Ulimwengu ulivyoukaribisha mwaka mpya 2023 katika picha

Iliyochapishwa

Sherehe za mwaka mpya zinaendelea kikamilifu katika sehemu nyingi za dunia ambapo 2023 tayari imewadia.

Taifa la Pasifiki la Kiribati lilikuwa la kwanza kuukaribisha mwaka mpya, likifuatiwa na New Zealand saa moja baadaye - na maelfu walikusanyika Sydney kwa maonyesho maarufu ya fataki katika jiji hilo la Australia.

Baadaye, mwaka mpya ulipoingia magharibi kote Ulaya na Afrika, miji mingi ilikaribisha 2023 kwa umati mkubwa, fataki, matamasha na karamu.

Lakini bado kuna mengi yajayo, huku Amerika ya Kaskazini na Kusini ikipangwa kuashiria kuanza kwa mwaka mpya.