Israel-Gaza: Israel yachunguza taarifa za madhara yanayodaiwa kutokea

Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 2

Jeshi la nchini Israel limesema linafanya uchunguzi kuhusu ''madhara waliosababishiwa raia'' kutokana na mashambulizi ya anga katika mji wa Gaza.

Wataalamu wa afya wa Palestina walisema watu wanane wa familia moja walipoteza maisha wakati wa shambulio hilo, miongoni mwao walikuwa watoto watano.

Israel imesema shambulio hilo lilikusudiwa kwenye makazi ya Rasmi Abu Malhous, ambaye Israel inamuita kamanda wa wanamgambo kutoka kundi la kipalestina la jihad (PIJ).

Israel imesema hakuna raia yeyote aliyekusudiwa kupata madhara.

Shambulio la Deir al-Balah, katikati mwa Gaza, lilikua tukio baya katika siku mbili za mashambulizi kati ya Israel na kundi la wapiganaji wa kipalestina.

Shambulio liliekelezwa siku ya Alhamisi, muda mfupi kabla ya makubaliano ya kusitisha mapigano kuanza kufanya kazi.

Mapema siku ya Alhamisi, mashambulizi ya anga yalilenga maeneo ya Hamas kwa mara ya kwanza katika mashambulizi hayo.

Unaweza pia kusoma

Kilichotokea siku ya Alhamisi

Makombora yalipiga katika eneo la wazi, na kusambaratisha kile majirani waliielezea BBC kuwa vijumba vilivyokaliwa na watu 22 familia za ndugu wawili.

Kulikuwa na madai kuwa mmoja wao alikuwa akihusishwa na kundi la Jihad la kiislamu.

Jeshi la Israel awali lilisisitiza kuwa mkuu wa familia hiyo, ambaye jeshi limesema aliuawa, alikuwa kamanda wa wanamgambo wa PIJ kikosi cha kurusha roketi.

Israel imesema taarifa kumuhusu bado zinafuatiliwa.

Kundi la Jihad halijasema chochote kuhusu madai ya kuwa Abu Malhous alikuwa mfuasi wao.

Kinachoendelea hivi sasa

Israel imesema roketi zake za ulinzi zilidhibiti roketi mbili zilizorushwa kutoka Gaza katika mji wa Beersheva siku ya Jumamosi.

Katika majibizano, vikosi vya ulinzi vya Israeli vilisema vishambulia maeneo ya Hamas mjini Gaza. Televisheni ya Hamas al-Aqsa iliripoti.

Mpaka sasa, Israel imekwepa kulenga Hamas, ambao wanadhibiti eneo la Palestina.

Sababu ya mapigano ya sasa

Mapigano yalipamba moto baada ya Israel kumuua kamanda wa PIJ mapema siku ya Jumanne.

Israel imesema kamanda, Baga Abu al-Ata , alikuwa mtu 'hatari' aliyekuwa nyuma ya matukio ya mashambulizi na alihusika kwenye shambulio la roketi kutoka Gaza.

Zaidi ya roketi 450 zilirushwa kuelekea Israel, na mashambulizi mengine kadhaa ya anga wakati wa siku mbili za mapigano huko Gaza.

Mapigano hayo yalisababisha watu 34 kupoteza maisha na wengine 111 kujeruhiwa, huku waisraeli 63 wakiwa na uhitaji wa matibabu.

Israel imesema wapalestina 25 waliouawa walikuwa wanamgambo, wakiwemo wale waliouawa wakati wakijiandaa kurusha roketi.