Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Habari kuu zilizogonga vichwa vya habari 2019: Khashoggi, Mugabe, Trump. Kim Jong Un, Iran, Kimbunga Idai, lori la mafuta na Afcon
Mwaka wa 2019 ni mojawapo ya miaka iliokuwa na habari chungu nzima, kutoka habari za kusikitisha, za kufurahisha na hata zile za kushangaza.
Miongoni mwao ilikuwa habari ya kuskitisha ya mauaji ya aliyekuwa mwandishi nchini Saudi Arabia, Jamal Khashoggi aliyeuawa kwa kukatwakatwa ndani ya kile kinachodaiwa kuwa ubalozi wa Saudia nchini Uturuki kama inavyosimuliwa hapa.
1. Jinsi Jamal Khashoggi alivyouawa
Nilitembea katika barabara iliojaa miti katika eneo tulivu mjini Istanbul na kukaribia nyumba moja iliopakwa rangi ya maziwa ikiwa na kamera za CCTV.
Mwaka mmoja uliopita mwandishi wa Saudia ambaye yuko mafichoni alitembea katika eneo hilo hilo.
Jamal Khashoggi alionekana katika kamera za CCTV. Ilikuwa picha yake ya mwisho. Aliingia katika ubalozi wa Saudia na aliuawa na kundi moja la wauaji.
Lakini ubalozi huo ulikuwa na kamera zilizofichwa za CCTV ambazo zilikuwa zimewekwa na majasusi wa Uturuki.
Kanda hizo zilizorekodiwa zimesikika na watu wachache sana, wawili kati ya watu hao sasa wamezungumza na kipindi cha BBC cha Panorama.
Jasusi wa Uingereza Baroness Hellena Kennedy alisikia wakati Jamal Khashoggi alipokuwa akifariki.
''Tisho la kusikiliza sauti ya mtu, hofu katika sauti ya mtu na kwamba unamsikiza mtu aliye hai . Inakufanya uogope mwilini''.
Kwa habari zaidi bonyeza Link hapa: Mauaji ya Jamal Khashoggi: Kanda za siri za mauaji hayo zafichuliwa.
2. Trump akutana na rais wa Korea Kaskazini
Baada ya tofauti za kidiplomasia na matamshi ya chuki kati ya Marekani na Korea Kaskazini yaliofuatiwa na hatua ya Korea Kaskazini kufanyia makombora yake majaribio mbali na vitisho vya Marekani, rais wa Marekani Donald Trump na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un hatimaye walisalimiana.
Lakini hakuna mtu alifahamu kile kingeendelea. Hapa tunachapisha picha kutoka mkutano huo kuonyesha kile kilichotokea.
"Nimefurahi kukutana nawe Bw Rais," ni maneno aliyoyatamka Bw. Kim alipokutana na Bw Trump.
Walisaliamiana kwa mkono kwa muda lakini muda walishikana mikono ulikuwa mfupi kuliko ule wa kawaida wa Trump.
Kwa picha zaidi bonyeza link: Kwa Picha: Kusalimiana kwa Donald Trump na Kim Jong-un kuna maana gani?
3. Iran yakamata meli ya Uingereza eneo la Ghuba
''Kutakuwa na 'madhara makubwa''ikiwa Iran haitaachia meli ya mafuta ya uingereza wanayoishikilia'',
Ni matamshi ya waziri wa mambo ya kigeni wa Uingereza Jeremy Aunt aliyekuwa akitoa onyoa kwa iran kufuatia hatu ya taifa hilo kukamata meli iliokuwa ikipeperusha bendera ya Uingereza katika mkondo wa bahari wa Hormuz.
Hatua hiyo ilijiri baada ya wamiliki, wa meli ya Stena Impero kushindwa kufanya mawasiliano na meli hiyo.
Kamati ya dharura ya serikali hiyo, cobra, baadaye ilikutana kwa ajili ya kuzungumzia jambo hilo.
Bwana Hunt alisema kwamba kitendo hicho ''hakikubaliwi kabisa.
''Tunajua wazi kuwa hali hii haitakuwa rahisi kuitatua, kutakuwa na madhara makubwa,'' alisema.
Bonyeza link kwa habari zaidi:Iran yakamata meli ya Uingereza eneo la Ghuba
4. Kimbunga Idai: 'Janga kubwa' nchini Msumbiji, Zimbabwe na athari kwa Afrika mashariki
Kimbunga Idai kilisababisha "janga kubwa" katika mataifa ya kusini mwa Afrika na kuathiri laki kadhaa za watu kama sio mamilioni, Umoja wa mataifa unasema.
Eneo hilo lilikabiliwa na mafuriko katika sehemu nyingi na uharibifu katika nchi za Musmbiji Zimbabwe na Malawi.
Huku kukiwa na ripoti kwamba takriban angalau watu 400,000 waliachwa bila ya makaazi Msumbiji ya kati, shirika la kimataifa la msalaba mwekundu lilionya kwamba huenda ikachukua siku kadhaa kabla ya athari kamili ya "janga la kibinaadamu" kujulikana dhahiri.
5. Robert Mugabe afariki dunia akiwa na miaka 95
Rais wa zamani wa Zimbabwe, Robert Mugabe aliaga dunia.
Mmoja wa wanafamilia walithibitishia BBC kuwa, Robert Mugabe alifariki dunia akiwa na miaka 95.
Mugabe alikuwa nchini Singapore akipokea matibabu kwa muda mrefu wakati wa kifo chake.
Aliiongoza Zimbabwe kutoka 1980 hadi 2017, alipong'olewa madarakani na makamo wake kwa msaada wa jeshi.
6. Waliokufa kwenye ajali ya ndege ya Ethiopian Airlines watambuliwa
Famlia na marafiki zilisubiri taarifa mjini Nairobi kuhusu hatma ya wapendwa wao waliokua wamesafiri kwa ndege ya Ethiopia iliyopata ajali .
Ndege hiyo ilitarajiwa kuwasili mjini Naorobi kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo kanyatta saa nne unusu kwa saa za Afrika Mashariki.
Taarifa ya Kampuni ya ndege ya Ethiopian Airlines iilisema abiria kutoka nchi 33 waliosafiri kwenye ndege iliyopata ajali wote wamekufa, kulingana na Msemaji wa Kampuni hiyo Asrat Begashaw.
Kwa habari zaidi bonyeza Link: Ethiopian Airlines: Uraia wa abiria waliokufa watambuliwa
7. Tanzania: Watu 90 wafariki dunia baada ya lori la mafuta kulipuka
Watu 90 walifariki na wengine zaidi ya 65 kujeruhiwa baada ya lori la mafuta kulipuka katika eneo la Msamvu mjini Morogoro, Mashariki mwa Tanzania.
Polisi wanasema watu hao walikuwa wakichota mafuta baada ya lori hilo kupinduka katika bara bara kuu wakati ajali hiyo ilipotokea.
8. Kimbunga Kenneth: Tanzania yanusurika, Msumbiji yachapwa
Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini Tanzania (TMA) ilitangaza kuwa Kimbunga Kenneth kimeongezeka kasi na kilitarajiwa kufika pwani ya kusini ya Tanzania na kaskazini mwa Msumbiji kuanzia usiku wa Alhamisi wiki hii.
Kwa mujibu wa TMA, kimbunga hicho kilikuwa kilomita 450 kutoka pwani ya Mtwara na kilikuwa na kasi ya kilomita 130 kwa saa.
Kufikia usiku wa tarehe 24 Aprili kimpunga hicho kilitabiriwa kuwa na kasi ya kilomita 250 kutoka pwani ya Mtwara, kikiwa kinasafiri kwa kilomita 150 kwa saa.
Kwa habari zaidi Bonyeza Link: Kimbunga Kenneth 'kuzikumba Msumbiji, Tanzania Alhamisi'
9. Kenya yaizamisha Tanzania 3-2 AFCON 2019
Ubishi umekwisha, Kenya ni mbabe wa Tanzania.
Baada ya presha kupanda na kushuka kwa muda mrefu nje ya uwanja, dakika 90 za ndani ya uwanja zilitoa majibu.
Kenya iliwafunga Tanzania goli 3-2 katiia michuano ya kombe la Afcon 2019
Kwa habari zaidi bonyeza Link: Jinsi Kenya ilivyoizamisha Tanzania