Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 13.02.2024

Chanzo cha picha, BBC Sport
Kiungo wa kati wa Manchester City na Ureno Bernardo Silva, 29, anawaniwa na Paris St-Germain, huku mabingwa hao wa Ufaransa wakiwa tayari kulipa dau lake la pauni milioni 51. (Fichajes - kwa Kihispania)
Mshambulizi wa Paris St-Germain Kylian Mbappe, 25, na klabu yake hawajashawishika na ofa ya hivi punde zaidi ya Real Madrid kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa, ambaye anaweza kuhama msimu huu wa joto, kwa kuwa ni chini ya pendekezo la awali la Mei 2022. (Athletic - usajili unahitajika)
Tottenham wana imani kuwa kocha Ange Postecoglou, 58, atasalia katika klabu hiyo licha ya Liverpool kumtaka huku Reds wakitafuta atakayechukua mikoba ya Jurgen Klopp msimu huu wa joto. (Telegraph - usajili unahitajika)

Chanzo cha picha, Getty Images
West Ham wamechelewesha mazungumzo ya kandarasi na meneja David Moyes, 60, huku klabu hiyo ikilenga kumaliza mfululizo wa mechi saba bila kushinda katika michuano yote. (Mail)
Manchester United wanavutiwa na mlinzi wa Bayern Munich Matthijs de Ligt, 24, ingawa mchezaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi hajafurahishwa na nafasi yake katika kikosi cha mabingwa hao wa Ujerumani. (Sun)
Arsenal pia wana nia ya kumnunua De Ligt lakini Manchester United kwa sasa wako katika nafasi nzuri. (Football Transfers)
Mabeki wawili wa Bayer Leverkusen pia wanafuatiliwa na Manchester United, huku mkufunzi wa Red Devils Erik ten Hag akimtaka beki wa kulia wa Uholanzi Jeremie Frimpong, 23, na mlinzi wa kati wa Burkino Faso Edmond Tapsoba, 25. (Manchester Evening News).
Ten Hag pia ameomba kusajiliwa kwa mshambuliaji wa Inter Milan na Argentina Lautaro Martinez, 26. (Fichajes - kwa Kihispania)

Chanzo cha picha, RONALD WITTEK
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Klabu za Arsenal na Liverpool zina nia ya kumsajili winga wa Ureno Pedro Neto kutoka Wolves, ambao wako tayari kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 ikiwa thamani yao itafikiwa kwa sababu ya shinikizo la kifedha linaloendelea. (Fichajes - kwa Kihispania)
Chelsea inamfuatilia beki wa kushoto wa Bournemouth na Hungary Milos Kerkez, 20, pamoja na beki wa pembeni wa Bayern Munich na Canada Alphonso Davies, 23. (Football Transfers)
Fulham walishindwa katika jaribio la kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund Sebastien Haller mwezi Januari huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 akitaka kuelekeza nguvu zake kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika akiwa na Ivory Coast na hakutaka kuhama katikati ya msimu. (Fabrizio Romano)
Barcelona imewaweka beki wa Denmark Andreas Christensen, 27, na winga wa Brazil Raphinha, 27, katika oodha ya wachezaji wanaopangwa kuuzwa ili kupunguza bili yao ya mishahara. (Mirror)
Mkufunzi wa Bayern Leverkusen Xabi Alonso sasa anasakwa na Barcelona pamoja na Real Madrid na Liverpool. (Sport - kwa Kihispania)

Chanzo cha picha, Getty Images
Paris St-Germain imemjumuisha winga wa AC Milan na Ureno Rafael Leao, 24, na mshambuliaji wa Napoli na Nigeria Victor Osimhen, 25, kwenye orodha yao inayotarajiwa iwapo Mbappe ataondoka katika klabu hiyo msimu huu wa joto. (La Repubblica - kwa Kiitaliano)
Mshambulizi wa Porto na Iran Mehdi Taremi, 31, anatazamiwa kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu katika klabu ya Inter Milan na kujiunga bila malipo msimu huu wa joto. (Fabrizio Romano)
Kiungo wa kati wa Manchester United Kobbie Mainoo atakubali kuitwa na Uingereza lakini anapanga kuweka mustakabali wake wa kimataifa wazi huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 18 pia akiweza kuiwakilisha Ghana. (Mail)
Imetafsiriwana Ambia Hirsi












