Tetesi za soka Ulaya Ijumaa: Liverpool wahamia kwa Osimhen

Chanzo cha picha, Getty Images
Liverpool wanapanga kumsajili Victor Osimhen, 26, ambaye msimu uliopita alicheza kwa mkopo Galatasaray (Givemesport)
Bayer Leverkusen wameweka kipao mbele kwa beki wa kati wa Liverpool, Jarell Quansah, 22, ambaye anakadiriwa kuwa na thamani ya 40m (Athletic)
PSG hawatamruhusu mshambuliaji wa Ufaransa Bradley Barcola, 22, kuondoka msimu huu licha ya kusakwa na vilabu vya Liverpool na Bayern Munich (Foot Mercato)
Manchester United wanavutiwa na mshambuliaji wa Kifaransa Hugo Ekitike, 22, wa Eintracht Frankfurt, anayekadiriwa kuwa na thamani ya takriban £85m (Sky Sports)
Arsenal wanatafakari kumsajili winga wa Athletic Bilbao na Hispania Nico Williams, 22 (Sun)
Hata hivyo, Bayern Munich wamekubaliwa kumsajili Williams baada ya kuwa tayari kulipa kiwango kikubwa cha pesa kwa mujibu wa mkataba wake (Sky Germany)

Chanzo cha picha, Getty Images
Arsenal pia wameulizia kuhusu beki wa kati wa Ajax na Uholanzi Jorrel Hato, 19 (Mail)
AC Milan wanavutiwa na beki wa Arsenal, Oleksandr Zinchenko, 28, ambaye ni raia wa Ukraine (Sky Sports)
Luka Modric, 39, atachelewesha uhamisho wake kwenda AC Milan ili acheze Kombe la Dunia la Klabu akiwa na Real Madrid (Gazzetta dello Sport)
Leeds United, waliopanda Ligi Kuu, wako kwenye mazungumzo na Udinese kuhusu beki wa Slovenia Jaka Bijol, 26 (Sky Sports)
Real Betis wamewasilisha mkataba wa miaka mitatu kwa beki wa pembeni Junior Firpo, 28, baada ya kuachwa huru na Leeds (Fabrizio Romano)

Chanzo cha picha, Getty Images
Brentford wamepanga kuzuia juhudi za kocha mpya wa Tottenham, Thomas Frank, kumvuta kiungo Christian Norgaard, 31, kutoka klabu yao ya zamani (Givemesport)
West Ham na Brentford wanavutiwa na mshambuliaji wa Rangers na Morocco Hamza Igamane, 22, ambaye alifunga mabao 16 kwenye Ligi ya Scotland msimu uliopita (Foot Mercato)
Klabu nne za Premier League ziko tayari kulipa kifungu cha £1.2m kumnasa beki wa Millwall, Japhet Tanganga, 26 (Sky Sports)
Kocha wa zamani wa Luton, Rob Edwards, ndiye mgombea kinara kuchukua mikoba ya Middlesbrough (Sky Sports)















