Maandamano ya Iran: Video zafichua ukatili ambao utawala ulijaribu kuificha dunia

Chanzo cha picha, Reuters
Video moja iliyochukuliwa kupitia mlango wa nyumba inaonekana ikimuonesha mwanamke akimtazama kijana mmoja mdogo akiwa amelala kwenye damu kando ya barabara, huku watu waliokuwa wakiwakimbia polisi wakipita na kumkanyaga chini.
Nyingine iliyochukuliwa kutoka katika mji wa kusini wa Shiraz ulionesha umati wa watu wakijaribu kumsaidia mtu ambaye amepoteza fahamu aliyekuwa amelala chini huku watu wengine wakijaribu kuutoroka mtaa uliokuwa umejaa moshi na sauti zikisikika za watu waliokuwa wakipiga kelele kwa hofu pamoja na milio ya risasi.
Ya tatu , ilichukuliwa kutoka ndani ya gari lililokuwa likiendeshwa katika mji mkuu Tehran, ambamo mwanamke aliweza kusikika akipiga mayowe huku mapolisi waliokuwa wamevalia sare wakimtia nguvuni mwanamume
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 1

Ilikuwa ni hofu ya picha za aina hiyo ambazo ziliwafikia wakazi wa maeneo ya dunia ambazo ziliwachochea maafisa wa Iran kufunga intaneti kwa zaidi ya siku nane mapema mwezi huu , wakati maandamano dhidi ya ongezeko kubwa ka bei ya mafuta yaliposambaa kote nchini humo. Na sasa intaneti imerejeshwa kwa muda , video zimekuwa zikionekana kwenye miytandao ya kijamii zinazoonyesha ukatili wa serikali katika kuzima maandamano kuwa mkubwa kuliko ilivyohofiwa awali . Utambulisho na hadithi za waandamanaji waliopoteza maisha yao zimejitokeza.
Maafisa wa Iran hawajatoa idadi yoyote rasmi ju ya watu waliokufa na majeruhi , lakini shirika la haki za binadamu la Amnesty International limepokea kile linachokiamini kuwa ni taarifa za kuaminika kwamba waandamanaji takriban 143 waliuawa baada ya kulipuka kwa maandamano tarehe 15 Novemba.
Shirika hilo la haki za binadamu linasema vifo husababishwa zaidi na matumizi zaidi ya silaha ya vikosi vya usalama dhidi ya waandamanaji - ingawa limeripoti kuwa mtu mmoja alikufa baada ya kuvuta hewa ya gesi ya kutoa machozi na mwingine baada ya kupigwa.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 2

Amnesty linaamini kuwa idadi ya vifo ni kubwa zaidi, na wanaharakati na duru za maafisa ndani ya Iran zimeiambia BBC idhaa ya Kipersian kuwa waliokufa ni zaidi ya 200.
Balozi wa Iran alipuuzilia idadi hiyo ya vifo akiitaja kuwa ni ya "uvumi" wiki iliyopita na akashutumu "taasisi za magharibi ''kwa kutoa "madai yasiyo na msingi ", huku rais Hassan Rouhani akisema maandamano yamesababishwa na "wapinzani" wanaotekeleza mpango ulioandaliwa na maadui wa Iran wa kigeni.
Hata hivyo video zilizochukuliwa na Wairan kwenye simu zao za smartphones - nyingi kati yake zikiwa ni za kutisha kutazama- zinakinzana na madai ya serikali.
Picha hizo zinaonekana kuonyesha maafisa wa usalama na maafisa wa kikosi cha Basij, ambao mara kwa mara hutumiwa kusaidia kuzima upinzani, wakiwapiga waandamanaji wasio na silaha katika mitaa na kuwapiga waandamanaji na kuwafyatua risasi kwenye umati wa waandamanaji.
'Maelfu walijeruhiwa au kukamatwa'
Miito inayoendelea inayowataka watu kutoa msaada wa damu inayotolewa na maafisa wa afya wa Iran pia inaonesha kuwa maelfu ya watu walijeruhiwa katika mashambulio dhidi ya waandamanaji.
Maafisa wa hospitali wameiambia BBC kuwa maafisa wa usalama wanazunguka katika mahospitali kuwasaka waandamanaji waliojeruhiwa.
Daktari mmoja amesema kuwa maafisa hao wanawatoa bendeji baadhi ya wagonjwa kubaini kama wanauguza jeraha la risasi na kumkamata mtu yeyote aliye na jeraha kama hili.
Idara ya mahakama siku ya Ijumaa ilisema karibu watu 100 "viongozi wakuu waliopanga maandamano hayo" wamekamatwa na wanajeshi wa Iran (Revolutionary Guards), na kwamba idadi kubwa ya watu walioshiriki maandamano hayo lakini hawakuhusika katika uharibifu wa mali wameachiliwa huru.

Chanzo cha picha, Fars
Lakini vyanzo vya habari ndani ya Iran vimeeambia BBC Idhaa ya Kiwajemi kwamba maelfu ya watu wanazuiliwa na mamlaka.
Katika baadhi ya miji, kambi ya kijeshi, viwanja vya michezo na shule zimeguzwa kuwa vituo vya kuzuilia watu.
Kanda ya video kutoka kwa mtu anayeishi katika jengo refu karibu na shule inaonesha jinsi watu waliozuiliwa wanavyoteswa na maafisa wa usalama.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 3

Licha tamko la kiongozi mkuu wa kidini nchini Iran Ayatollah Ali Khamenei kwamba waandamanaji hao "wanaungwa mkono na watu wa nje ya nchi", Wizara ya maswala na kiintelijensia imelimabia bunge kwamba wengi wa wale wanaozuiliwa ni vijana wasiokuwa na kazi kutoka familia masikini.
'Tunaishi kama ombaomba'
Waandishi ya nchini Iran walikabiliwana changamoto ya kuripoti kuhusu maandamano nchini humo baada ya huduma za intaneti kukatizwa.
Lakini Idhaa ya Kiwajemi, ambayo imepigwa marufuku nchini Iran, ilifanikiwa kuwasiliana na waandishi nchini humo kwa njia ya simu na njia zingine.
Licha idara ya mahakama kuonya watu kutosambaza vido za maandamano hayo na kuongeza kuwa ni kosa la kihalifu, tumepokea video kutoka kila sehemu ya nchi.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 4

Video hizo zilionesha waandamanaji wakilenga nembo za serikali, taasisi za kidini na vikosi vya usalama, pamoja na beki na vituo vy amafuta.
Kitovu cha maandamano hayo kilikuwa miji ya Wakurdi iliyopo katika mpaka wa magharibi wa Iraq, pamoja na maeneo yalio viungani mwa miji mikuu kama vile Tehran, Karaj na Shiraz.
Yote ni maeneo yanayoshuhudia viwango vya juu ukosefu wa ajira nchini.
"Bei ya mafuta ya petroli inapanda, sisi ni masikini," waandamanaji katika mji wa Shiraz walionekana wakisema katika kanda hiyo.
"Kiongozi mkuu wa kidini anaishi kama Mungu. Sisis, wananchi tunaishi kama ombaomba," walisema watu katika eneo la Malard, karibu na mji wa Tehran na kwengineko.
"Tunapinga Gaza, tunapinga Lebanon. Tunahatarisha maisha yetu kwa maslahi ya Iran" ndio maneno yaliyotumiwa na wandamanaji mjini Isfahan.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa YouTube ujumbe