Mageuzi ya Macron ya hazina ya uzeeni yaibua maandamanao makubwa kuwahi kushuhudiwa kwa miaka

Maelezo ya video, Waandamanaji katika mitaa ya Ufaransa wakishiriki maandamano makubwa ya kitaifa kuwhi kushuhusiwa kwa miaka
Iliyochapishwa

Mgomo wa kitaifa umeathiri shule na usafiri wa umma nchini Ufaransa.

Wafanyakazi wameghabishwa na mpango wa kuwalazimisha kustaafu kuchelewa ama malipo yao ya uzeeni yapunguzwe.

Maafisa wa polisi, mawakili, wafanyakazi wa hospitali na viwanja vya ndege wameungana na wafanyakazi wa mashuleni na sekta ya usafiri wa umma katika mgomo wa kitaifa ambao huenda ukajumuisha mamilioni ya watu.

Maandamano hayo makubwa ambayo hayajawahi kushuhudiwa kwa miaka mingi yaliidhinishwa na chama cha wafanyakazi ambacho hakijafurahishwa na mipango ya rais Macron ya kutaka kuanzisha mfumo wa malipo ya uzeeni ambapo kila siku moja iliyofanyiwa kazi inapata alama kwaajili ya mapato ya pensheni ya siku za usoni.

Mamlaka imekuwa ikijaribu kuweka mipango ya kuanzisha mfumo huo.

Gazeti la Ufaransa la Le Monde, limeelezea siku hii ya Alhamisi kama "mtihani mkubwa kwa Macron", na kuandika: "Siku zijazo kuanzia sasa kiongozi wa taifa atalazimika kufanya maamuzi."

Maandamano hayo yatadumu kwa muda gani?

Maandamano yanatarajiwa kuendelea na baadhi ya viongozi wa vyama vya wafanyakazi wameonya kwamba mgomo huo utaendelea hado pale Bwana Macron atakapoachana na ahadi yake ya wakati wa kampeni ya kubadilisha mfumo wa malipo ya uzeeni.

Matokeo ya kura ya maoni yameonesha kwamba asilimia 69 ya wafanyakazi wa umma wanaounga mkono mgomo huo wengi wao wakiwa ni kati ya umri wa miaka 18 hadi 34.

Utawala wa Bwana Macron unatarajia kutojirejelelea kwa mgomo mkubwa wa kitaifa kuhusu mabadiliko ya mfumo wa pensheni uliofanyikwa mwaka 1995, ambao ulisambaratisha mfumo wa usafiri wa umma kwa wiki tatu na hatimaye serikali ililazimika kubadilisha maamuzi yake

Je ghasia za upande wa usafiri ni mbaya kiasi gani?

Usafiri wa umma umeathirka pakubwa huku asilimia 90 ya safari za treni za mwendo kasi na zile za kawaida zikifutwa. Mjini Paris, ni njia tano tu kati ya 16 za usafiri wa treni zinazofanyakazi.

Treni za safari za kimataifa kama Eurostar na Thalys pia zimeathirika huku kampuni ya Eurostar ikitangaza kupunguza safari zake hadi Desemba 10.

Vilevile, safari nyingi za ndege zimefutwa.

People ride bikes on the streets of Paris during a strike by French SNCF railway workers on 5 December, 2019

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Baadhi ya wale walioathiriwa na mgomo wa mabasi na treni waliendesha baiskeli zao mjini

Usafiri wa umma umeathirka pakubwa huku asilimia 90 ya safari za treni za mwendo kasi na zile za kawaida zikifutwa. Mjini Paris, ni njia tano tu kati ya 16 za usafiri wa treni zinazofanyakazi.

Treni za safari za kimataifa kama Eurostar na Thalys pia zimeathirika huku kampuni ya Eurostar ikitangaza kupunguza safari zake hadi Desemba 10.

Vilevile, safari nyingi za ndege zimefutwa. Shirika la Air France limetangaza kufuta asilimia 30 ya safari zake za ndani pamoja na asilimia 30 ya safari zake za kimataifa za muda mfupi kwa sababu ya kukosekana kwa waongoza ndege angani.

A poster reads: "All on strike on 5 December" - at the Bourse du Travail during preparations for the national strike against the French government's pension reform plans, in Nice

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Watu katika mji wa Nice wakijiandaa kwa maandamano wakiwa wameshikilia bango lililoandikwa: " Kila mtu katika maandamano tarehe 5 Disemba"

Ndege ya gaharama za chini ya EasyJet imefuta safari zake 223 za ndani pamoja na safari za kimataifa za muda mfupi, na kutaka abiria watarajie kucheleshwa kwa safari zao.

Ni kina nani tena wanaogoma?

Wauguzi, wafanyakazi wa hospitali, mawakili, maafisa wa polisi, waokotaji takataka, na wafanyakazi katika sekta ya nishati ni miongoni mwa wanaoandamana.

Wizara ya afya ya Ufaransa imesema bado haijafahamika hospitali zitaathirika kwa kiwango gani lakini wamejiweka sawa kukabliana na athari za mgoro huo.

Wazazi wenye watoto wa shule ya msingi pia wataathirika.

A boy enters in his classroom at the Chaptal elementary school in Paris, 2 September 2019

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Idadi kubwa ya watoto wa shule za msingi kote nchini Ufaransa wataathiriwa na mgomo

Chama kikubwa cha walimu wa shule ya msingi kimesema kinatarajia shule zaidi ya nne kati ya kumi kufungwa kote nchini humo.

Karibia asilimia 70 ya walimu wa shule za msingi wanatarajiwa kushiriki maandamano hayo.

Chama cha walimu wa sekondari kinatarajia walimu asilimia 60 kushiriki mgomo japo shule zitaendelea kufunza.

Wakulima ambao kiwango chao cha pensheni ni cha chini zaidi nchini humo wamesema hawatashiriki mgomo huo.

Wafuasi wa chama cha Labourwakiandanana mjini Marseille

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Wafuasi wa chama cha Labourwakiandanana mjini Marseille

Vuguvugu la "yellow-vest" kwa jina jingine "gilets jaunes" limethibisha kushirika maandamano hayo.

"Gilets jaunes" ni kina nani?

Vuguvugu hil o lilianzishwa mwaka 2018 ambali lilianzishwa na waandamanaji waliopinga vikali kuongezeka kwa kodi ya mafuta ya dizeli lakini kwa sasa limepanuka zaidi na kuanza kuangazia kuongezeka kwa gharama ya maisha na sera za kiuchumi za rais Macron.

Mageuzi ya akiba ya uzeeni ya Macron ni kweli ni yenye utata?

French President Emmanuel Macron

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Hadhi ya rais wa Ufaransa Emmanuel Macron imeingia dosari kutokana na mageuzi nchini Ufaransa

Kwa sasa Ufaransa ina mifumo kadhaa ya malipo ya uzeeni na Bwana Macron anataka kuundwe mfumo mmoja ambao alisema hautakuwa na mapendeleo kwa kundi lolote.

Mpango wake mpya unalenga kutoa alama kila siku ambayo mtu atafanyakazi, na baadaye alama hizo zibadilishwe kuwa mapato ya uzeeni.

Katika kipindi cha miaka 10 iliyopita, umri wa kustaafu uliongezwa kutoka miaka 60 hadi 62 lakini bado umri huo ni wa chini mno ukilinganishwa na mataifa mengine yaliyoendelea. Mfano umri wa kustaafu Uingereza ni miaka 66.