Tetesi za soka Ulaya Jumapili 24.03.2024

Chanzo cha picha, Getty Images
Meneja wa Manchester United Erik ten Hag anaamini kuwa bado ana muda wa kumshawishi mmiliki mwenza wa klabu Sir Jim Ratcliffe kuendelea naye, licha ya majadiliano kufanyika kuhusu mrithi wake. (ESPN)
Newcastle United wanataka kumsajili beki wa kati wa Ureno Goncalo Inacio, 22, na mlinzi wa Ivory Coast Ousmane Diomande, 20, kutoka Sporting Lisbon lakini vikwazo vya kifedha vinaweza kuwazuia. (Fichajes - In Spanish)
Barcelona wana nia ya kumsainisha mlinzi Pau Cubarsi mwenye umri wa miaka 17 kwa kandarasi mpya kufuatia mafanikio yake katika kikosi cha kwanza, huku kukiwa na nia ya Ligi ya Premia. (Marca in Spanish)

Chanzo cha picha, Getty Images
Arsenal wanamfuatilia kiungo wa kati wa Uingereza Morgan Gibbs-White huku Nottingham Forest wakifikiria kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 ili kusawazisha vitabu vyao. (Star)
Rais wa Barcelona Joan Laporta alisema klabu hiyo ilikataa ofa ya euro 200m (£172m) kwa mshambuliaji wa Uhispania Lamine Yamal, 16. (Marca)
Klabu ya Saudi Arabia Al-Hilal inataka kumnunua winga wa Brazil Raphinha kutoka Barcelona na wako tayari kutoa ofa ya hadi euro 100m (£86m) kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27. (Sport - In Spanish )

Chanzo cha picha, Getty Images
Fowadi wa Ufaransa Kylian Mbappe hatatangaza kuhama kwake kutoka Paris St-Germain hadi Real Madrid huku kukiwa na uwezekano wa timu hizo mbili kukutana kwenye Ligi ya Mabingwa. (Sport - In Spanish)
Juventus wanatafuta kumnunua fowadi wa umri wa miaka 22 Mason Greenwood, ambaye yuko kwa mkopo Getafe kutoka Manchester United na ambaye mkataba wake na klabu hiyo ya Old Trafford utakamilika 2025. (Gazzetta dello Sport - in Italian).
Eintracht Frankfurt hawana uwezekano wa kuamsha kipengele cha pauni milioni 8.5 kubadilisha kiungo wa kati wa Uholanzi Donny van de Beek, 26, kutoka Manchester United hadi uhamisho wa kudumu. (Bild, via Goal)
Manchester United haitatafuta kumsajili mchezaji aliyecheza kwa mkopo wa Fiorentina Sofyan Amrabat kutoka Fiorentina, lakini kiungo huyo wa kati wa Morocco mwenye umri wa miaka 27 analengwa na AC Milan na Juventus.(Tuttosport via Football Italia)
Beki wa kati wa Juventus, Gleison Bremer ndiye anayelengwa na Manchester United msimu ujao, huku beki huyo wa Brazil mwenye umri wa miaka 27 akiwa na kipengele cha kutolewa cha euro 50m (£43m) katika mkataba wake. (Corriere dello Sport - In Itali)
Napoli hawana nia ya kuanzisha chaguo la £7.7m kumnunua kiungo wa kati wa Ubelgiji Leander Dendoncker, ambaye yuko kwa mkopo katika klabu hiyo ya Italia kutoka Aston Villa.(Fabrizio Romano).












