Kuku wanaokuzwa maabara ni mlo salama, wasema wadhibiti wa viwango Marekani

Chanzo cha picha, Getty Images
Nyama inayokuzwa katika maabara imeidhinishwa kuliwa na binadamu kwa mara ya kwanza.
Shirika la usalama wa chakula na dawa nchini Marekani (FDA), limetoa idhini ya kuliwa kwa kuku ambao seli zao zinakuzwa ndani ya maabara, baada ya kufanya ‘’tathmini ya uangalifu’.’
Kuku hawa wanatengenezwa katika matanki ya chum ana kampuni ya Upside Foods, kwa kutumia seli zilizovunwa kutoka kwa Wanyama hai.
Wataweza kuuzwa kwa walaji baada ya ukaguzi wa Wizara ya kilimo ya Marekani.
FDA ilisema ilitumia data na taarifa zilizotolewa na kamouni kufikia uamuazi wake, kwamba ’’haikuwa na maswali zaidi wakati huu’’.
Mwanzislishi wa kampuni na mkurugenzi mtendaji Uma Valeti alisema: "tulianzisha kampuni ya Upside katika wakati ambapo dunia ilikuwa imejaa watu wenye mashaka na hili, na sasa, tumeweka historia tena kama kampuni ya kwanza kupokea 'Barua ya kutokuwa na maswali' kutoka kwa FDA kwa kuvuna nyama."
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Upside Foods itakuwa na vikwazo kadhaa kabla ya kuwezeshwa kuuza bidhaa zake – kwa mfano, mahali ambapo bidhaa zimetengenezwa patatakiwa kuidhinishwa rasmi – lakini Bw Valeti amesema taarifa hiyo ni sawa na ‘’mkondo wa maji yanayoingia kisimani katika historia ya chakula ".
Hamu ya uvumbuzi
Kampuni kadhaa za chakula zinazoanza shughuli zake zimekuwa zikijaribu kutengeneza bidhaa zinazofanana, jambo linaloweza kusababisha kupungua kwa utoaji mkubwa wa hewa chafu ya kaboni na kupunguza matumizi ya maji , pamoja na ardhi kwa ajili ya siku sijazo.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Wanasayansi wanasema shinikizo kwa sayari dunia linaweza kushuka kwa zaidi ya asilimia 80, iwapo vyakula kama hivyo vitatumika, ikilinganishwa na mlo wa kawaida wa Ulaya.
Nyama inayokuzwa kwenye maabara inatarajiwa kuchukua na2fasi kubwa katika soko la jula la nyama katika siku zijazo.
The start-up Eat Just, kampuni ambayo ni mshindani wa Upside Foods, ilikuwa ya kwanza kupokea idhini ya kutengeneza nyama bandia ‘‘nyama safi’’ , nchini sinagapole mwaka 2020. Nyama zake zilitengenezwa kutokana na seli za myama katika maabara.
Makampuni mawili katia ya makampuni makubwa katika sekta hiyo ya ukuzaji wa nyama za maabara ni kampuni yenye makao yake Israel-Future Meat Technologies na Impossible Foods, ambapo mikate yake ya Burger inayofahamika kama Impossible Burger ilizinduliwa mwaka 2016 na umaarufu wake umeongezea.
Matokeo yake, kampuni ilianzisha ushirikiano na kampuni ya Burger King na sasa Impossible Whoppers inauzwa katika migahawa mingi nchini Marekani .
Idhini iliyopewa The Upside Foods na FDA aimeelezewa kama "hatua kubwa " katika sekta na Ernst van Orsouw, Mkurugenzi mkuu mtendaji wa Roslin Technologies – kampuni ya teknolojia ya chakula ya Uskochi.
‘’Inafurahisha sana kuona mdhibiti wa viwango kote duniani sasa anaafiki kwamba nyama iliyovunwa ni salama kuliwa," alisema." FDA imekuwa ikifuata misingi ya hatari, sayansi na mbinu ya kivitendo kudhibiti chakula hiki, ambacho kinaweza kuwa mwongozo bora kwa maeneo mengine pia ."
Alisema hatu hii "itachochea uwekezaji zaidi na uvumbuzi " katika sekta ya vyakua vya kukuzwa kwenye maabara.















