Coronavirus: Kunawa mikono kulivyo kugumu katika nchi zinazoendelea

Chanzo cha picha, Mukuru Promotion Centre, Winnie Ogutu
Huku mataifa ya Ulaya na yale yaliyostawi duniani yakifunga mipaka yao katika juhudi za kukabiliana na na ya maambukizi ya coronavirus, mamilioni ya watu hawajakuwa wakizingatia ushauri wa kuosha mikono na kutokaribiana uliotolewa Shirika la Afya Duniani, WHO.
Karibu watu bilioni moja wanaishi katika mitaa ya mabanda na wanakadiria hadi 30% ya idadi ya watu wanaoishi maeneo ya mjini.
Makazi hayo yanakumbwa na msongamano wa watu, huku mfumo wa maji taka na usafi kwa jumla ukiwa changamoto ambayo huchangia kusamba kwa haraka kwa magonjwa.
Celestine Adhiambo, 43, anaishi mtaa wa mabanda wa Mukuru nje kidogo ya mji wa Nairobi pamoja na mume wake na watoto sita.
Familia hiyo inaisha katika chumba kimoja ambacho hakina maji wata umeme. Anasema watoto wake hawawezi kutembea katika chumba hicho bila ya kugongana.
"Ni vigumu kumtenganisha mtoto mmoja na wenzake endapo kutatokea maambukizi ya aina yoyote. Hatuna nafasi katika chumba hiki. Serikali iwapeleke watu walioambukizwa hospitali,"aliambia BBC.
Mume wake anafanya kazi ya uselemala na kwa siku anayofanya kazi malipo yake ni analipwa shilingi 400 Kenya sawa na (£3.15, $4) na kila siku familia yake inatumia shilingi 50 kukunua ndoo 10 za maji.
Lakini zile siku hakuna maji familia hiyo inalazimika kuishi bila kuoga na wamezoea.

Chanzo cha picha, Mukuru Promotion Centre, Winnie Ogutu
Zaidi ya watu nusu milioni wanaishi katika mtaa wa Mukuru. Nyumba zo zimetengenezwa kutokana vipande vya maboksi na vifaa vya plastiki huku wale ambao nyumba zao ni nzuri kidogo wakiishi katika nyumba za mabati. Hakuna huduma ya uzoaji taka, huku baadhi ya taka zikitumwa moja kwa moja kwenge mto.
Shirika moja lisilokuwa la kiserikali la Mercy Mukuru linaendesha shule nne za msingi zilizo na jumla ya wanafunzi 7000 katika eneo hilo.
Karibu nusu ya wanafunzi hao hawana uwezo wa kununua sabuni kwa mujibu wa mkuu wa shirika hilo, Mary Killeen.
"Nina hofu. Endapo maambukizi ya virusi vya corona yatasambaa katika eneo letu hali itakuwa mbaya sana," Bi Adhiambo anasema.
Dkt. Pierre Mpele, mwakilishi wa zamani wa WHO ambaye amefanya kazi katika nchi nyingi za Afrika Magharibi na Kati anasema familia nyingi za kiafrika zinaishi katika mazingira ya msongamano. Wakati mwingine hadi watu 12 wanaishi pamoja katika nyumba ndogo. "Suala la kujitenga halitawezekana katika maeneo mengi," alisema.
Sio watu wanaoishi katika mitaa ya mabanda pekee wanaokabiliana na changamoto ya ukosefu wa maji.
Miji ya Johannesburg na Chennai pia zilikabiliwa na uhaba wa maji mwaka jana.

Chanzo cha picha, Getty Images
Shanthi Sasindranath, mama wa watoto wawili anayeishi viungani mwa mji wa Chennai aliambia BBC: "Kukiwa na upungufu wa maji kama mwaka jana, itakuwa vigumu kupata maji safi ya kuosha mikono mara kadhaa."
Wakati kulishuhudiwa uhaba wa maji mwaka uliopita, familia yake ililazimika kununua na kutumia maji ambayo hayajatiwa dawa yaliyokuwa yakitumiwa kwa shughuli za kilimo lkutoka visima vilivyopo umbali wa kilo mita 50.
Kuna vyoo vichache vya umma ana maeneo ya kuteka maji na kuongeza kuwa watu hawazingatii ushauri wa afya kwa umma.

Chanzo cha picha, Shanthi Sasindrantah
"Katika treni, watu wanakohoa karibu na uso wako, bila kufunika mdomo. Nikihoji hali hiyo baadhi yao wanasema samahani, lakini wengine wanagombana ."
Jamaa na marafiki humtembelea kwake karibu kila siku lakini Bi Sasindranath hajapata jibu la jinsi ya kudhibiti utangamano huo.
"Nawaambia watoto wangu kunawa mikono pole pole kwa muda ili kuhakikisha inakuwa sawa. Nawahimiza kuosha mikono kila wanapotoka nje kucheza hata kama ni kwa dakika tano. Kama familia hatusafiri kama ilivyokuwa ada yetu."


Daktari Poppy Lamberton, mhadhiri anayetoa huduma za afya katika chuo kikuu cha Glasgow nchini Uingereza,amesema serikali zinaitaji kuongeza juhudi za kuzuia maaambukizi.
"Baadhi ya nchi ni masikini, blakini sio masikini kama baadhi ya raia wake. Endapo mlipuko utatokea zinatakiwa kutenga jamii nzima."

Chanzo cha picha, Dr Pierre Mpele
WHO imesema inafanya kazi ya kuzisaidia nchi kuweza kukabiliana na janga hili, lakini Dokta Mpele anataka suala hili lije na muongozo ambao utafanya kazi kwa nchi zinazoendelea.
Pia ametaka kuwepo kwa jitihada za kuhusisha viongozi katika jumuia kabla hali haijawa mbaya barani Afrika.
''Hali ya maambukizi Afrika haiko kwa kasi. Ripoti nyingi za wagonjwa ni wale watu waliosafiri kutoka China au Ulaya. Hatujui kwanini havisambai kwa haraka,'' alisema.
WHO imesema usambaaji ni wa chini kwa watu ambao hawana historia ya kusafiri













