Lee Njiru: Wasiompenda Daniel Arap Moi 'walimuua mara 14' kabla ya kifo chake rasmi

Chanzo cha picha, Getty Images
Msemaji wa aliyekuwa rais mstaafu wa Kenya Daniel Arap Moi anadai kwamba "watu wasiompenda Moi walimuua mara 14" tangu 1983 kabla ya kifo chake leo Jumanne.
''Tangu 1983 nimekuwa nikihesabu katika karatasi, amekufa mara 14.''
''Hayo ni kwa mujibu ya watu wasiompenda , lakini hiki ndio kifo chake rasmi'', Lee Njiru alikuwa akizungumza na runinga ya Citizen nchini Kenya.
Anasema kwamba amekuwa akifanya kazi naye tangu Agosti 1978.
Lee Njiru ambaye amekuwa katibu wa habari wa rais mstaafu amemfanyia kazi kiongozi huyo kwa muda wa zaidi ya miaka 40.
Njiru alijiunga na kiongozi huyo wa zamani baada ya kumhudumia rais wa kwanza wa Jamhuri ya Kenya mzee Jomo kenyatta mwaka1978.
Kulingana na Njiru , Mzee Moi amekuwa mwalimu wake, Kiongozi wake mtu aliomsadia katika pilkapilka za maisha mbali na kumlinda kama 'mboni ya macho yake'.
Akizungumza na runinga ya Citizen kwa njia ya simu Njiru amesema ametembea maeneo yote ya Kenya na ulimwengu kwa jumla kupitia kiongozi huyo .
''Alinionyesha jinsi ya kukabili pandashuka za maisha, alikuwa mwalimu wangu, babangu alinifunza jinsi ya kupenda watu na jinsi ya kuishi nao''.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Anasema kwamba Moi alimchukua akiwa kijana kutoka mashambani akamjenga na kuwa mtu mwenye mali.
''Alinisaidia kujenga nyumba katika eneo la kieleshwa jijini nairobi kwa lengo la kumhudumia yeye''.
Anasema kwamba anadhani anamjua Moi zaidi ya mtu mwengine yeyote yule kwa kuwa aliajiriwa kufanya kazi hiyo na kwamba amemhudumia kwa muda mrefu zaidi.
Nimetembelea kila sehemu nchini Kenya kila aneo ambalo ametembelea nimetembea alinifanya kuwajua watu.. Leo mungu ametangaza rasmi kwamba amemchukua na ni lazima tukubaliane na hilo.
Aliongezea kwamba katika siku zake za mwisho amemuona kiongozi huyo kutoka kuwa mtu aliye na nguvu zake hadi aliyeanza kudhoofika kutokana na umri wake.
Ameongezea kwamba wiki iliopita alihisi uchovu hali ya kwamba hakuweza kusoma gazeti wala kutazama runinga akihisi kwamba kulikuwa na kitu kikubwa ambacho kilikuwa kinakaribia kufanyika.
Anasema kwamba wakati alipoanza kuugua alipelekwa katika hospitali ya Nairobi ambapo chumba chake kilibadiliushwa na kuwa chumba cha kumuuguza
Anasema kwamba katika siku zake za mwisho amemuona kiongozi huyo kutoka kwa mtu aliye na nguvu zake hadi aliyeanza kudhoofika kutokana na umri wake.
Alimalizia kwa kusema kwamba Moi hana umri wa miaka 95 kama inavyoangaziwa na vyombo vya habari bali kati ya miaka 102 na 103 .
Alikuwa akiniambia kwamba wachana na yalioandikwa katika kitambulisho.Anasema kwamba wakati alipoanza kuugua alipelekwa katika hospitali ya Nairobi ambapo chumba chake kilibadilishwa na kuwa chumba cha kumuuguza.













