Virusi vya corona: FC Seoul yaomba msamaha kwa kuweka 'wanasesere wa ngono'' uwanjani

Iliyochapishwa

Ni changamoto kwa ligi za soka kote duniani- hasa kama mchezo utaanza kayika viwanja vitupu, vipi hali hii inaweza kuboreshwa.?

Hatahivyo sio klabu nyingi zinaweza, kukimbilia kufuata mfano wa FC Seoul.

Klabu ya hiyo ya Korea Kusini ilibidi iombe msamaha baada ya mashabiki kuwalaumu kwa kuwaweka wanasesere wa ngono katika nafasi za kukaa mashabiki.

FC Seoul ilisisitiza kuwa walikua ni "wanasesere wanaotumiwa katika kuuza nguo madukani" na wala sio wanasesele wa ngono -lakini ikakiri kuwa waliwapata kutoka katika kampuni inayotengeneza wanasesele wa ngono.

Na baadhi ya wanasesele walikua wakionyesha ishara za wavuti wa matangazo ya ngono-licha ya kwamba ponografia imepigwa marufuku nchini Korea Kusini.

Ni nini kilichotokea katika mechi ?

JUmapili, FC Seoul ilicheza mchezo wao wa kwaza ya msimu wa Ligi ya Korea Kusini - League K

Uwanja ulikua mtupu- ikiwa ni moja ya hatua zilizochukuliwa kuzuwia mlipuko wa Covid-19.

Kwa hiyo kabla ya mechi, kampuni inayoitwa Dalcom ilijitolea kujaza nafasi za viti zilizoachwa wazi, na klabu ikakubali. Kwa ujumla, walikua ni wanasesele 30- 25 kati yao walikua ni wanawake na watano walikua ni wanaume.

Hatahivyo, mashabiki waliokua wakitazama mechi hiyo kwa njia ya mtandao walibaini kuwa baadhi ya wanasesere waliokua na muonekano kama wa wanasesele wa ngono -jambo lililoilazimisha klabu iombe radhi kupitia kurasa zake za Facebook na Instagram.

Afisa wa klabu hiyo Lee Ji-hoonameiambia BBC kuwa haikufanya uchunguzi juu ya kampuni ya Dalcom, na haikufahamu kazi inayofanya.

Lakini klabu hiyo imesema kwamba Dalcom ilisisitiza kuwa wanasesere inaowapatia ni "wale wa kawaida wanaotumiwa kuuza nguo madukani ", na wala hawahusiani kabisa na ponografia.

Bwana Lee amekiri kuwa alihisi kweli wanasesere hao "walionekana swa kabisa na binadamu " - lakini akasema haikumuingia akilini kwamba wangekua ni wanasesele wa ngono.

Mechi za soka zilifufuliwa lini Korea Kusini?

Msimu wa 2020 wa K League ulitakiwa kuazna mnamo mwezi wa February lakini ulicheleweshwa kutokana ana mlipuko wa virusi vya corona

Lakini mafanikio ya Korea Kusini katika mapambano dhidi ya virusi yaliruhusu kufufuliwa kwa soka mapema kuliko maerneo mengine duniani.

Na, wakati msimu ulipoanza tarehe 8 Mei, K League yalikua ni mojawapo ya maeneo muhimu kwa mashabiki wa kuelekeza macho yao- jambo lililofanya dunia kufuatilia mechi zao.

Mechi ya ufunguzi - kati ya Jeonbuk Motors na Suwon Bluewings - hata ilitazamwa moja kwa moja kupitia BBC.

Licha ya viti vitupu, kusalimiana kwa mikono ni marufuku na makocha lazima wavae barakoa.

"Kutema mate au kupenga makamasi ni marufuku na wachezaji wamekatazwa kuzungumza wakati wanapokua wamekaribiana ," alisema afisa wa K League kabla ya mechi ya kwanza.

Taarifa zaidi kuhusu virusi vya corona

Ni Ligi gani za soka zimefufuliwa ?

Ligi ya Ujerumani Bundesliga ilianza tena mechi wikendi, lakini, sawa na Korea Kusini, hakuna mashabiki uwanjani.

Ligi kuu ya Primia ya England imetangaza kuwa huenda ikafungua mezi zake tarehe 12 Juni - lakini kuna "hisia kubwa " kuwa tarehe hii inaweza kusogezwa nyuma.

Ligi nyingine, kama Ligi ya Ufaransa zilifuta misimu yake yote.

Unaweza pia kutazama: