Seneti ya Marekani yaidhinisha muswada wa kwanza wa udhibiti wa bunduki

The proposals fall far short of what many Democrats and activists have called for

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Mapendekezo yana mapungufu ya kile ambacho Wademocrat na wanaharakati wamekuwa wakikitaka
Iliyochapishwa

Bunge seneti la Marekani limeidhinisha muswada wa udhibiti wa silaha- ikiwa ni sheria muhimu zaidi kuhusu silaha kuwahi kuidhinishwa kwa karibu miaka 30.  

 Warepublican kumi na watano walijunga na Wademocrat katika bunge la congress kuidhinisha hatua hiyo kwa kura 65 dhidi ya 33 zilizopinga.   

 Hii inafuatia ughasia kubwa za ufyatuaji risasi  uliotokea katika soko kubwa lililopo   Buffalo, New York, na  kwatika shule ya msingi iliyopo Uvalde, Texas, uliosababisha vifo vya watu 31.

 Muswada huo utatakiwa kupitishwa katika Bunge la awakilishi kabda Rais Joe Biden kuweza kuusaini kuwa sheria.

 Hii inaweza kutfanyika katika kipindi cha siku kadhaa.

 Licha ya kwamba ni muhimu, mapendekezo  ya sheria hii yanamapungufu ya kile ambacho Wademocrat na wanaharakati wamekuwa wakikiomba.

 Sheria mpya inajumuisha  uchunguzi wa kina wa historia  kwa wanunuzi wa silaha wenye chini ya miaka  2 na dola bilioni 15 (£12.2bn) zitatolewa  na  serikali ya shirikisho kwa ajili ya kudhamini mpango wa afya ya akili na kuboresha usalama wa shule.   

 Aidha unaoa  wito kwa ajili ya udhamini ili kuyashawishi majimbo kutekeleza sheria za kuondoa silaha mikononi mwa watu wanaoangaliwa kama  tisho.   

 Na unamaliza kile kinachoitwa   "boyfriend loophole" kwa kuzuwia mauzo ya bunduki kwa wale waliopatikana na hatia ya kuwanyanyasa wenza wao wa kimapenzi  ambao hawajaolewa.  

 Seneta wa Republican  wa jimbo la Tecxas John Cornyn, ambaye alikuwa mmoja wa walioongoza mazungumzo kuhusu muswada huo, alisema katika kikao cha bungee kwamba muswada huo utawafanya Wamarekani kuwa salama. 

 "Siamini katika kutofanya lolote katika kukabiliana na na  kile tulichokishuhudia    katika Uvalde na kile tulichokiona katika jamii nyingi ," Bw Cornyn alisema.

 "Kutofanya chochote ni kushindwa kutekeleza wajibu wetu kama wawakilishi wa watu wa Marekani hapa katika Seneti ya Marekani."

 Kura ya Alhamisi ilipigwa katika siku ambayo Mahakama ya juu zaidi ya Marekani ilibasheria ya New Yoek inayodhibiti ubebaji wa bunduki, ikiwa ni moja ya maamuzi muhimu zaidi kuhusu silaha kuwahi kupitishwa kwa zaidi ya muongo. 

 

Unaweza pia kusoma: