Silvio Berlusconi ajigamba kuhusu uhusiano wake wa karibu na Vladimir Putin

G

Chanzo cha picha, Getty Images

Iliyochapishwa

Silvio Berlusconi, ambaye atakuwa sehemu ya serikali mpya ya muungano ya Italia, amezua mjadala mkubwa baada ya kujigamba kuwa ameanzisha upya uhusiano na Vladimir Putin kupitia mawasilaino ya "barua za upendo "ambapo kiongozi wa Urusi amekuwa akimuita "namba moja miongoni mwa marafiki zake watano bora".

Belusconi ambaye amekuwa Waziri Mkuu mara tatu, ambaye sherehe ya ngono ya  "bunga bunga" na ukaribu wake kwa Kremlin havijamfanya kuwa mgeni katika utata   alitoa kauli hizo kwa wabunge wake.

Katika sauti iliyorekodiwa ya mkutano iliyonaswa na shirika la habari la Italia  LaPresse, Bw Berluscon alisema Bw Putin alikuwa amemtumia chupa 20 za pombe aina ya  vodka kwa ajili ya maadhimisho ya siku yake ya kuzaliwa  na "barua nzuri sana ya upendo."

Aliendelea kusema: "Nilijibu kwa chupa za Lambrusco na ujumbe mtamu saw ana alionitumia", akiongeza kuwa alikuwa "ameanzisha  upya mahusiano na Rais Putin, kupita kiasi."

"Mawaziri wa Urusi wamesema mara nyingi kwamba, tuko vitani nao kwasababu tunatoa silaha na ufadhili kwa Ukraine," Bw Berlusconi aliongeza.

"Siwezi binafsi kutoa maoni yangu kwasababu kama yatajulikana kwa vyombo vya habari, yatageuka kuwa maafa."

Chama cha Berlusconi -Forza Italia, kilitaka kutoa ufafanuzi kuhusu kauli hizo tata kwa kusema kwamba kiongozi wake alikuwa akizungumzia kuhusu mawasiliano ya awali na Kremlin  na kusisitiza kuwa msimamo wake juu ya Urusi uko ‘’ sawa na wa Ulaya na Marekani."

Lakini tukio hilo bado ni mtihani kwa Giorgia Meloni, ambaye anajianda kuitangaza serikali yake ya mrengo wa kulia, ambayo itajumuisha maafisa wa chama cha Berlusconi Forza Italia.  

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Baada ya kushinda uchaguzi mwezi uliopita na chama chake cha mrengo wa kulia, mitizamo ya kijamii ya kihafidhin, Bi Meloni ametaka kuwahakikishia washirika wa Italia wa Magharibi kurudia msimamo wake wa kuunga mkono Nato na aliendelea kutoa silaha kwa Ukraine.  

Lakini yuko katika muungano na Silvio Berlusconi na Matteo Salvini – wote wakifahamika kwa kumhusudu Putin.

Mwaka 2015, Ukraine ilimuwekea marufuku  Berlusconi kwa miaka mitatu kwa kufanya ziara Crimea, eneo  ambalo Putin alilitwaa kinyume cha sheria na kulifanya shemu ya Urusi.  

Mwanasiasa huyo mkongwe wa Italia wakati mmoja alimpatia  Putin zawadi ya shuka(duvet) ya kutandika kitandani yenye picha ya nyuso zao. Wakati wa kampeni za uchaguzi, alisema Putin alitaka tu kumbadilisha rais wa Ukraine   Volodymr Zelensky na "watu wenye heshima."

Kauli mpya za Bw Berlusconi zimekuja baada ya msururu wa malumbano na Bi Meloni. Huku kukiwa na ripoti kuwa alikuwa anapinga uteuzi wa mawaziri wake, alikataa kuunga mkono chaguo la spika la Bi Meloni.

Picha ilijitokeza ya waraka aliokuwa ameandika akimuita  "mtu anayetaka kusikilizwa kwa maoni yake pekee, asiyevumilika , kiburi na mwenye matusi ". Alimjibu: "Berlusconi alisahau kitu kimoja : Mimi sio mtu wa kulaghaiwa."

Hali ya wasi wasi imeongezeka huku mwanasiasa huyo mkongwe akisistiza kuwa mbunge wake ateuliwe kuwa waziri wa sheria, licha ya kushindwa kufikia makubaliano na Bi Meloni.

"Berlusconi  ni kama nge na chura: Anauma hata kama anajua kama atakufa," alisema, ulingana na gazeti la Corriere della Sera.

Mchezo wa mamlaka baina ya wawili hao unaonyesha jinsi Bi  Meloni alivyoweza kukabiliana na Bw Berlusconi mwenye umri wa miaka 86, ambapo ameendelea kupanda kisiasa  kwa kukitwaa chama cha mrengo wa kulia ambacho wakati mmoja alikitawala. 

Katika serikali yake yam waka 2008,  alifanya utezi wa Waziri wake mdogo zaidi kuwahi kuhudumu nchini Italia akiwa na umri wa miaka  31.

Baada ya kulazimishwa kuondoka mamlakani  miaka mitatu baadaye, mamlaka yake yaliisha kutokana na matatizo yake na mahakamani.

Wakati sasa Bi Meloni yuko tayari kuwa Waziri Mkuu akiwa na umri wa miaka 45, kushindi wa kizazi chake unaonekana kukamilika. Lakini uhasama unaoendelea baina ya wawili hao unafichua  makabiliano ambayo bado hayajaisha. 

Wapinzani wao wanaonekana kufurahia uhasama huo. Mwanasiasa wam rengo wa kati Carlo Calenda aliandika kwamba kitu kingine pekee ambacho Berlusconi anaweza kukifanya ni kuzuia kuzaliwa kwa serikali ambayo inaweza kupiga bomu makao makuu ya chama cha bi Meloni.  

Lakini  maigizo haya ya kisiasa sio mazuri. Kwani wakati Muungano wa Ulaya ulikuwa umepunguza wasi wasi kuhusu kiongozi wa kwanza wa mrengo wa kulia zaidi wa Italia tangu Vita vya pili vya dunia, sasa utakuwa na wasi wasi mkubwa kuhusu mwelekeo wa sera ya kigeni wa nchi hiyo.

Na  Kwa Wataliano waliochoshwa na ripoti za karibu kila siku za malumbano baina ya viongozi wa juu wa chama cha mrengo wa kulia zaidi bado wako mbali kupata udhabiti ambao wamekuwa wakiutamani kwa muda mrefu.