Wafahamu vijana wadogo watoto 5 walioleta mabadiliko duniani

Chanzo cha picha, Getty Images
- Author, Dinah Gahamanyi
- Nafasi, BBC Swahili
- Iliyochapishwa
Mara nyingi, vijana wadogo walio katika umri wa kubarehe hufikiriwa kama watu ambao huwa hawana upeo wa juu wa kufikiria mambo, na wakati mwingine huonekana kama wavivu. Lakini kwa vijana hawa ni tofauti.
1: Nkosi Johnson

Nkosi Johnson alizaliwa 1989 na kufariki dunia 2001. Nkosi alizaliwa na maambukizi ya HIV/AIDS - aliyoyarithi kutoka kwa wazazi wake. Katika mwaka 1997, alikataliwa kujiunga na shule ya umma kwasababu ya hali yake ya HIV.
Hata hivyo alikuwa mwanakampeni mkuu wa jinsi waathiriwa wa HIV wanavyopaswa kuchukuliwa sawa na watu wengine na kwa heshima katika kipindi ambacho kulikuwa na ubaguzi mkubwa dhidi ya watu wenye maambukizi hao.
Pamoja na mama yake mlezi, alianzisha kituo cha wakimbizi cha akina mama na watoto wao wenye HIV. Alipokea Tuzo ya Amani ya Watoto . Rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela alimuelezea- kama ‘alama ya mapambano kwa ajili ya maisha.’
2: Malala Yousafzai

Chanzo cha picha, AFP
Malala Yousafzai alizaliwa mwaka 1997 nchini Pakistani. Akiwa mshichana wa shule nchini mwake, alipinga vitisho vya kampeni za kundi la Taliban kwa ajili ya kampeni ya elimu kwa wasichana.
Alinusurika kuuawa baada ya kupigwa risasi kichwani na kuwa mtetezi wa haki za binadamu, haki za wanawake, na haki ya elimu.
Amekuwa akisisitizia asili ya amani ya Uislamu na heshima Uislamu ulionayo kwa elimu.
Kutokana na hilo Malala amekuwa alama ya mapambano ya elimu kwa wasichana duniani.
3: Samantha Smith

Chanzo cha picha, Getty Images
Samantha Smith alikuwa mwanafunzi msichana Mmarekani kutoka eneo la Maine. Alizaliwa mwaka 1972 na kufariki 1985. Katika mwaka 1982, salimuandikia barua kiongozi wa Muungano wa Usovieti , Yuri Andropov, akimuuliza ni kwanini uhusiano baina ya Marekani na Muungano wa Usovieti ulikiwa wa wasi wasi.
Barua yake ilichapishwa katika Pravda, na baadaye Andropov alimjibu. Smith pia alialikwa kutembela Muungano wa Usovieti na kwenda.
Ziara yake ilifuatiwa na taarifa nyingi za vyombo vya habari , ambavyo vilimnukuu Smith akisema kuwa alikuta Warusi wako tu kama sisi.
Katika mwaka 1983, aliitembelea Japan, akiwa kama balozi mdogo zaidi wa Marekani. Alifariki akiwa na umri wa miaka 13 pekee, katika ajali ya ndege.
Emma González

Chanzo cha picha, AFP
Mnamo mwezi wa Februari 2018, mtu mwenye silaha alivamia katika shule ya sekondari ya Marjory Stoneman Dauglasiliyopo Parkland, Florida, na kuwauwa watu 17.
Lakini badala ya kuathiriwa na tukio hilo baya, vijana wengi walionusurika na ufyatuaji huo wa risasi walianza kampeni ya kitaifa kujaribu kumaliza ghasia za bunduki.
Emma González, wakati huo akiwa na umri wa miaka18 pekee, alijitokeza kama mmoja wa viongozi wa vuguvugu hili jipya na akawa muasisi mwenza wa kikundi kilichozungumzia kuhusu haja ya udhibiti wa silaha kinachojulikana kama Vever Again MSD .
Mwezi Machi 2018, alitoa hotuba nzito katika maandamano yaliyolenga kuhimiza udhibiti wa silaha nchini Marekani - March for Our Lives mjini Washington, D.C. wakati ambapo alisoma wazi majina ya wanafunzi wenzake waliofariki na kukaa kimya kwa mud awa dakika nne- muda uliotumiwa na mshambuliaji kufanya shambulio.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Jack Andraka

Akiwa na umri wa miaka 15 pekee, mwanafunzi wa shule ya sekondari nchini Marekani Jack Andraka alivumbua kile kinachoonekana kama , njia mpya ya kugundua saratani ya kongosho.
Mvulana huyu, ambaye alishinda $75,000 (£58,000) katika maonyesho ya kisayansi ya mwaka 2012- Intel International Science and Engineering Fair- kwa ubunifu wake , alisema kuwa alipata wazo hilo kwa kusoma magazeti ya Kisayansi aliyoyapata kwenye mtandao.
Kifaa cha ubunifu wake, ambacho bado kinafanyiwa uchunguzi wa kina, kimetengenezwa kwa karatasi ya kichujio iliyofunikwa na kimiminika cha chupa zenye kaboni na protini inayoulinda mwili dhidi ya maambukizi (antibody), kulingana na Wired, na kinahitaji matone sita ya damu ili kupima saratani ya kongosho.















