Kwa nini maandamano ya Iran ni tofauti na ni vipi waandamanaji walikaidi kuzimwa kwa intaneti?

Chanzo cha picha, Getty Images
Ni nini tofauti kuhusu msururu wa maandamano nchini Iran? Kile kilichoanza tarehe 1 mwezi Novemba kama msururu wa maandamano dhidi ya kupanda kwa bei ya mafuta kulibadilika na kuwa wito wa mabadiliko ya uongozi wa serikali.
Raia wengi nchini humo walijitokeza katika barabara mbalimbali na kuunda mabango ya kiongozi huyo wa kidini ambapo walimtaja kuwa dikteta.
Siku sita za ghasia na maadamano katika miji kadhaa nchini humo licha ya mtandao kuzimwa zilikamilika huku watu 106 wakiwa wameuawa kulingana na Umoja wa mataifa na shirika la kutetea haki za kibinadamu la Amnesty International , ijapokuwa vyanzo vingine vimesema kuwa idadi ya watu waliouawa huenda ni kubwa zaidi.
Iran bado haijathibitisha idadi ya waliojeruhiwa , huku ikiwalaumu 'wakora' wanaoshirikiana na maadui wa kigeni kwa kufanya maandamano hayo.
Ijapokuwa maafisa wa Umoja wa Mataifa walitoa wito kwa utawala nchini humo kutotumia risasi dhidi ya waandamanaji , picha zilionyesha maafisa wa usalama wakiwafyatulia risasi waandamanaji moja kwa moja.
Kufikia Novemba 20 , kufuatia msako wa mali , rais wa Iran Hassan Rouhani alidai ushindi dhidi ya njama za adui wa taifa hilo
Lakini ni nini kilicho tofauti wakati huu?

Chanzo cha picha, Getty Images
Kulingana na mtaalam wa BBC nchini Iran, kile kilichosababisha maandamano 'kuwa ya kipekee' ni ghasia za kiwango cha juu, uharibifu mkubwa, na utapeli wa kikatili unaofanywa na viongozi ".
Kufuatia kisa hicho , wachunguzi wa kieneo wanasema kwamba agizo lilikuwa kutohurumia mtu yeyote na kusitisha maandamano hayo haraka iwezekanavyo ambapo maelfu ya raia walikamatwa.
Wataalamu pia waliangazia ukweli kwamba maandamano hayo hayakufanyika Tehran pekee , lakini nchi nzima huku miji mingi ikihusika.
Pia yalionekana kukosa kiongozi, na kwa mara ya kwanza katika miaka ya hivi karibuni , yalishirikisha raia wa mapato ya kadri.
Ni nani anayeandamana?

Chanzo cha picha, Getty Images
"Tuna matatizo mengi ya kiuchumi . Nyama iko bei ghali, kuku yuko bei ya juu, mayai pia yako ghali na sasa mafuta , alisema mwanadamanaji mmoja wa kike akizungumza na BBC.
Na mtaalamu huyu wa BBC anakubaliana: Kufaidhaika ndio sababu kuu ilioshinikiza maandamano hayo.
Ijapokuwa maandamano hayo yalianza katika maeneo yanayokandamizwa kiuchumi ambapo bei ya mafuta imepanda kwa asilimia 200 yalisambaa nchini humo kupitia mitandoa ya kijamii.
Iran imekuwa chini ya shinikizo za kiuchumi tangu Marekani ilipoiwekea upya vikwazo Iran 2018. Mfumuko umepanda na kufikia sailimia 40 huku ukosefu wa ajira ukiwa asilimia 15.

Chanzo cha picha, Getty Images
Kutokana na hilo , rais Rouhani ameshindwa kutimiza ahadi zake nyingi alizotoa wakati wa kampeni - hatua inayosababisha hasira kuhusu hali mbaya ya kiuchumi na ukosefu wa mabadiliko ya kisiasa, kulingana na wachunguzi.
Na sasa amepoteza idadi kubwa ya wafuasi wake , raia wa mapato ya kadri ambao wamekasirishwa na hali hiyo na kujiunga na maandamano, anasema mtaalamu huyo wa BBC.
Hofu kati ya makabila ya walio wachache na serikali pia imesababisha mgogoro zaidi katika eneo hilo ambao wanataka kujitenga na Iran.














