wiki hii baada ya meli kadhaa za kubeba mafuta kutoka Venezuela kuonekana zikitoka Iran na mafuta.
Huku maafisa wakikiambia chombo cha habari cha Reuters kwamba Washington inafikiria jinsi ya kukabiliana na meli inayokiuka vikwazo vyake, siku ya Jumanne wizara ya fedha iliiwekea vikwazo kampuni moja ya China inayofanya kazi katika shirika la ndege la Iran, Mahan Air , ambayo inaishutumu kwa kushirikiana na magaidi na kuchukua dhahabu kutoka Venezuela.
Meli za kijeshi za Marekani kama kawaida hupiga doria katika maji ya Carebean , karibu na eneo linalotumika kama njia ya meli za mizigo za Iran.
Meli ya kijeshi ya Marekani kwa jina Fourth Fleet, inayotoka katika eneo la Jacksonville, Florida hufanya operesheni zake zote katika eneo hilo.
Ni kutokana na hilo ndipo waziri wa masuala ya kigeni nchini Iran Mohamed Javad Zarif aliandika barua kwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akionya kwamba hatua yoyote ya kijeshi kutoka kwa Marekani dhidi ya meli zake itachukuliwa kama kitendo cha uharamia na itafuatiwa na athari kali..
Mwandishi wa BBC katika idhaa ya Persia Kasra Naji anasema kwamba uwezekano wa Iran kulumbana na Marekani upo juu.
Kwa nini Maduro aliomba usaidizi kutoka kwa Iran
Tangu wakati wa utawala wa rais wa zamani wa taifa hilo Hugo Chavez , Venezuela ilikuwa na uhusiano mzuri na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Venezuela inakabiliwa na hali ngumu ya kiuchumi kwa sasa katika historia ya taifa hilo.
Uchumi huo umeshuka kwa zaidi ya asilimia 50 tangu Nicholas Maduro kuingia madarakani 2013 na mamilioni ya raia wa Venezuela wameondoka nchini humo.
Ujio wa virusi vya corona na kushuka kwa bei ya mafuta kumefanya mambo kuwa mabaya zaidi kwa taifa hilo la mafuta.
Usimamizi mbaya na ufisadi katika kampuni ya mafuta katika miaka ya hivi karibuni ulisababisha kuanguka kwa kiwanda cha kusafisha mafuta na hivyo basi kupungua kwa gesi.
Kwa miezi kadhaa , serikali ya Venezuela ilikabiliana na uhaba huo kwa kuuza mafuta ghafi kwa ubadilishanaji wa gesi kwa mteja wake mkuu ambaye ni kampuni ya Urusi ya Rosneft.
Lakini utawala wa rais Trump uliweka vikwazo vingine mnamo mwezi Februari na Machi dhidi ya washirika wa kampuni ya Rosneft ambayo ilikuwa ikiuza mafuta ya Venezuela katika soko la kimataifa .
Hadi kufikia mwezi Machi , Rosneft ilitangaza kuondoka kwake Venezuela .
Afisa wa wizara ya kigeni nchini Marekani aliambia BBC Mundo kwamba ilikuwa hatua ya kulinda mali yake kutowekewa vikwazo.
Tangu wakati huo , kumekuwa na upungufu wa gesi nchini Venezuela na watu hulazimika kupanga foleni kubwa ili kununua sio zaidi ya lita 30 kwa siku.
Na Maduro sasa anajaribu kupata usaidizi kutoka kwa Iran kuziba pengo hilo lililoachwa na Rosneft.
Je Iran inafanya nini nchini Venezuela?
Wiki chache zilizopita, muda mfupi baada ya kampuni ya Rosneft kuondoka, ripoti kadhaa zimesema kwamba ndege za kampuni binafsi ya Iran Mahan Air zimeanza kuwasili katika jimbo la Falcón zikiwa na vifaa na wafanyakazi kutoka Iran ili kurekebisha viwanda vya kusafishia mafuta vilivyopo katika eneo la Paraguana, likiwa ndio eneo muhimu zaidi nchini humo.
Tarehe 28 mwezi Aprili , waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani Mike Pompeo alisema kwamba Mahan air ilikuwa ikitoa usaidizi usiojulikana kwa utawala wa Maduro na kuonya kwamba safari hizo za ndege zinapaswa kusitishwa.
Japokuwa serikali ya Venezuela haijatoa habari zozote kuhusu kinachoendelea na kukataa kujibu ombi la kutoa tamko, Eudis Girot Mkurugenzi wa muungano mmoja wa mafuta nchini Venezuela aliambia BBC Mundo kwamba Iran inajaribu kuving'oa viwanda hivyo na kwamba vina tatizo kubwa linalotokana na kutotumika kwa muda mrefu ambalo haliwezi kutatuliwa haraka.
Inakadiriwa kwamba wakati viwanda hivyo viwili vya Paraguana vilipokuwa vikifanya kazi, vilikuwa vinaweza kuzalisha mapipa 965,000 kwa siku ya mafuta , lakini wataalamu wanaamini kwamba ukosefu wa umeme wa mara kwa mara na maji nchini Venezuela utazuia kiwango hicho.
Kwa nini meli ni muhimu?
Meli za mizigo za Iran ambazo zimeikasirisha Marekani ni muhimu kwa rais wa Venezuela, kwa kuwa ndio ambazo zimekuwa suluhu ya muda mfupi ya kuingiza gesi nchini humo.
Afisa mmoja wa masuala ya kiufundi kutoka kwenye kampuni ya Refinitiv, ambayo huchunguza trafiki baharini , iliiambia AP kwamba kuna meli tano na husafirisha mizigo ya gesi na bidhaa kama hizo zenye gharama ya $ 45 million .
Iwapo meli hizo zitawasili, Maduro atakuwa amefungua njia ya kuuza mafuta na huenda akaokoa tatizo la mafuta lililopo.
Kwa Iran , taifa ambalo limeathirika sana na virusi vya corona, kupata dhahabu kutoka Venezuela kutaisaidia kuzuia athari ya vikwazo na kuibadilisha kuwa fedha ili kugharamia masuala yake ya dharura.
Je Marekani itafanya nini?
Mgogoro kati ya Marekani na Iran ulifikia kilele Januari mwaka jana , wakati ndege ya Marekani isiyo na rubani ilipomuua kiongozi mkuu wa jeshi jenerali Qasem Soleimani.
Mapema mwezi Julai, vikosi vya Iran viliikamata meli ya Uingereza katika maji ya mkondo wa Hormuz na kuiangusha ndege isio na rubani ya Maarekani ambayo inaishutumu kufuata meli zake.