Rwanda: Bunge lapinga marekebisho ya muswada wa kuzuia mimba kwa wototo

G

Chanzo cha picha, Rwanda parliament/Twitter

Iliyochapishwa

Bunge la Rwanda limepinga muswada wa marekebisho ya sheria ya mwaka 2016  ili kuruhusu matumizi ya dawa za kuzuia mimba kwa watoto wenye umri wa miaka 15.   

Kikundi cha wabunge kilikuwa kimeleta muswada huo bungeni kwa ajili ya kukabiliana na mimba za utotoni ambazo idadi yake imeongezeka nchini humo kwa  23% kutoka zaidi ya  19,000 katika mwaka  2020 hadi mimba 23,000 katika mwaka  2021, walisema maafisa.

Sheria ya sasa inaruhusu wanawake wenye umri wa miaka 18 pekee ndio wanaoruhusiwa kupata huduma za uzazi. Kumekuwa na mjadala miongoni mwa wanaharakati wa afya, wanaharakati wa utamaduni, na viongozi wa kidini kuhusu ukomo huo.   

 Kukataliwa kwa muswada huo ni mwisho wa “mabadiliko yaliyotarajiwa” katika sheria ambayo  ina mianya”, alisema  Aflodis Kagaba mwanaharakati wa afya ya uzazi nchini Rwanda aliiambia BBC. 

“Kwa bahati mbaya, hili limefunika kila kitu ikiwa ni pamoja na fursa ya kufungua tena mazungumzo haya muhimu katika bunge ”, anasema Bw Kagaba , Mkuu wa HDI, shirika ambalo linafanya kampeni kwa ajili ya upatikanaji  wa afya bora nchini Rwanda.

Zaidi ya wabunge 30 ambao walipinga kuidhinishwa kwa muswada huo walitoa sababu za kijamii, kitamaduni na kiimani, vimeripoti vyombo vya habari. Wabunge wanne hawakupiga kura.

 

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

Mwisho wa X ujumbe

Lakini Bw Kagaba anasema sheria ya hivi sasa  ina “mapungufu” na anaamini “bado inahitaji kurekebishwa”.  

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

“Ukiwa na chini ya miaka 18 na unahitaji  huduma za afya ya ngono na uzazi unatakiwa kusindikizwa na wazazi ili watoe idhini! Hiki ni kikwazo kikubwa.” Alisema Bw Kagaba.

 Aliongeza kuwa: “Bado ninaamini kuwa sheria hii inahitaji marekebisho ili kuongeza kipengele kitakachowapa vijana  wenye umri wa kubalehe haki ya afya ya uzazi,  na kuongezewa vipengele ambavyo tayari vimeidhinishwa katika sheriakama vile kuavia mimba kwa njia inayokubalika.” 

Tangu mwaka 2020 nchini Rwanda kumekuwa na mjadala miongoni mwa wataalamu wa afya, wawasikishi wa familia, dini, na mashirika yasiyo ya kiserikali , kuhusu iwapo watoto wenye umri wa miaka 15 wanapaswa kupewa huduma ya afya ya kuzuwia mimba au la.   

 Baadhi wanaonelea kuwa kuongezeka kwa idadi ya wasichana wadogo wanaobeba mimba  kila mwaka ni sababu tosha ya kuidhinishwa kwa kipengele ambacho kilikuwa mojawapo ya vipengele ambavyo wabunge waliviweka katika muswada huu wa marekebisho ya sheria hiyo.

Katika ujumbe wake wa Twitter ,Olivier T. Mhuriro anasema ‘’Kwa upande mwingine kuwanyima watoto wenye umri wa miaka 15 uwezo wa kupata dawa za kuzuia mimba inamaanisha kuwa wasichana wadogo wenye chini ya miaka 16 wataendelea kupata ujauzito na idadi ya mimba za wasichana wenye umri wa kubalehezitaongezeka’’

Olivier T.Mhuriro/Twitter

Chanzo cha picha, Olivier T.Mhuriro/Twitter

Wanaopinga mbinu hii ya kupanga uzazi kwa watoto wanasema kuwa haiendani na utamaduni wa Wanayarwanda na kwamba itawachochea watoto kushiriki ngono.

 @ishimweWilly anasema: ‘’kama wanandoa watu wazima hawawezi kupanga wenyewe uzazi kwa kutumia dawa za kuzuia ujauzito; na unaamini wabunge watazuia mimba za utotoni. Tafadhali, hauana suluhu kwa suala hili!’’

G

Chanzo cha picha, @IshimweWilly

Kagaba anasema: “Inasikitisha kwamba mushwada huu haujaidhibishwa kwani hii imeondoa fursa ya kufanyika kwa mazungumzo tena muhumu kuhusu vipengene hivi katika Bunge la taifa