Uganda yakumbwa na ugonjwa wa matende ambao ni nadra sana

Chanzo cha picha, BBC/Allan Atulinda
Akiwa ameketi chini kudondoa maharagwe, miguu ya Margaret Tindimutuma iliyofura ina maumivu.
Mama huyo anaugua aina ya ugonjwa wa matendee ambao ni nadra sana na umetaabisha sana familia yake.
"Kila wakati mimi huwa na mzio tangu nikiwa mdogo. Kwa hiyo miguu yangu ilipoanza kufura na kufanya kama majipu, nilichukulia ni jambo la kawaida," mama huyo mwenye umri wa miaka ya 80, anasema hivyo akiwa ameketi mkekani katikati ya uwanja wa nyumbani kwake.
"Lakini maumivu yaliendelea kuongezeka, nilikuwa ninahisi kuchomwa mwili mzima. Ngozi katikati ya vidole vya miguuni ilianza kupasuka na kufanya vidonda. Kisha vijana wangu wakaanza kuumwa. Na hapo ndipo nilipoanza kujiuliza kama pengine nimewarithisha ugonjwa huo."
Vijana wake wawili walifariki 2017, na mwaka uliotangulia baada ya kupata vidonda mguuni na baadaye kupata maambukizi ya ugonjwa huu.
When we could afford painkillers, my husband would walk around. But by the time he died, he couldn't even leave his bed"

Wakiwa wameketi katika kiti cha mbao uani na Hope Amooti, mjane wa mmoja ya vijana walioaga dunia alianza kuonyesha picha za wakati wakiwa na furaha.
Mume wake,18, alikuwa mrefu na katika picha nyengine anaonesha tabasamu la nguvu na kuangalia chini kwa haya.
"Uchungu wa miguuni ulipomzidia, mgongo wake ulikuwa unamuuma.
"Tulipomnunulia dawa za kupunguza maumivu, alikuwa anaweza kutembea. Lakini hadi wakati anafariki, hakuweza hata kutoka kitandani," Bi Amooti anasema huku akijinga macho kwa jua la asubuhi lililochomoza.

Chanzo cha picha, BBC/ALLAN ATULINDA
Katika picha nyengine, kaka mdogo wa Bi Amooti ameketi na dada yake kwenye hema. Hana viatu na unaweza kuona miguu yake inabonyea, na ngozi ya katikati ya vidole vya miguu ikitoka.
'Kukataliwa na wakwe'
Enid Twasiima, mmoja wa binti za Tindimutuma ambaye alikuwa ameolewa katika kijiji kingine, alikuwa mgonjwa.
Mkono wake ulianza kubadilika rangi na kuwa wa kijivu na pia ukaanza kufura mfano wa gogo.
Kisha ugonjwa huo ukasambaa hadi kwenye miguu yake. Familia ya mume wake ilimkataa na akarejea katika kijiji cha Kyakatoma na watoto wake.

Chanzo cha picha, BBC/Allan Atulinda
"Nilikuwa ninalima chakula cha kutosha kwa ajili ya familia yangu. Miaka mitano sasa, nimekuwa tu nyumbani,"Bi. Tindimutuma anasema.
Ms Twasiima, akiwa ameketi kwenye kiti, anasikiliza kwa makini. Anafunika kidonda chake kwa kutumia kitambaa kichafu, kilichozungushwa mguuni kujikinga dhidi ya nzi.
Katikati ya mazungumzo, jirani yake akaingia. Upande wa chini wa mguuni ana kidonda kinachotoka maji ambacho kinatoa harafu mbaya.
2015, timu ya wanasayansi walitembelea kijiji hicho kufanya utafiti kuhusiana na ugonjwa huo ambao ni nadra sana - kulingana na Shirika la Afya Duniani (WHO) miongoni mwa magonjwa ya maeneo ya kitropiki yaliyopuuzwa.
Watafiti hao walichukua mchanga kidogo pamoja na vipimo vya wagonjwa.

Chanzo cha picha, BBC/Allan Atulinda
Matokeo yalionesha kwamba ugonjwa huo wa matende ambao umekumba makumi ya watu magharibi mwa Kamwenge, ni aina nadra sana ya matende inayofahamika kama podoconiosis kwa Kiingereza.
Huku aina ambayo imezoeleka ya ugonjwa wa matende ikiwa ni yenye kusababishwa na minyoo aina ya mikrofilaria, unaosambazwa na mbu. Matokeo yanaonesha kwamba chimbuko la ugonjwa huo ni madini ya eneo hilo ambalo mchanga wake ni wa volkano.
"kuna wadini kama vile ya chuma, silikoni, alumini, yakiwa katika chembechembe ndogo hupenyeza kwenye ngozi," amesema Mtaalamu wa magonjwa ya kuambukiza, Christine Kihembo, ambaye aliongoza utafiti huo wakati anafanya kazi katika Wizara ya Afya.
"Madini hayo yanaathiri mtiririko wa kawaida wa majimaji kwenye viungo vya mwili, na kusababisha maumivu na uvimbe. Hali hiyo hujitokeza baada ya madini hayo kuingia mwilini kwa miaka kadhaa."

Baadhi ya taarifa zinaonesha kwamba zaidi ya watu 300 huenda wameathirika na ugonjwa huo katika eneo la Kamwenge pekee. Visa kidogo vimeshuhudiwa katika maeneo ya mbali ya kusini mwa Kisoro.
Ugonjwa wa Podoconiosis pia umebaini katika nchi za Ethiopia, Rwanda na Cameroon. Aina hii ya ugonjwa wa matende inakadiriwa kuathiri watu milioni nne kote duniani, kulingana na Shirika la Afya Dunia.
Ugonjwa usiokuwa na tiba zaidi na dawa za kupunguza maumivu

Familia za eneo la Kamwenge hutegemea kilimo na hutumia vifaa vya kilimo vya kawaida tu pamoja na mikono yao.
Baada ya utafiti huo kuchapishwa, wanasayansi waliwashauri wana vijiji kuvaa vifaa vya kujikinga, kunawa mikono na kuosha miguu yao punde tu baada ya kumaliza shughuli za kilimo.
Viatu aina ya 'Gumboots' ikiwa kitu cha muhimu sana kwa wale wenye uwezo
Katika kijiji jirani, Provia Arinaitwe, 39, anapiga ukelele wakati anainuka kutoka mkekani mbele ya nyumba yake ndogo.
Pia amepata ugonjwa wa malaria na hilo limefanya kutoweza kuhudumia miguu yake vizuri jambo ambalo limerejesha maumivu ya miguuni.
Miguu yake ina alama za weusi lakini Bi Arinaitwe hana vidonda ambavyo pengine vingekuwa vinatoa harufu mbaya.
Yuko katika hali nzuri kuliko mwengine yeyote wakati huo.
When I use salt three times a day, it gives me great relief... But sometimes I have no money to buy the salt"

Baada ya kuosha miguu yake kwenye karai ya plastiki, anapima vijiko vitatu vya chumvi kwenye kiganja cha mkono, na kuitumbukiza kwenye karai kisha binti yake anaongeza maji.
Baada ya hapo anatumbukiza miguu yake kwenye maji hayo kwa dakika 15.
"Ninapofanya hivi mara tatu kwa siku, huwa napata nafuu kubwa. Ninaweza kwenda kazini.
"Lakini wakati mwingine sina hata pesa ya kununu chumvi na hapo malengelenge na maumivu hurejea," anasema, huku akiwa anajikunyata wakati anatoa miguu yake kwenye maji na kuvaa sapatu.
Dr. Kihembo anasema kuwa wakati wa utafiti huo, ilibainika kwamba watu ambao wanaosha miguu yao ndani ya saa mbili baada ya kumaliza kazi za shambani wanapunguza uwezekano wa kuambukizwa ugonjwa wa podoconiosis mara 11 ikilinganishwa na wale ambao huchukua muda mrefu kuosha miguu yao baada ya kutoka shambani.
Dawa zinazotibu aina nyengine ya matende tofauti na huu ambao ni nadra sana, zinapatikana madukani nchini Uganda lakini waathirika wa ugonjwa wa podoconiosis wanaweza tu kupata nafuu kupitia dawa za kupunguza maumivu ambazo bei yake si ghali mno.












