Alshabab wamekiri kuivamia hoteli Mogadishu iliyo karibu na ofisi ya rais

Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 2

Vikosi vya usalama nchini Somalia hatimaye vimewashinda washambuaji waliovamia hoteli ya SYL katiika mjii mkuu Mogaadishu.Makabaliano hayo ya masaa saba yamesababisha vifo vya wanajeshi wawili na raia watatu.

Mamlaka ya usalama nchini humo inaripoti kuwa wanajeshi wengine wawili na raia tisa walijeruhiwa.

''Kufikia sasa,vikosi vya usalama vimewaokoa watu 82.wakiwa rai na maafisa wa serikali,''Naibu wa kamanda wa polisi wa Zakia ameandika kwenye mtandao wa Twitter.

Washambuliaji watano wanadaiwa kutekeleza shambulizi hilo.

Kundi la wapiganaji wa Al Shabaab limekiri kutekeleza shambulizi hilo.Washambuliaji walitumia bunduki na bomu kuvamia maafisa wa vikosi vya usalama waliofika kukabiliana nao.

Washambuliaji wote watano waliwauwa katika makabiliano kulingana na maafisa wa usalama.Hata hivyo idara ya polisi imeonya kuwa idadi ya raia waliowauwa inaweza kuongezeka

Wanamgambo wa Alshabab nchini Somalia wamekiri kuhusika na shambulio linaloendela katika hoteli ya kifahari mjini Mogadishu SYL nchini Somalia na makabiliano bado yanaendelea.

Polisi nchini humo inasema kuwa imewakoa watu 82 waliokuwemo ndani ya hoteli hiyo.

Taarifa zinasema kuwa makundi ya wanajeshi wanaonekana kwenye barabara inayoelekea katika kasri ya rais.

Taarifa ambazo hazijathibitishwa zinasema kuwa makumi kadhaa ya watu waliokuwemo ndani ya hoteli ya SYL wanaripotiwa kuokolewa, na washambuliaji wawili wameuawa na vikosi vya usalama vya Somalia, huku wengine watatu wakiwa bado wanaendesha mashambulio ndani ya hoteli.

Kituo cha redio cha Dalsalam mjini Mogadishu kimesema kenye ukurasa wake wa twitter kuwa wabunge wawili kwa jina Mahgan pamoja na waziri wa zamani wa mambo ya ndani wa Somalia Abdulkadir Ali Omar wamejeruhiwa katika shambulio lilitokea katika hoteli ya SYL:

Vyombo vya habari nchini humo vimeripoti kuwa shughuli ya uzinduzi wa kitabu ilikua ikiendelea ndani ya hoteli ya SYL wakati shambulio hilo lilipotokea ambapo watu zaidi ya 70 walikua wamekusanyika kwa ajili ya tukio hilo.

Walioshuhudia wanasema kuwa wapiganaji 7 waliokua na silaha huku wakiwa wamevalia sare polisi waliingia kwenye uwanja wa hoteli hiyo na kuanza kufyatua risasi na makabiliano bado yanaendela ndani ya hoteli hiyo.

Imeripotiwa kuwa hoteli ya SYL ni maarufu sana kwa wanasiasa na wasomi wa kisomali.

Shambulio hili ni la kwanza kutekelezwa na kikundi cha Alshabab katika mji mkuu wa Somalia, tangu kuuawa meya wa mji huo miezi minne iliyopita...Meya wa Mogadishu afariki baada shambulio la bomu

Unaweza pia kusoma:

Tutaendelea kukupa maelezo zaidi juu ya shambulio hili...