Siku ya akina mama: Anna Jarvis, mwanamke aliyejuta kubuni siku ya mama duniani

Anna Jarvis

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Anna Jarvis: Mwanamke aliyejuta kubuni siku ya mama duniani
Iliyochapishwa

Mwanamke aliyebuni siku ya mama, ambayo huadhimishwa katika nchi nyingi Jumapili ya pili ya mwezi Mei,

Wakati Elizabeth Burr alipopokea simu siku chache zilizopita kutoka kwa mtu aliyekuwa akimuuliza kuhusu historia ya familia yake, awali alihisi kuwa amedukuliwa. ''Nilifikiri kwamba 'Sawa nimedukuliwa, sitaweza kuziona fedha zangu tena'', alisema.

Kiukweli simu ile ilitoka kwa mtafiti wa historia ya familia aliyekuwa akitafuta ndugu wa Anna Jarvis walio hai, mwanamke aliyebuni siku ya mama nchini Marekani miaka 100 iliyopita.

Anna Jarvis alikuwa mmoja kati ya watoto 13, wanne pekee waliishi mpaka kuwa wakubwa. Kaka yake mkubwa alikuwa pekee aliyepata watoto, lakini wengi walifariki wakiwa wadogo kutokana na ugonjwa wa kifua kikuu na ndugu te wa mwisho alifariki miaka ya 1980.

Hivyo Elisabeth aliamua kuwatafuta binamu zake, hatua ambayo ndio iliyomfikisha kwa Elizabeth Burr.

Elizabeth alihakikishiwa kuwa fedha zake ziko salama.

Baba na shangazi zake hawajesherehekea siku ya mama walipokuwa wakikua-kwa kumheshimu Anna, na mawazo yake kuwa wazo lake liliibwa kwa ajili ya maslahi ya kibiashara na kudhoofishwa

Ann Reeves Jarvis

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ann Reeves Jarvis

Kampeni ya Anna ni muhimu ya kusheherekea wakina mama aliirithi kutoka kwa mama yake, Ann Reeves Jarvis.

Bibi Jarvis alitumia maisha yake akiwashawishi wakina mama kuwajali watoto wao, anaeleza mwana historia Katharine Antolini, na alitaka kazi za wakina mama zitambulike.

''Nina matumaini kuwa mtu mmoja siku moja atafanya siku ya kumbukumbu kwa ajili ya siku ya mama kukumbuka huduma alizozitoa za kiutu katika kila Nyanja ya maisha. Anastahili hilo,''alisema bibi Jarvis.

Norman Rockwell mchoraji wa m,arekani akichoroa bango rasmi la siku ya kina mama duniani

Chanzo cha picha, Getty Images

Katika klabu yao kina mama walijifunza usafi kama vile umuhimu wa kuchemsha maji ya kunywa.

Waratibu walitoa dawa kwa familia zenye wagonjwa, na ilipokuwa na ulazima waliwekwa karantini nyumba nzima ili kuzuia maambukizi ya maradhi.

Bibi Jarvis mwenyewe alipoteza watoto wake tisa, watano wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Marekani (1861-1865) kwa maradhi anasema Antolini , profesa katika chuo cha Wesleyan West Virginia.

Bibi Jarvis aliaga dunia mwaka 1905, akiwa amezungukwa na watoto wake wanne waliokuwa, huzuni ilikua kubwa, Anna aliahidi kutimiza ndoto ya mama yake, ingawa njia aliyoitumia ilikuwa ya tofauti, Antolini alisema.

Wakati Bibi Jarvis alipotaka kusheherekea kazi iliyofanywa na wakina mama kuboresha maisha yaw engine, mawazo ya Anna yalikuwa kwa mtoto wake wa kike aliyekuwa akijitoa . Ujumbe mkuu kwa siku ya mama ilikuwa ''kwa mama bora aliyewahi kuishi-Mama yako.''

Siku ya mama ilipokuwa Jumapili

Ujumbe huu uligusa pia makanisa- uamuzi wa Anna wa kuwa na siku hii Jumapili ulikuwa wa akili, anasema Antolini.

Miaka mitatu baada ya kifo cha bibi Jarvis, sherehe ya kwanza ya siku ya mama ilisheherekewa kwenye kanisa la wamethodisti huko Grafton- Anna Jarvis alichagua jumapili ya pili ya mwezi Mei kwa sababu ni karibu na tarehe 9, siku ambayo mama yake alifariki. Anna alikua akiwapa mamia ya wakina mama waliohudhuria sherehe maua meupe ya carnations , yaliyopendwa zaidi na mama yake.

Umaarufu wa sherehe ulikua na kukua. Mwaka 1910 siku ya mama ikawa sikukuu ya jimbo la Virginia Magharibi na mwaka 1914 Rais Woodrow Wilson akaifanya sikukuu ya kitaifa nchini Marekani.

Siku hii ilionesha mafanikio makubwa kwa upande wa biashara.

''Ingawa Anna hakutaka siku hii kuwa ya kibiashara , faida ilianza kuonekana mapema sana. Soko la maua, watengeneza kadi na peremende walipata umaarufu na faida siku hizo''.Alisema Antolini.

Mtu pekee ambaye hakutaka faida kwa ajili ya siku hii ni Anna mwenyewe. Alikataa ofa za fedha zilizotolewa na viwanda vya kutengeneza maua.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mtu pekee ambaye hakutaka faida kwa ajili ya siku hii ni Anna mwenyewe. Alikataa ofa za fedha zilizotolewa na viwanda vya kutengeneza maua.

Mtu pekee ambaye hakutaka faida kwa ajili ya siku hii ni Anna mwenyewe. Alikataa ofa za fedha zilizotolewa na viwanda vya kutengeneza maua.

''Hakupata faida kutokana na siku hii, wakati ingekuwa rahisi kwake kufanya hivyo. Nilimpenda sana kutokana na hilo,'' alisema Antolini.

Lakini Anna alitumia fedha yake kwa ajili ya kupambana na biashara wakati wa sherehe za siku ya mama.

ELIZABETH BURR

Chanzo cha picha, Getty Images

Hata kabla siku hii haijawa ya kimataifa alidai haki miliki na kutishia kumshtaki yeyote atakeifanya siku hii kuwa ya kibiashara bila ruhusa yake.