Mabomu ya kutawanyika nchini Ukraine: 'Kila kitu karibu nasi kilianza kulipuka'

Oleksandr Avdeienko na familia yake wamekuwa wakijificha katika nyumba yao kwa wiki tatu.
Nje kulikuwa na mashambulio ya mara kwa mara ya makombora ya Urusi na ufyatulianaji risasi
"Ilikuwa karibu saa 08:00 (saa za nyumbani). Kulikuwa na makabiliano ya risasi mjini. Ilikuwa karibu sana," sanasema Oleksandr.
"Lakini wakai huo, hakukua na huduma ya usambazaji maji katika mji huo. Yale maji ya kunywa tuliyokuwa nayo yalikua yameanza kuisha."
Mji wa Chernihiv kaskazini mwa Ukraine ulishambuliwa siku ya kwanza ya uvamizi wa Urusi Februari 24. Maji na umeme ulitolewa kwa vipindi fulani.
Wiki tatu baadaye, tarehe 17 Machi, Oleksandr na mke wake Nataliia walikubaliana kwamba mmoja wao alihitaji kutoka kwenda kutafuta maji.
Aliyesalia alikuwa ampelekea mtoto wao wa kiume wa miaka sita Danya, katika makazi ya kujikinga dhidi ya mabomu.
Wakati familia ilipotoka nje tu walisikia mlio wa sauti angani na mara wakaona moshi mweupe ukifuka ".
"Baada ya hapo kila kitu kilicho wazunguka kilianz akulipuka. Kila ulikogeuza kichwa chako, milipuko na glasi zilikuwa zikianguka," alisema.
Baada ya kuangushwa chini na mlipuko huo, Oleksandr anasema vipande vidogo vya vichuma hatari vilianza kumnyeshea kama mvua.

"Uchungu niliyohisi ulikuwa mbaya sana. Nilidhani mguu wangu umepuliwa."
Aligeuka taratibu na kumuuliza: "Danya, uko sawa mwanangu?"
Danya alijibu kwamba yuko sawa.
Oleksandr kisha akamgeukia mke wake. "Damu ilikuwa ikitaririka kutoka kwa paja lakethigh," anasema Oleksandr.
Alichukua mkoba wake na kukata kambaili ajaribu kumfunga ili asiendelee kuvuja damu.
Kwa bahati nzur, mmoja wa jirani yao alifika eneo la tukio na kumilia katika kituo cha polisi kilicho karibu kupata usaidizi.
Dakika chache baadaye , magari kadhaa yaliwasili. Oleksandr anasema Nastaliia alilia akisema, "Tafadhali msinikate mguu "alipoinuliwa kuingizwa kwenye gari.
Oleksandr kisha akamuangalia mwanawe kwa mshtuko. Nguo za Dany zilikuwa zimechanika.
Alipomwambia ainue nguo yake juu, hofu ya, Oleksandr ilithibitishwa. Kulikuwa na kidonda kibaya chenye damu kwenye mgongo wa mwanawe.
Familia iliwekwa kwenye magari tofauti na kuondolewa haraka katika eneo la tukio.
Safari ya upweke
Oleksandr sasa alikuwa peke yake, kuelekea hospitali ya Chernihiv Oblast inayoshughulikia ajali na hali ya dharura.
Anaelezea kuwa hospitali hiyo ilikuwa imefurika watu waliojeruhiwa huku mifuko ya kubeba maiti ikitundikwa kwenye kuta.
Kufikia 09:30 (saa za huko) mnamo Machi 17, Dk Tetyana Lukash alikuwa imepokea majeruhi 51 katika muda wa saa moja tu. Wengi anasema, walikuwa raia.
"Nakumbuka uso wa msichana mdogo, ambaye hata hajatimiza umri wa miaka 20 na mwanamke mzee aliyekuwa ameloa damu akiomba, Bwana 'waokoe wajukuu zangu'."

Dk Lukash anasema idadi kubwa kama hiyo ya majeruhi wote walio na majeraha sawa inaweza kumaanisha jambo moja tu. Lilikuwa ni shambulio la makundi ya kivita, anasema.
"Wagonjwa wote walikuwa na majeraha mengi, nguo zilizochanika, mifupa iliyovunjika na uharibifu wa tishu laini," anasema.
Licha ya machafuko hayo, Dkt Lukash kwa kujigamba anasema hakuna mtu aliyeachwa bila kuhudumiwa.
"Ilikuwa ni msururu usio na mwisho wa watu. Wengi walipelekwa moja kwa moja hadi kwenye jumba la upasuaji," anasema.

Dkt Serhii Yevtushek ni mpasuaji aliyemtibu Oleksandr.
"Tulimfanyia upasuaji [Oleksandr] huku tukishikilia tochi kwa mkono. Hatukuwa na umeme," anasema.
"Katika mazingira kama hayo hatukuweza kuchukua sampuli kutoka kwa kidonda ili kuchunguza ikiwa mgonjwa amepata maambukizi.
Walioshuhudia waliambia BBC kuwa asubuhi ya tarehe 17 Machi, mabomu mengi ya kutawanyika yalishambulia maduka kadhaa, ikiwa ni pamoja na duka la dawa na soko la mboga.
Uchunguzi tofauti
Kikosi cha mabomu cha jiji na idara za ujasusi za eneo hilo ziliiambia BBC kwamba mabaki ya vifaa vya kusafirisha mabomu yalikusanywa karibu na eneo ambalo watu walikuwa wakipanga foleni ya mkate na Hospitali ya Watoto mnamo 17 Machi.
Oleksandr Remenets, fundi wa kikosi cha mabomu kutoka Huduma ya Dharura ya Ukraine, alituonyesha eneo la kutupa risasi.
Anasema alikusanya moja ya mabomu ya kivita katika eneo la tukio tarehe 17 Machi, pamoja na shehena ya nguzo.

Mabomu ya nguzo ni ya kiwango cha juu sana, kumaanisha kwamba asilimia kubwa ya mabomu mara nyingi hushindwa kulipuka yanaporushwa.
Serikali ya Urusi imekanusha kutumia mabomu ya mtawanyiko nchini Ukraine. Ripoti za vyombo vya habari pia zimeishutumu Ukraine kwa kuzitumia angalau mara moja. Kyiv amekanusha tuhuma hii.
Urusi na Ukraine hazijatia saini mkataba wa kimataifa uliopiga marufuku utumiaji wa mabomu ya mtawanyiko mwaka wa 2008.
Licha ya hayo, Ukraine inasema utumiaji wa silaha hizi katika maeneo yenye wakazi wengi bado unakiuka sheria za kimataifa kwa sababu hawawezi kutofautisha malengo ya kiraia na mapigano.
Hii ndiyo sababu wataalam wa Ukraine wanachunguza mashambulizi kama uhalifu wa kivita unaoweza kutokea.

Andrii Prosniak ni Mpelelezi Mkuu wa Huduma ya Usalama katika eneo la Chernihiv.
Anasema wanategemea mwelekeo wa kurusha risasi kuthibitisha kwamba Urusi ilihusika na kutumia mabomu ya mtawanyiko huko Chernihiv.
"Kinadharia inawezekana kubainisha ni wapi silaha zilitoka ikiwa tunajua eneo la vikosi vyetu na nguvu za adui," anasema.
"Na taarifa hiyo tunayo."
Mashambulizi ya kiholela
Tulirekodi utumiaji wa mabomu ya mtawanyiko katika mashambulizi ya mabomu katika eneo lote la Chernihiv kwa angalau siku 10 tofauti.
Tulitembelea maeneo manne kati ya haya na tukakusanya ushahidi halisi ambao tumekuwa tukichanganua na wataalamu wa silaha.
Alama za athari tulizopata kwenye lami zingeweza tu kufanywa na mabomu ya mtawanyiko.
Mykhailo Zhyrokhov, mchambuzi wa kijeshi kutoka Chernihiv, anasema alama hizi, zikiunganishwa na uchafu kutoka kwa roketi zenyewe, na alama za athari kwenye majengo yanayozunguka, zote zinaonyesha matumizi ya mabomu ya mtawanyiko.
Mamlaka za mitaa, vyombo vya habari na mashirika ya haki za binadamu kote Ukraine yameripoti na kurekodi mamia ya mashambulizi kama hayo.















