‘Hofu ya wananchi si ya bure ni hofu  halali ni hofu ya haki’

Maelezo ya video, Othman Masoud Othman:’Mchakato wa Katiba sasa ni namna gani ya kuuendea’
‘Hofu ya wananchi si ya bure ni hofu  halali ni hofu ya haki’
Iliyochapishwa

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman amesema tayari imedhihirika kuwa suala la Katiba mpya ya Tanzania ni lazima hivyo linalohitajika sasa ni kuamua namna ya kutekeleza hitaji la watanzania lililobainishwa katika ripoti mbalimbali.

Kiongozi huyo wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar ameiambia BBC katika mahojiano maalumu na mwandishi wetu  Roncliffe Odit kuwa tayari Watanzania wamejifunza masuala mengi yanayohitaji muongozo madhubuti wa Katiba mpya.