Tetesi za soka Ulaya Jumanne 05.12.2023

 David de Gea

Chanzo cha picha, Getty Images

Iliyochapishwa

Mlinda lango wa zamani wa Manchester United na Hispania, David de Gea (33) yuko tayari kujiunga na Newcastle United ili kuziba pengo la mlinda lango wao aliyeumia Nick Pope (31) kwa mujibu wa gazeti la Telegraph.

Mlinda lango wa Arsenal, Aaron Ramsdale pia anafikiriwa kuhamia Newcastle United, lakin klabu hiyo inasita kutoa kitita kinachotakiwa na Arsenal cha pauni za Uingereza milioni 50 kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25, imeripoti redio ya Talksport.

Newcastle na Manchester United wanawania kumnunua mshambuliaji wa Guinea, Serhou Guirassy, ​​27, kutoka Stuttgart mwezi Januari. (Football Insider)

Serhou Guirassy,

Chanzo cha picha, Getty Images

Arsenal wako tayari kusikiliza ofa kwa mshambuliaji wa Uingereza Eddie Nketiah, 24, mwezi Januari. (Football Transfers)

Beki wa zamani wa Ufaransa, Raphael Varane (30), ameelezea nia ya kusalia Manchester United baada ya dirisha la usajili la Januari. (Manchester Evening News).

Manchester United , Arsenal na Chelsea wanamfuatilia mlinda mlango wa Ufaransa Mike Maignan (28), huku akikwama kusaini mkataba mpya na AC Milan. (Footmercato).

Bayern Munich wanakabiliwa na kibarua cha kumbakisha mshambuliaji Mfaransa, Mathys Tel, 18, huku vilabu kadhaa vya Ligi Kuu ya Uingereza vikimtaka kwa mujibu wa gazeti la Bild.

Mathys Tel

Chanzo cha picha, Getty Images

Jean-Philippe Mateta anatafuta kuondoka Crystal Palace mwezi Januari na Eintracht Frankfurt inaweza kumpa mshambuliaji huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 26 ruhusa ya kuondoka. (The Athletic).

Newcastle wanatazamiwa kumsajili kiungo wa kati wa Manchester City na timu ya taifa ya Uingereza, Kalvin Phillips (28), mwezi Januari. (Rudy Galetti).

Kalvin Phillips

Chanzo cha picha, Getty Images

Juventus pia wanamtaka kiungo wa kati wa zamani wa Leeds, Phillips na wanaweza kujaribu kumsajili kwa mkopo mwezi Januari. (Metro).

Chelsea na Manchester City zinaonesha nia ya kumnunua kiungo wa kati wa River Plate, Claudio Echeverri (17), mshambuliaji Agustin Ruberto, (16) na winga Ian Subiabre, ambao walionyesha uwezo mkubwa huko Argentina kwenye Kombe la Dunia la chini ya umri wa 17 hivi karibuni. (90Min).

West Ham, Burnley na Sheffield United wanatazamiwa kusaka saini ya beki wa Derby, Muingereza, Eiran Cashin mwenye umri wa miaka 22. (TeamTalk).

Everton wana nia ya kumsajili beki wa Lyon mwenye umri wa miaka 22 kutoka Ireland, Jake O'Brien mwezi Januari. (Footmercato).

Imetafsriwa na Rashid Abdallah na kuhaririwa na Florian Kaijage