Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mke wa waziri mkuu wa Lesotho Thomas Thabane auwawa kwa kupigwa risasi
Mke wa waziri mkuu aliyechaguliwa nchini Lesotho ameuwawa siku mbili kabla ya kuapishwa kwake.
Polisi wanasema mke wa Thomas Thabane, Lipolelo, ambaye walikuwa wametengana aliuwawa hapo jana Jumatano wakati akiendesha gari karibu na nyumbani kwake, katika mji mkuu wa Maseru.
Hawajakuwa wakiishi pamoja tangu mwaka 2012, baada ya Bwana Thabane kuwasilisha kesi ya talaka mahakamani.
Lesotho imekuwa na historia ya migogoro ya kisiasa.
Mnamo mwaka mwaka 2014 wanajeshi walijaribu kumpindua Bwana Thabane, pale alipokuwa waziri mkuu.
Lipolelo alishinda kesi dhidi ya mumewe wakati akiwa waziri mkuu, akitaka akuwe na cheo cha mama wa taifa, baadala ya mke wake mdogo Liabiloe Thabane.
Uchaguzi ulifanyika nchini Lesotho mapema mwezi huu na ndio wa tatu katika kipindi cha miaka mitatu kutokana na mgogoi mbaya wa kisiasa.
Bwana Thabane ataapishwa siku ya Ijumaa