Ni lini nchi ya Afrika itashinda Kombe la Dunia?

Chanzo cha picha, BBC Sport
- Author, Rob Stevens & Ian Williams
- Nafasi, BBC
- Iliyochapishwa
- Muda wa kusoma: Dakika 5
"Kama kuna kitu nataka kukiona kabla Mungu hajanipeleka peponi au motoni, ni kuona taifa la Afrika likishinda [Kombe la Dunia], kwa sababu haya ni mashindano ambayo sote tunayapenda sana barani Afrika."
Sunday Oliseh alikuwa sehemu ya timu ya kwanza ya Afrika kushinda medali ya dhahabu ya mpira wa miguu katika Olimpiki, akiisaidia Nigeria kuweka historia katika Michezo ya Atlanta ya 1996, lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 51 bado anasubiri kuona mafanikio katika Kombe la Dunia la Fifa.
Kombe la Dunia limefanyika mara 22 tangu 1930, na kufikia sasa Afrika imewakilishwa na timu mara 49, zikitoka katika nchi 13, lakini Afrika imefikia nusu fainali mara moja tu.
Ni miaka minne iliyopita huko Qatar 2022, wakati Morocco ilipoweka historia hiyo kwa bara hili la pili kwa ukubwa na la pili kwa idadi ya watu duniani.
Utabiri uliofanywa na mshindi mara tatu wa Kombe la Dunia, raia wa Brazil, Pele, ambaye alisema katika miaka ya 1970 kwamba taifa la Afrika litashinda ifikapo mwaka 2000, bado haujatimia.
Juhudi za Afrika
Afrika ina timu tatu zilizofika robo fainali - Cameroon mwaka 1990, Senegal mwaka 2002 na Ghana mwaka 2010 - kabla ya Morocco kuifunga Ubelgiji, Uhispania na Ureno katika safari yao ya kuelekea robo fainali nchini Qatar.
Jambo moja linaloleta mafanikio ya Waafrika Kaskazini ni uwekezaji wa muda mrefu unaofanywa na Mfalme Mohammed VI wa nchi hiyo.
Akademia na kituo cha mafunzo vyote vikiwa na jina lake, vilifunguliwa mwaka 2009 na 2019 na vimeisaidia Atlas Lions kujiimarisha kama timu ya nafasi ya kwanza barani Afrika.
Kwa upande wa Shirikisho la Soka la Afrika (Caf) limekuwa likijaribu kuongeza nguvu kupitia mashirikisho ya kitaifa na vilabu kwa kuongeza pesa za zawadi kwa Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) na mashindano makubwa ya vilabu barani, pamoja na kuwekeza katika mashindano ya shule.
"Nchi ya Afrika itakuwa mabingwa wa dunia," rais wa Caf Patrice Motsepe alitabiri.
"Hilo ndilo tunalofanyia kazi, ndilo tunalowekeza na tuna uhakika litatokea."
Claude Le Roy (78), ambaye aliiongoza Cameroon katika Kombe la Dunia la 1998 na amewahi kufundisha mataifa mengine matano ya Afrika, anasema kuwekeza katika vijana kutatoa faida za muda mrefu.
"Huo ndio msingi wa kila kitu," anasema.
Hadithi ya Ukoloni

Chanzo cha picha, Getty Images
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Katika miaka ya nyuma, mataifa ya Afrika yalikosa kushiriki katika Kombe la Dunia kutokana na ukoloni uliokuwa ukizuia fursa hiyo, kabla ya nchi nyingi kutangaza uhuru wake katika miaka ya 1950 na 60.
Misri, mwaka 1934, ilikuwa mshindani pekee kutoka bara hilo katika mashindano manane ya kwanza - na Afrika ilisusia fainali za 1966 baada ya Fifa kutangaza kuwa haitakuwa na mechi ya moja kwa moja ya kufuzu Kombe la Dunia la mwaka huo nchini Uingereza.
Bara hilo lilipeleka timu moja kwenye fainali za 1970, 1974 na 1978 – wakati kulikuwa na angalau timu tisa kutoka Ulaya na tatu kutoka Amerika Kusini.
Nafasi mbili kwa Afrika zilianza kutolewa kuanzia mwaka 1982, tatu mwaka 1994 na tano kuanzia mwaka 1998 na kuendelea wakati mashindano hayo yalipopanuka hadi timu 32.
Sita zilishiriki mwaka 2010 wakati Afrika Kusini ilipoandaa, lakini fainali za mwaka huu zenye timu 48 nchini Canada, Mexico na Marekani zitashuhudia timu nyingi zaidi kuwahi kutokea. Timu tisa zimefuzu moja kwa moja pamoja na DR Congo, ambao walipitia mechi za mchujo za mashirikisho.
Kutumia wachezaji wa diaspora
Afrika kuna mrundikano wa vipaji ambapo wachezaji waliozaliwa Afrika au wenye asili ya Kiafrika wanachagua kuwakilisha mataifa ya Ulaya, lakini bara hilo sasa linatumia fursa ya mataifa makubwa ya kigeni.
Baadhi ya wachezaji hao wamefunzwa katika akademi za vilabu bora vya Ulaya.
Pamoja na uwekezaji wao, Morocco imewashawishi wachezaji kadhaa waliozaliwa nje ya nchi, akiwemo kipa Yassine Bounou (Canada) na Achraf Hakimi na Brahim Diaz (wote Uhispania), kuvaa jezi ya Atlas Lions.
Wakati huo huo, timu ya Cape Verde inayoshiriki kwa mara ya kwanza na DR Congo inayorejea kwenye fainali kwa mara ya kwanza tangu 1974, zote zimefuzu baada ya kutumia wachezaji wengi kutoka nje.
Kati ya kikosi cha wachezaji 26 cha Congo, 11 walizaliwa Ufaransa, watano Ubelgiji, wawili Uswisi na wawili Uingereza. Mabeki Aaron Wan-Bissaka na Axel Tuanzebe wote wameamua kuitumikia Congo baada ya kuiwakilisha Uingereza katika ngazi ya vijana.
Imani inaongezeka

Mafanikio ya Morocco nchini Qatar yamewatia moyo wachezaji wa mpira wa miguu kutoka kote barani kwamba kufikia angalau nusu fainali kunawezekana.
Senegal walishindwa kwenda nusu fainali 2002, kutokana na sheria ambayo sasa imefutwa. Ni sheria ambapo timu itakayo shinda goli wakati wa muda wa nyongeza wa dakika 30, inafuzu na mechi inakuwa imemaliza.
Katika robo fainali mwaka 2010, mshambuliaji wa Ghana Asamoah Gyan aligongesha penalti kwenye mwamba wa Uruguay mwishoni mwa muda wa ziada, huku Morocco wakitolewa kwa mikwaju ya penalti.
Morocco na Senegal, ziko katika nafasi ya nane na ya 14 duniani, zinatoa matumaini zaidi kwa Afrika ya kusonga mbele, mbele ya timu za Ulaya na Amerika Kusini, lakini zote zina makundi magumu.
Ikiwa timu za bara hilo zitashindwa tena, basi Morocco itakuwa na faida ya nyumbani mwaka 2030, wakati ufalme huo utakapoandaa kombe la dunia, kwa kushirikiana na Ureno na Uhispania.















