Tetesi za Soka Ulaya Jumanne: Man City inamfuatilia El Mala Cologne

 Said El Mala,

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Winga wa klabu ya Cologne ya Ujerumani Said El Mala,
Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 3

Meneja wa Manchester City Pep Guardiola anavutiwa na winga wa klabu ya Cologne ya Ujerumani Said El Mala, 19, na amewaomba wasaka vipaji wa City kumfuatilia kwa makini. (Sky Sports Germany - kwa Kijerumani)

Nottingham Forest haina mpango wa kumuuza kiungo wa England Elliot Anderson,23, wakati wa usajili wa wachezaji Januari mwakani. Mchezaji huyo ambaye thamani yake inakadiriwa kuwa zaidi ya pauni milioni 100m anawaniwa na Manchester United na klabu yake ya zamani Newcastle. (Telegraph - usajili unahitajika)

Kiungo wa kati wa Wolves Joao Gomes yuko tayari kujiunga na Manchester United kwa ada ya £44m ya kutosha kumzawadia Mbrazil huyo mwenye umri wa miaka 24 mbali na Molineux mwezi Januari. (Record - kwa Kireno)

Manchester United haitaimarisha safu yake ya kati hadi msimu ujao wa joto watakapoweka kapuni nia ya kumsajili mchezaji wa kimataifa wa Cameroon Carlos Baleba na mchezaji wa kimataifa wa England wa Crystal Palace Adam Wharton, wote 21, pamoja na mchezaji wa kimataifa wa Ujerumani wa Stuttgart Angelo Stiller, 24. (ESPN)

Matumaini ya Liverpool kumsajili Antoine Semenyo, 25, kutoka Bournemouth katika uhamisho la Januari yametibuka kbaada ya Cherries kumkatalia winga huyo wa Ghana. (Team talk)

Mshambulizi wa Ujerumani Niclas Fullkrug, 32, anatarajiwa kuondoka West Ham mwezi Januari. Mchezaji huyo amefanya mazungumzo na vilabu kadhaa vya Bundesliga. (Fabrizio Romano)

Mshambulizi wa zamani wa Brentford Ivan Toney anatarajiwa kusalia katika klabu ya Saudi Pro League Al-Ahli licha ya vilabu vya Tottenham, Everton na West Ham kuonyesha nia ya kutaka kumsajili Muingereza huyo mwenye umri wa miaka 29 . (Football Insider)

Kiungo wa kati wa Atletico Madrid na timu ya taifa ya England Conor Gallagher ahana nia ya kukihama klabu hicho cha La Liga, Anasema "anafurajia sana" kukipiga mji mkuu wa Uhispania licha yakuhusishwa na kuhamisho wa Manchester United. (AS - kwa Kihispania)

Arsenal, Chelsea na Real Madrid wanajiandaa kumenyana katika kinyan'ganyiro cha kumsajili mshambuliaji wa Juventus Kenan Yildiz baada ya mazungumzo ya kandarasi kati ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Uturuki mwenye umri wa miaka 20 na klabu hiyo ya Turin kugonga mwamba. (Caughtoffside)