Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 10.06.2024

tt

Chanzo cha picha, Getty Images

Iliyochapishwa

Everton wapo kwenye mazungumzo ya kumsajili mshambuliaji wa Albania Armando Broja, 22, kutoka Chelsea kwa mkataba wa £30m. (Ben Jacobs)

Wolves wamekubali mkataba wa kumsajili mchezaji wa Ureno Rodrigo Gomes, 20 kutoka Braga. (Athletic - usajili unahitajika)

Arsenal wameambiwa watalazimika kutumia pauni milioni 50 kumsajili kiungo wa kati wa Brazil Douglas Luiz mwenye umri wa miaka 26 kutoka Aston Villa. (Mirror)

Manchester City wanatazamiwa kumfanya kiungo wa kati wa Uingereza Phil Foden, 24, kuwa mchezaji wa Uingereza anayelipwa zaidi katika historia kwa kupandisha mshahara wake hadi £375,000 kwa wiki. (Sun)

Phil Foden

Chanzo cha picha, PA Media

Arsenal na Manchester United bado wanavutiwa na mshambuliaji wa Bologna Mholanzi Joshua Zirkzee, 23, ambaye pia anasakwa na AC Milan. (Sky Sports)

Bayern Munich wamewasilisha ofa mwanzo ya thamani ya takriban Euro milioni 30 kumnunua kiungo wa kati wa Fulham Mreno Joao Palhinha, 28. (Mail)

Mlinda mlango wa zamani wa Arsenal Jens Lehmann anasema hana uhakika kama kocha wa sasa Mikel Arteta ndiye mtu sahihi kuinoa klabu hiyo. (Telegraph - usajili unahitajika)

Mmiliki mwenza wa Wrexham Rob McElhenney hajakata tamaa ya mshambuliaji wa zamani wa Wales na Real Madrid Gareth Bale, 34, kusajiliwa na klabu hiyo ya League One. (Mirror)

tt

Chanzo cha picha, Getty Images

Klabu hiyo ya Wales pia iko kwenye mazungumzo na mlinda mlango wa Uingereza Arthur Okonkwo, 22, kuhusu mkataba wa kudumu baada ya kuachiwa na Arsenal. (Talksport)

Klabu ya Al-Nassr ya ligi kuu ya Saudia ioo kwenye mazungumzo ya kumsajili kipa wa Poland Wojciech Szczesny,34, kutoka Juventus . (Fabrizio Romano)

Newcastle wanataka kusajili mshambuliaji mwingine msimu huu wa joto. (Football Insider)

Kocha wa zamani wa Barcelona Xavi angependa kuwa mkufunzi wa klabu ya ligi kuu ya England. (Sport - kwa Kihispania)

Imetafsiriwa na Ambia Hirsi