Berlin kuruhusu wanawake kuogelea kifua wazi

Iliyochapishwa

Wanawake hivi karibuni wataruhusiwa kuogelea kifua wazi katika mabwawa ya umma ya kuogelea mjini Berlin, kufuatia ya uamuzi wa mamlaka ya jiji hilo.

Haya yanajiri baada ya mwanamke aliyekuwa akiogelea kifua wazi kwa ajili ya kuchomwa na jua kuchukua hatua za kisheria.

Mwanamke wa pili aliambiwa ajifunike akiwa katika kidimbwi kimoja cha kuogelea mnamo mwezi Desemba.

Mamlaka zilikubali kuwa walikuwa waathiriwa wa ubaguzi na ikasema kwamba wageni wote waliotembelea mabwawa ya Berlin sasa walikuwa na haki ya kuogelea bila vazi la kufunika kifua

Uamuzi huo utaungwa mkono na wale ambao wanatetea kile kinachojulikana kama Freikörperkultur - utamaduni wa uhuru wa mwili.

Wageni wanaotembelea Ujerumani mara nyingi hushangazwa - na wakati mwingine hufadhaika kabisa - kwa kuona Wajerumani wakiwa utupu wakicheza katika maziwa yake, wakikoroma kwenye bustani zao, au kutokwa na jasho kwenye sauna zao.

Lakini hii ni nchi ambayo inachukulia utupu katika maeneo ya umma kuwa unafaa na ni suala la kiafya.

Lakini Suali la iwapo, na kwa kiwango gani, wazo hilo linaruhusiwa katika mabwawa ya kuogelea ya manispaa limesababisha mjadala mkubwa mitaani.

Majira ya joto yaliyopita, Göttingen huko Lower Saxony na Siegen huko North Rhine Westphalia waliwaruhusu wanawake kuogelea kufunika sehemu zao za juu za mwili.

Msimamizi wa bwawa la kuogelea la Berlin, Berliner Bäderbetriebe (BBB), kwa kweli hajabadilisha sheria zake, ambazo zinasisitiza kuwa vazi la kuogelea ni sharti lifunike sehemu za siri.

BBB ilifafanua tu kwamba hii inatumika kwa kila mgeni, bila kujali jinsia yao.