Tetesi za soka Ulaya Jumamosi tarehe 09.11.2024

Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 3

Kocha wa klabu ya Fenerbahce Jose Mourinho, 61, bado anamipango ya kurejea katika Ligi ya Primia, na kwa sasa analenga kujiunga na klabu ya Newcastle endapo mkufunzi wake Eddie Howe, 46, ataikacha klabu hiyo yenye maskani yake katika uwanja wa St James' Park. (Guardian), external

Shirikisho la Kandanda la Brazil (CBF) have limempigia simu mara kadhaa mwaka huu kocha wa Manchester City Pep Guardiola katika harakati za kumshawishi Mhispania huyo mwenye miaka 53 kuinoa timu ya taifa ya Brazil. (The Athletic)

Guardiola huenda akabadili msimamo wake wa kutopenda kufanya usajili katika dirisha la mwezi Januari ili kukabiliana na changamoto zinazoikumba kikosi chake kwa kumuwania kiungo mkabaji kutoka Brazil anayekipiga katika klabu ya Atalanta Ederson, 25. (The I - subscription required)

Newcastle wanasuka mpango wa kumsajili mshambuliaji wa Brentford na timu ya taifa ya Kameruni Bryan Mbeumo, 25, kwa dau la pauni milioni 50. (Football Insider), external

Bayern Munich wanamfuatilia mshambuliaji wa klabu ya Sporting na timu ya taifa ya Sweden Viktor Gyokeres, 26, ambaye anaweza kuruhusiwa kuondoka klabuni mwishoni mwa msimu kwa dau la wastan wa pauni milioni 60. (Sky Germany),

Arsenal inapanga kusubiri mpaka mwishoni mwa msimu ili kusajili mshambuliaji mpya na si katika dirisha la usajili la mwezi Januari. (Independent)

Matumaini yamerejea ndani ya kikosi cha Manchester United wakati kocha mpya wa klabu hiyo Ruben Amorim akitarajiwa kuanza majukumu yake hivi karibuni. coach. (Manchester Evening News)

Kocha Hansi Flick amefanikiwa kurejesha ubora wa Barcelona kwa kuweka kanuni kali za kinidhamu, ikiwa ni Pamoja na kuwatupa benchi wachezaji wanaochelewa. (Marca - in Spanish)

Barcelona wanapanga kuwapiku Liverpool katika kinyang’anyiro cha kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Ujerumani Karim Adeyemi, 22, kwa kumjumuisha wing awa Uhispania Ferran Torres, 24, kama sehemu ya uhamisho huo. (Fichajes - in Spanish)

Wachezaji wa zamani wa Arsenal Tomas Rosicky na Per Mertesacker wanajadiliwa na uongozi wa klabu hiyo wakati akitafutwa mbadala wa Edu ambaye amebwaga manyanga ya mkurugenzi wa ufundi. (Footmercato - in French), external

Imetafsiriwa na Athuman Mtulya