William Ruto: Naibu rais wa Kenya akiri 'walaghai' waliingia ofisini mwake jumba la Harambee House jijini Nairobi
Ofisi ya William Ruto ilivamiwa na wachunguzi kufuatia madai ya mpango wa kununua silaha

Chanzo cha picha, Getty Images
Naibu rais wa Kenya William Ruto amekiri kwamba watu waliopanga kashfa ya mamilioni ya fedha walitembelea ofisi yake katika jumba la Harambee House Annex.
''Mbali na dakika 23 katika ofisi yake'' bwana Ruto alituma ujumbe wa twitter akisema, ni ofisi gani za serikali zinazohusishwa na zabuni hiyo ambazo walaghai hao walitembelea?.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 1
Aliongezea kwamba kile kinachoendelea dhidi ya afisi yake ni ufadhili wa porojo katika vyombo vya habari na kusisitiza kuwa afisi yake haikununua vifaa vya kijeshi vya serikali.
Lakini vyombo vya habari nchini Kenya vilisema kwamba chapisho hilo la hivi karibuni linaonesha kwamba aliyekuwa waziri wa michezo Rashid Echesa ambaye anakabiliwa na mashtaka ya kuhusika katika mkataba bandia wa kununua silaha, alitumia ofisi ya bwana Ruto ili kufanya biashara yake.
Katika chapisho jingine la twitter, bwana Ruto alimtaja bwana Echesa na wengine kuwa ''walaghai'' kuhusiana na ripoti kuhusu madai hayo kwamba bwana Echesa alitumia ofisi ya Ruto katika jumba la Harambee ili kufanya mikutano yake.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 2
Bwana Ruto ambaye ofisi yake ilivamiwa na wachunguzi wikiendi iliopita , alisema kwamba hakukutana na waziri huyo wa zamani pamoja na wafanya biashara wake waliotembelea ofisi yake na hakuhusika katika mkataba huo uliodaiwa kugharimu dola milioni 397.
Bwana Echesa ambaye alikana madai hayo pamoja na wenzake waliachiliwa kwa dhamana ya shilingi milioni moja kila mmoja wao.
Amedaiwa kujaribu kujipatia dola za Marekani 395, 442,000 kutoka kwa wafanyabiashara wa Poland kwa kuwaahidi zabuni ya kuiuzia idara ya ulinzi ya Kenya vifaa vya kijeshi.
Waziri huyo wa zamani wa michezo alifutwa kazi na rais Uhuru Kenyatta mnamo mwezi Machi kutokana na sababu zisizojulikana.
Aliambia gazeti la Daily Nation wakati huo kwamba hakuambiwa kwanini alikua anafutwa kazi , lakini aliamini ni kutokana na kumuunga mkono bwana Ruto.
Stakhabadhi za mahakamani zinaonesha kwamba maafisa wa polisi wanaamini 'biashara' hiyo ilifanyika mwisho wa mwaka jana katika afisi ya naibu wa rais katika jumba la Annex.
Tayari majasusi nchini Kenya wanaendelea kuwahoji wafanyakazi katika ofisi ya naibu huyo. Bwana Echesa pia ameshtakiwa na kujifanya kuwa msaidizi wa kibinafsi wa naibu wa rais William Ruto .
Polisi wanasema kwamba bwana Echesa tayari alikua amelipwa takriban dola 115,000.
Bwana Ruto ameshutumiwa sana kufuatia kesi hiyo, huku viongozi wengine wakihoji vipi ulaghai wa hali ya juu unaweza kufanyika katika afisi yake bila yeye kujua.
Bwana Ruto ameshutumu ripoti hizo kama porojo zilizofadhiliwa.












