Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Corona: Mwanamziki wa R & B Jeremih apata nafuu
Iliyochapishwa
Mwanamziki wa Marekani mdundo wa RnB Jeremih amesema daima atawashukuru wahudumu na madaktari waliookoa maisha yake baada ya kuugua vibaya virusi vya Covid-19. Nyota huyo sasa anapona nyumbani kufuatia kulazwa wiki kadhaa katika hospitali ya Chicago. Awali iliripotiwa kuwa kwenye mashine ya kumsaidia kupuma, lakini sasa anasema "anazidi kuwa na nguvu kila siku".