Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 13.03.2024

Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester United wanataka £43m kumuuza mshambuliaji wa Uingereza Mason Greenwood, 22, ambaye yuko Getafe nchini Uhispania kwa mkopo. Klabu ya Saudi Arabia ambayo haikutajwa jina imeonyesha nia ya kutaka kumsajili Greenwood. (Mirror)
Winga wa Arsenal Mwingereza Reiss Nelson mwenye umri wa miaka 24 anawaniwa na Brighton msimu wa joto. (Teamtalk)

Chanzo cha picha, Getty Images
Arsenal wamemfanya mshambuliaji wa Sporting Lisbon na Uswidi Viktor Gyokeres, 25, kuwa shabaha yao kuu msimu huu. Mchezaji huyo wa zamani wa Coventry ana kipengele cha kutolewa cha £85m katika mkataba wake. (Football Transfers)
Liverpool wameiambia Barcelona kuwa winga wa timu ya taifa ya Colombia Luis Diaz, 27, ni sehemu ya mipango ya muda mrefu ya klabu hiyo na hatauzwa msimu huu wa joto. (Mirror)
Klabu za Arsenal na Liverpool zinavutiwa na beki wa Ecuador na Eintracht Frankfurt Willian Pacho, 22. (90min).

Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester United wanataka £43m kumuuza mshambuliaji wa Uingereza Mason Greenwood, 22, ambaye yuko Getafe nchini Uhispania kwa mkopo. Klabu ya Saudi Arabia ambayo haikutajwa jina imeonyesha nia ya kutaka kumsajili Greenwood. (Mirror)
Manchester United inajaribu kumrejesha Uingereza kiungo wa zamani wa Newcastle United Mikel Merino, 27. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uhispania anachezea Real Sociedad. (COPE - kwa Kihispania)
Licha ya kutakiwa na Juventus na AC Milan, ni Aston Villa ambao wako katika nafasi nzuri ya kumsajili beki wa Atletico Madrid Mario Hermoso, 28, kwa uhamisho wa bila malipo msimu huu. (calciomercato.com)

Chanzo cha picha, Getty Images
Chelsea huenda wakawauza wachezaji nyota kadhaa msimu huu, akiwemo mshambuliaji wa Uingereza Raheem Sterling, 29. (Mail).
West Ham inamfuatilia kiungo mshambuliaji wa Sporting Lisbon na Ureno Pedro Goncalves, 25. Kandarasi yake na Sporting inaendelea hadi Juni 2027 lakini ana kipengele cha kuachiliwa kwa pauni milioni 68. (Record- kwa Kireno)
Manchester City wako kwenye mazungumzo ya kuongeza kandarasi ya mlinda mlango wa Ujerumani Stefan Ortega mwenye umri wa miaka 31 katika klabu hiyo. (Florian Plettenberg)
Mlinzi wa Manchester City na England Kyle Walker, 33, anasema angependa kuhamia Saudi Arabia, ingawa hayuko tayari kuondoka katika Ligi ya Premia. (FIVE)

Chanzo cha picha, Getty Images
Maurizio Sarri, mkufunzi wa zamani wa Chelsea, amejiuzulu kama meneja wa Lazio baada ya kipigo cha Jumatatu cha 2-1 kutoka kwa Udinese nyumbani na kuiacha timu yake pointi saba kutoka kwa Atalanta, ambao wanasalia katika nafasi ya Ligi ya Europa ya Italia. (Soka Italia)
Fulham na Nottingham Forest wanavutiwa na kiungo mshambuliaji wa Bologna na Scotland Lewis Ferguson, 24, ambaye amefunga mabao sita ya Serie A msimu huu. (calciomercato.com - kwa Kiitaliano)
Kiungo wa kati wa Brighton wa Scotland Marc Leonard, 22, anasakwa na Preston, Plymouth na Swansea. (Fabrizio Romano)
Imetafsiriwa na Ambia Hirsi












