Tetesi za soka Ulaya Jumapili 01.09.2024

Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 3

Winga wa Uingereza Raheem Sterling, 29, alikataa ofa ya £650,000 kwa wiki kutoka Saudi Arabia ili kujiunga na Arsenal kwa mkopo kutoka Chelsea. (Mirror)

Beki wa Newcastle mwenye umri wa miaka 33 Kieran Trippier, ambaye alistaafu kutoka Uingereza wiki iliyopita, amekubali mkataba na Eyupspor ya Uturuki. (Sportsdigitale – In Turkish).

Beki wa Chelsea na England Ben Chilwell, 27, amepewa ofa ya kuwa mchezaji wa mkopo wa Fenerbahce inayofunzwa na Jose Mourinho. (Givemesport)

Timu ya Ubelgiji Anderlecht inavutiwa na kiungo wa kati wa Manchester United na Denmark Christian Eriksen, 32. (Het Belang van Limburg – in Dutch)

Kiungo wa kati wa Manchester City Mjerumani Ilkay Gundogan, 33, ana chaguo la kuongeza mkataba wake wa mwaka mmoja hadi msimu mwingine iwapo atajumuishwa katika zaidi ya asilimia 50 ya mechi za City za msimu wa 2024-25. (Star)

Mshambulizi wa Napoli, Victor Osimhen, ambaye alilengwa na Chelsea katika dirisha la majira ya kiangazi, ameachwa nje ya orodha ya kikosi cha timu yake kwa msimu wa Serie A. (La Gazzetta dello Sport – In Italian).

Liverpool wanataka kumsajili kiungo mkabaji mwezi Januari baada ya kushindwa kumsajili katika dirisha la usajili la majira ya kiangazi. (Football Insider)

Nottingham Forest ilikataa ofa yenye thamani ya pauni milioni 50 kutoka kwa Newcastle kwa ajili ya winga wa Uswidi Anthony Elanga, 22, siku ya mwisho ya dirisha la uhamisho. (Sky Sports}.

Beki wa kati wa Arsenal Mholanzi Omar Rekik, 22, ambaye hajawahi kuichezea klabu hiyo mechi yoyote ya wakubwa, amekatisha mkataba wake. (Fabrizio Romano)

imetafsiriwa na Seif Abdalla