Wanasayansi wanasema mashimo hayo ni kiungo muhimu kilichokosekana kuhusu uundaji wa anga

Iliyochapishwa

Kundi moja la wataalamu wa angana limegundua kile linachosema ni ushaidi bora zaidi kuwahi kupatikana kuhusu shimo jeusi lililopo angani.

Wanasema kwamba shimo hilo lilisaliti uwepo wake kwa kuitawanya vipandevipande nyota iliolikaribia.

Ni vitu vyenye ukubwa kama huo vinavyokosekana kama kiungo cha jinsi ulimwengu ulivyouumbwa . Watafiti walitumia mionzi ya X-ray, pamoja na daraubini ili kuyaona mashimo hayo.

''Mashimo meusi yanayopatikana angani huwa hayaonekani kwa urahisi , hivyobasi ni muhimu kufikiria na kuamua maelezo mbadala kwa kila shimo'', alisema Dkt Daceng Lin kutoka chuo kikuu cha New Hampshire mjini Dutham Marekani ambaye aliongoza utafiti huo.

''Hivyo ndivyo darubuni kubwa ya Hubble ilifanikiwa kutusaidia kuona shimo hilo.

Mnamo 2006, chombo cha Nasa kinachozunguka Chandra X-ray Observatory na XMM-Newton satelaiti ya Shirika la Ulaya ziliona picha ya nguvu ya X-ray iliyoitwa 3XMM J215022.4−055108.

''Hali ya picha hiyo ya X-ray ilikuwa inaweza kuelezewa kwa mazingira mawili kulingana na Dkt Lin. Kuna uwezekano ipo mbali na nje ya galaxy ambapo shimo jeusi limemeza nyota ama nyota baridi iliotawanyika katika galaxy yetu'', aliambia BBC News.

Nyota za Netron ni mabaki ya nyota iliotawanyika

Je shimo jeusi ni nini?

  • Ni eneo lenye nafasi angani ambapo hakuna chochote hata mwangaza kinaweza kuepuka.
  • Licha ya jina lake shimo hilo halipo tupu na badala yake lina idadi kubwa ya vitu vilivyojaa katika eneo dogo na hivyobasi kulipa nguvu kubwa ya mvuto wa kati au gravitational pull.
  • Kuna eneo lenye mwanya katikati ya shimo jeusi kwa jina event horizon. Kitu kinachopita karibu na mwanya huo hakiwezi kuepuka mvuto wake na kinapoingia hakiwezi kupatikana tena.

Ili kutofautisha kati ya mazingira haya mawili, darubini ya Hubble Space ilielekezwa kwenye chanzo cha X-ray ili kubaini eneo lake sahihi.

Darubini ilitoa ushahidi mkubwa kwamba X ray hiyo ilitoka sio tu katika chanzo kilichotengwa bali katika mkusanyiko wa nyota nje ya galaxy.

Hili ndio eneo ambalo wataalam wa angani walitarajia kupata shimo jeusi la wastani. Mashimo makubwa meusi hupatikana katikati ya galaxy , kwa mfano , mwanga unaotoka angani unahifadhi shimo jeusi ilililopo katikati kwa jina Sagittarius A*.

Lakini mashimo meusi ya katikati yamekuwa vigumu kuyapata kwasababu ni madogo na hayana utendakazi mkubwa yakilinganishwa na yale makubwa.

Kuongezea, ni kwamba hayana nyenzo za karibu kufanya kazi kama mafuta na hayana nguvu zinazohitajika kuvuta nyota ndani ili kutoa mwangaza wa X ray.

Wataalam wa angani walilazimika kulipiga picha shimo ,moja jeusi lenye ukubwa wa wastani lilipokuwa likiimeza nyota. Dkt Lin na wenzake walilazimika kupitia maelfu ya picha za XMM-Newton ili kuweza kuliona shimo hilo.

Mwangaza unaotolewa na mionzi ya X ray kutoka kwa nyota zilizopasuliwa vipande vipande uliwaruhusu wanaanga kukadiria ukubwa wa shimo hilo kuwa mara 50,000 zaidi ya ukubwa wa jua.

Hili sio shimo jeusi la kwanza , lakini unapoona jinsi linavyopasua nyota vipande vipande linafanya ugunduzi huo kuwa na ushawishi mkubwa, kulingana na kundi la Dkt Lin.

''Ukichunguza kuhusu chanzo na ugunduzi wa mashimo hayo meusi utapata majibu ya chimbuko la mashimo meusi makubwa ambayo hupatikana katikati ya galaxy'', alisema mmoja ya wanachama wa kundi hilo Dkt Natalie Webb kutoka chuo kikuu cha Toulose , Ufaransa.