Tetesi za soka Ulaya Jumatatu 15.05.2024

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Zinedine Zidane
Iliyochapishwa

Bayern Munich wamewasiliana na Zinedine Zidane, ambaye bado hajarejea kwenye uongozi tangu aondoke Real Madrid miaka mitatu iliyopita, ili kupima nia yake ya kurithi mikoba ya Thomas Tuchel mwishoni mwa msimu huu. (Marca in Spanish)

Kocha wa zamani wa Bayern Munich, Monaco na Wolfsburg Niko Kovac ameibuka kama kocha anayetarajiwa kumrithi Jurgen Klopp katika klabu ya Liverpool. (Mail)

Newcastle wamemfanya kiungo mshambuliaji wa Nottingham Forest Muingereza Morgan Gibbs-White, 24, kuwa mmoja wa wachezaji inaowalenga msimu ujao. (Mirror)

Liverpool wanaweza kumsajili winga Mwingereza Marcus Edwards, 25, kutoka Sporting Lisbon kwa pauni milioni 30 msimu huu. (Football Insider)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Marcus Rashford

Marcus Rashford anatazamiwa kusalia Manchester United huku Paris St-Germain wakiweka wazi kuwa hawana nia ya kumsajili mshambuliaji huyo wa England mwenye umri wa miaka 26. Sun)

Chelsea wanatayarisha ofa ya kumnunua kiungo wa kati wa Uholanzi Teun Koopmeiners, 26, baada ya kutuma maskauti kumwangalia wakati wa ushindi wa Atalanta wa Ligi ya Europa dhidi ya Liverpool. (Sportmediaset – Via italia)

Tottenham wanamfuatilia kiungo wa kati wa Leicester City Muingereza Kiernan Dewsbury-Hall na wanaweza kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 kwa kati ya £30m na £40m msimu huu. (Football Insider)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Dewsbury-Hall aliifungia Leicester City mabao matatu msimu uliopita

Tottenham pia wana nia ya kumsajili beki wa Italia Riccardo Calafiori, 21, kutoka Bologna msimu wa joto. (Tuttosport – In Italy)

Winga wa Uhispania Bryan Gil anaweza kutaka kuondoka Tottenham msimu ujao na Spurs itakuwa tayari kumruhusu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 kuondoka kwa uhamisho wa kudumu. (Give Me Sport)

Everton wanataka kumsajili kiungo wa kati wa Ubelgiji Leander Dendoncker, 28, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo Napoli, kutoka Aston Villa msimu huu. (Football Insider)

Barcelona wana imani kuwa beki wa kati wa Uhispania Pau Cubarsi, 17, atasaini mkataba mpya licha ya kutakiwa na baadhi ya klabu kubwa barani Ulaya. (Mundo Deportivo – In Spanish)

.

Chanzo cha picha, Twitter

Maelezo ya picha, Yamine Lawal

Barca pia wanafanya kazi ya kuongeza mkataba wa Lamine Yamal, hata iwapo Paris St-Germain itafuatilia nia yao kwa kutoa ofa kubwa kwa winga huyo wa Uhispania mwenye umri wa miaka 16. (Nicolo Schira)