Virusi vya corona: China inaweza kuwapima wakazi wote wa Wuhan kwa siku kumi pekee?

Mamlaka ya China imeapa kuwapima wakazi wote wa Wuhan

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mamlaka ya China imeapa kuwapima wakazi wote wa Wuhan
    • Author, Pablo Uchoa na Vincent Ni
    • Nafasi, BBC World Service
  • Iliyochapishwa

Mkakati wa China wa kupambana na virusi vya corona umeelezewa kama "labda ni juhudi kubwa zaidi za kukabili katika historia ", na Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO).

Lakini lengo la hivi karibuni la Beijing la kupima watu wote wa Wuhan, jiji ambalo lilikuwa kitovu cha janga la Covid-19 mnamo Januari, katika siku 10 tu kumezusha maswali.

Mamlaka za mji zimeamriwa kupanga mipango ya kuwapima wakazi milioni 11 wa jiji hilo waliosajiliwa, kuanzia na watu walio katika hatari na walio katika "kazi muhimu", kama vile huduma ya afya.

Mamlaka sasa zimeonesha kuwa vipimo vinaweza kuharibiwa, kwa hivyo sampuli zinaweza kukusanywa na kutunzwa kwa kiwango kikubwa kama hicho.

Vipimo vitaonesha ikiwa wameambukizwa na Covid-19.

Lakini lengo hili kubwa linaweza kuwa nadharia, kumaanisha kwamba Wuhan itapima angalau watu milioni moja ya wakazi wake kwa siku -uwezo wa upimaji wa kila siku wa sasa ni watu 40,000 hadi 60,000.

"Tunapaswa kutarajia muujiza," Yanzhong Huang, afisa mwandamizi wa Afya wa Global Health kwenye Baraza la Mambo ya nje huko New York, Marekani ameeleza

Kwa nini imedhamiria kuwapima watu wengi ?

Mamlaka zina hofu kuwa kuna watu walio na virusi ambao hawaoneshi dalili

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mamlaka zina hofu kuwa kuna watu walio na virusi ambao hawaoneshi dalili

Mipango hii kabambe ilitangazwa baada ya kupatikana kwa watu sita walioambukizwa katika eneo moja la makazi katika mji wa Wuhan mwishoni mwa juma lililopita.

Watu hawa a walipima virusi lakini hawakuonesha dalili kama kikohozi au homa.

Kufuatia utambuzi huo, wakaazi wote 5,000 wa eneo waliamriwa kufanya vipimo.

Wengine wanasema kuwa kati ya wakazi milioni 11 waliosajiliwa wa Wuhan, wengi wao wameondoka jijini kabla ya kuwekwa kizuizini au tayari wamepimwa katika wiki za hivi karibuni.

Kati ya wakazi wa Wuhan milioni tatu hadi tano tayari wamepimwa, Yang Zhanqiu, naibu mkurugenzi wa idara ya biolojia ya pathogen katika Chuo Kikuu cha Wuhan, aliambia gazeti la Global Times.

"Wuhan ina uwezo wa kuwapima watu milioni sita hadi nane kwa siku 10," alisema.

Hata kama idadi halisi ya vipimo ambavyo vitafanywa imepunguzwa kutoka milioni sita hadi nane, hii bado inamaanisha idadi ya upimaji ya kila siku ya 600,000 hadi 800,000, ikiwa viongozi watazingatia muda uliowekwa wa siku 10.

Hii ni changamoto

Tarehe 22 mwezi Aprili, mji wa Hubei uliripoti kuwa watu takribani 89,000 hupimwa kila siku.

Iliongeza kuwa mjini Wuhan, idadi ya watu wanaopimwa kila siku ilikuwa 63,000.

Na tarehe 10 mwezi Mei, watu chini ya 40,000 walipimwa mjini Wuhan kwa siku moja, kwa mujibu wa mamlaka za mji huo.

Ni namna gani mamilioni ya watu watapimwa kwa haraka?

Wakazi wakiwa wamevalia barakoa

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wakazi wakiwa wamevalia barakoa

Wataalam wana maoni kwamba ikiwa mamlaka ya China imedhamiria hili, inawezekana zoezi hili likawa na majibu ya nadharia.

Siku ya Jumatano [Mei 13], vyombo vya habari vya China Caixin vilinukuu Wuhan CDC ikisema kwamba upimaji wa watu wengi hufanywa hasa na kampuni za tatu.

CDCs za mitaa na hospitali wilaya zote za mji zitatuma wafanyikazi kukusanya sampuli.

Afisa huyo alikadiria kuwa uwezo wa mashirika ya kupima watu ni 100,000 kwa siku, na alikubali kwamba haiwezekani kufanikiwa kupima kwa wingi ndani ya muda mfupi.

"Kwa hivyo, vipimo vitayumbishwa, ikimaanisha kuwa wilaya kadhaa [katika jiji] zinaanza Mei 12; zingine kutoka Mei 17, kwa mfano. Kila wilaya inakamilisha vipimo ndani ya siku 10 tangu tarehe inapoanza."

China ina uwezo wa kuzalisha vifaa vya kupimia milioni tano kwa siku, wizara ya viwanda ya nchi hiyo ilisema mwezi uliopita. Na vituo zaidi vya kupima na maabara vinajengwa kuchambua sampuli zilizokusanywa.

Wengine, pamoja na Profesa Yang, wanasema kwamba hakuna haja ya kumpima kila mkazi huko Wuhan ikiwa vitongoji wanavyoishi haviripoti kuwepo kwa maambukizi.

"Hautawahi kujua ikiwa watu wameambukizwa baada ya kukutwa hawana maambukizi ... kimsingi ni uchunguzi wa janga kutazama hali ya sasa," aliliambia gazeti la Global Times.

‘Hofu ya kuwepo wimbi la pili na maambukizi'

Wuhan ilitoka kwenye masharti ya kukaa ndani yaliyoumu kwa wiki 11

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wuhan ilitoka kwenye masharti ya kukaa ndani yaliyoumu kwa wiki 11

Wakati nchi zaidi zinaanza kupunguza makali ya masharti, wasiwasi kuhusu wimbi la maambukizi

Wuhan iliibuka kutoka kwa kizuizi kikali cha wiki 11 mnamo Aprili 8 lakini sasa kuna hofu ya wimbi la pili la maambukizi mapya, hasa baada ya maambukizi mapya.

Hatua za tahadhari pia zinachukuliwa mahali pengine nchini Uchina: mji wa Kaskazini Mashariki mwa Jilin, kwa mfano, umejitenga kutoka kwa kazi za nje, na ni wakazi tu awaliokutwa hawana maambulizi ya Covid-19 katika saa 48 zilizopita wanaruhusiwa kuondoka mjini.

Huduma za treni na basi zimesimamishwa, na sinema, kumbi za michezo na vituo vya mawasiliano ya mtandao imefungwa.

Wu Zunyou, daktari mkuu wa magonjwa katika Kituo cha Uchina cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa, alisema serikali iko macho kwa maambukizi ambayo yatabainika baada ya vipimo.

Vipimo 'vitagharimu'

Kipimo cha joto

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kipimo cha joto

Kupima watu wote Wuhan itakuwa "ghali sana", anasema Profesa Huang.

"Lakini kumbuka hii ni China. Jinsi walivyoweka marufuku ya kutotoka nje, vitu vyote hivyo vilikuwa vya gharama. "

"Lakini hiyo ndio ilikuwa lengo kuu: kuongeza usalama kwa gharama zote."

Msimamo wa China dhidi ya janga hili ni tofauti kabisa na nchi nyingine.

Huko Marekani, upimaji wa wastani wa kila siku ni 300,000 na Rais Donald Trump analaumiwa kwa hatua anazochukua, licha ya kuwa na idadi kubwa zaidi ya vifo ulimwenguni kwa sababu ya virusi.

coronavirus