Ulimwengu ulivyoukaribisha mwaka mpya 2023 katika picha

Huko Bangkok, Thailand, fataki zinalipuka kwenye hekalu la Wat Arun Buddhist

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Huko Bangkok, Thailand, fataki zililipuka kwenye hekalu la Wabudha la Wat Arun.
Iliyochapishwa

Sherehe za mwaka mpya zinaendelea kikamilifu katika sehemu nyingi za dunia ambapo 2023 tayari imewadia.

Taifa la Pasifiki la Kiribati lilikuwa la kwanza kuukaribisha mwaka mpya, likifuatiwa na New Zealand saa moja baadaye - na maelfu walikusanyika Sydney kwa maonyesho maarufu ya fataki katika jiji hilo la Australia.

Baadaye, mwaka mpya ulipoingia magharibi kote Ulaya na Afrika, miji mingi ilikaribisha 2023 kwa umati mkubwa, fataki, matamasha na karamu.

Lakini bado kuna mengi yajayo, huku Amerika ya Kaskazini na Kusini ikipangwa kuashiria kuanza kwa mwaka mpya.

Mwanamume na mtoto wanasherehekea pamoja huko Kuala Lumpur, Malaysia

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Mwanamume na mtoto wanasherehekea pamoja huko Kuala Lumpur, Malaysia
China

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Wakazi wa Wuhan, China, walipeperusha puto na kukusanyika kwa sherehe huku kukiwa na ongezeko la maambukizi ya Covid-19 nchini.
Sydney Australia

Chanzo cha picha, BIANCA DE MARCHI/EPA-EFE/REX/SHUTTERSTOCK

Maelezo ya picha, Fataki za Sydney zilizinduliwa kutoka kwa Daraja lake la Bandari, Jumba la Opera na mashua katika bandari yake maarufu
Watu walikuwa wamekusanyika mapema ili kupata mahali pazuri

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Watu walikuwa wamekusanyika mapema ili kupata mahali pazuri
London

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Maonyesho ya fataki ya London - yaliyotazamwa na umati wa watu 100,000 - yaliandana na heshima kwa marehemu Malkia Elizabeth katika ndege zisizo na rubani.
England

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Mvua haikuwazuia watu huko Edinburgh maelfu ya watu kukusanyika katika bustani ya Princes Street kwa sherehe za kwanza za Hogmanay katika miaka mitatu.
Huko Paris, onyesho la fataki lilifanywa kwenye Arc de Triomphe huku wakikusanyika kwenye Champs-Elysees.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Huko Paris, onyesho la fataki lilifanywa kwenye Arc de Triomphe huku wakikusanyika kwenye Champs-Elysees.
Urusi

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Huko Urusi, watu walikusanyika katikati mwa mji wa Moscow. Mamlaka ilifunga Red Square eneo maarufu ya jiji hilo, kutekeleza vikwazo vya Covid huku ikiongeza uwepo wa polisi katika eneo hilo
Katika mji mkuu wa Ukraine wa Kyiv, familia inakusanyika karibu na mti wa Krismasi kusherehekea mwaka mpya kabla ya amri ya kutotoka nje, huku kukiwa na mashambulizi ya Urusi nchini humo.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Katika mji mkuu wa Ukraine wa Kyiv, familia zilikusanyika karibu na mti wa Krismasi kusherehekea mwaka mpya kabla ya muda wa amri ya kutotoka nje kufika, huku kukiwa na mashambulizi ya Urusi nchini humo.
Wenyeji wa Mathare, mojawapo ya makazi maskini zaidi nchini Kenya, wafanya misa ya kuukaribisha mwaka mpya jijini Nairobi, Kenya.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wenyeji wa Mathare, mojawapo ya makazi maskini zaidi nchini Kenya, wafanya misa ya kuukaribisha mwaka mpya jijini Nairobi, Kenya.
 Mwanamke anakula zabibu huko Madrid, utamaduni wa mwaka mpya nchini Uhispania

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mwanamke anakula zabibu huko Madrid, utamaduni wa mwaka mpya nchini Uhispania